mdhalendo
JF-Expert Member
- Dec 14, 2011
- 282
- 273
Wadau wa JF.
Leo ningependa tujadili kidogo hali ya afya ya akili inayoendelea kuwatafuna vijana wetu mitaani bila jamii kuangazia.
Leo ni hali ya kawaida kukuta kijana teenager anayesoma sekondari au chuo kikuu akilalamika kuwa na msongo mkubwa wa mawazo au kitaalamu inaitwa Sonona (depression). Hali hiyo imepelekea baadhi yao kujizuru hadi kufikia hatua ya kujaribu kujiua.
Swali la kujiuliza: Nini kimepelekea ongezeko kubwa la vijana wadogo kuwa na depression: Je, ni kukosa malezi mazuri?, kushindwa kufikia ndoto na malengo yao? Je, mitandao ya kijamii imesababisha wao kutamani maisha ya kifahari wanayoyaona kwenye 'status' za wenzao? Je, ni hali ngumu za kiuchumi kwenye familia zao? Je, ni changamoto za kimapenzi?
Leo ningetamani nipate maoni yako, nini kinachangia ongezeko kubwa la sonona kwa vijana tofauti na ilivyokuwa miaka 15 na kurudi nyuma iliyopita Karibu tujadiliane pamoja
.