Kwanini Spika hakumtetea Ester Matiko kuwa alimtuma Burundi

Inapendeza sana kama maamuzi haya kayafanya kwa kudata misingi na kanuni za kazi yake lakini hayatopaswa kupongezwa iwapo kupewa maelekezo kutoka kwengine
Nalog off
 
Kama Matiko alikuwa anajua masharti ya dhamana yake.....
Alipaswa kukataa kazi aliyopewa na Spika, na hata kama Spika angeamua kumchukulia hatua lakini isingekuwa kubwa kama ya hii ya Mahakama....

Vilevile, Matiko alikuwa na uwezo wa kumuandikia barua Spika kuwa awezi kutekeleza wito wake kutokana na masharti ya dhamana aliyonayo, hivyo spika kama alitaka kuendelea na nia ya kumtuma angemjibu kwa barua kumruhusu kuendelea na wito huko akipeleka nakala mahakamani.....

Hivyo iyo barua ya Spika ndiyo ingetumika kama ushahidi na siyo kumwita spika mahakamani......

Hakimu alipaswa kuipokea ile barua na kuthibitisha, khs kutumwa Burundi na Hon Speaker.

Hon Matiko alikuwa hana sababu ya kutotii wito wa kwenda safari aliyotumwa na Hon Speaker.

Wana haki zao za kikatiba,
Isome vzr hukumu ya Judge Hon S R.
 
Amfungulie kesi na kudai fidia kwa kushindwa kumtetea ili hali alijua fika sababu ya kutokuwepo kwake nchini lakini akaamua kukaa kimya.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Sam Rumanyika amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha Mbowe na Matiko hawakuruka masharti ya dhamana kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri.

Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.

Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.
 
Ester alienda kufanya uhuni wake huko na mabwana zake hakutumwa na Tulia anaongea hivo ili kumhadaa mume wake

Umeamua kujivika ujinga.
Ni bora ungekaa kimya kuliko kuandika non sense.

Hon Tulia ni Deputy Speaker,
Hon Ester M alitumwa na Hon Speaker.
 
tatizo humueleweki nyie chadema, walipokua mahabusu mlikua mnadai mahakama itende haki, mahakama imetenda haki mnaanza kuishutumu serikali kwamba ndio iliwaweka ndani...hao watu wenu mahakama imewaonea huruma tu japo hamuwezi amini, rais akiamua kuwaweka ndani kama mnavyo dai mnaweza msiwaone uraiani hadi 2025.

kuachiwa hao viongozi wenu ni kwa hisani ya watu wa mahakama na acheni tabia yenu chafu ya kuihusisha serikali/rais katika kesi zilizoko mahakamani.
Nilitaka nikujibu ovyo....
Sema ni kipindi cha kwaresma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo unayoeleza unafikiri Jaji hayajui,

kama umeruka dhamana kinachotakiwa ni kwenda na evidence kitu ambacho Ester alifanya, kosa lililofanywa na hakimu Mashauri ni kukataa kupokea evidence, kwa hiyo Mashauri hakupata muda wa kumuuliza matiko kujua kama ombi lake kwa spika kutoenda Burundi lilikataliwa ama la.

Kilichotakiwa ni mahakama kupokea ushahidi then ndipo hayo maelezo mengine ya kuomba ruhusa au kwa nini hukuomba kubadilishwa yangefuata, halafu hiyo inategemea pia na umuhimu wa kazi uliyotumwa.
Sheria haziko kama ufipa wanavyotafsiri. Jamaa kakueleza taratibu zilivyo, ukipata udhuru first ni kutoa taarifa kuwa ninahudhuru sitaweza fika siku flani sio usifike then uje na sababu baadae. Sio kweli kwamba Matiko alitumwa ghafla, maana yake alikua na muda wa kumweleza speaker kuwa tarehe hizo natakiwa niwe mahakaman na hapo speaker alikua na option ya kuchagua mwingine au kuandika barua kueleza Mahakama juu ya kutumwa kwa Matiko au taratibu zozote za kisheria zingefuatwa. Lkn inaonesha Matiko hakutoa taarifa kuwa nina kesi mahakaman na aluchukulia hiyo nafasi kama advantage ya kutohudhuria mahakaman. So biashara ya kumwita speaker athibitishe kisheria haina nguvu hata kidogo coz speaker anaweza sema ndio nilimtuma lkn hakuniambia kuwa anakesi mahakaman kias mm nimteue mwingine

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Akisoma uamuzi huo, Jaji Sam Rumanyika amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha Mbowe na Matiko hawakuruka masharti ya dhamana kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri.

Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.

Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.
Hakumtetea mahakamani au JF? Maana mahakamani kuna utaratibu wa kuwasilisha utetezi. Mpaka utetezi huo utakikane na mahakama, ila JF unaloloma tuu muda wowote.
 
Back
Top Bottom