Kwanini siasa za Tanzania zimeegamia kujadili yaliyopita

Bunchari

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
489
531
Habari wakuu,

Sio lengo langu kufundisha mamlaka husika namna ya utendaji wa majukumu yao wala kuelekeza nini cha kufanya lakini mimi pia sio mwanasiasa, mahusiano yangu na serikali yapo upande wa ulipaji kodi pekee nawapa chao nabaki na changu.

Mapema leo nimeona nami nitoe maoni yangu kuhusu kinachoendelea katika medani za kisiasa na serikali kwa ujumla, kwanini muda mwingi mnamzungumzia JPM tatizo nini? Kwanini msitumie huo muda na nguvu kumpa ushirikiano aliepo madarakani ili kuua mijadala ya kulinganisha uongozi kwamba huyu mbaya huyu mzuri.

Najua JPM alikuwa mtu mbaya kwa makundi fulani ya watu na mkombozi kwa baadhi,nimejaribu kufanya utafiti ninyi watumishi wa umma mnapenda majungu ndio mmekua chanzo cha hizi kelele za kulinganishana,sote tunajua jamaa aliziba mianya ya pesa za chap chap kwaupande mwingine net amount due hazipo vizuri lazima jamaa angeonekana mbaya tu...Wacha jamaa apumzike kibaya kwako kizuri kwa wengine na kizuri kwako kibaya kwa wengine.

Viva Tanzania mama anaupiga mwingi nchi inasonga,vituo vya afya kila mahali.
 
Ni AIBU kubwa kupambana na MAREHEMU huku ukijua nawe ni marehemu TARAJARI.

Ubadhilifu wa dhahili umeshamiri kwasababu wanaamini mnoko hayupo! Ukiibia Serikali unaonekana mjanja jamii inakusifu.

Viongozi SASA wameamua kujijenga haraka haraka kufidia hasara Kwa kipindi kilichopita.

Miradi binafsi inakuwa Kwa Kasi
 
Sahihi
 
Sababu hawana sera zao kuisaidia nchi. Sera ni divide and rule kuwatenganisha Watz ili kuwatawala na kutumbua pesa zao kirahisi.
 
Hao wanaompenda nao waje wamsifie au kumtetea, wale waliokuwa wanaona ni ibilisi ngoja wampe ukweli wake.
 
Ni AIBU kubwa kupambana na MAREHEMU huku ukijua nawe ni marehemu TARAJARI.

Ubadhilifu wa dhahili umeshamiri kwasababu wanaamini mnoko hayupo! Ukiibia Serikali unaonekana mjanja jamii inakusifu.

Viongozi SASA wameamua kujijenga haraka haraka kufidia hasara Kwa kipindi kilichopita.

Miradi binafsi inakuwa Kwa Kasi
Hata dhalimu aliiba serekalini, alipokuwa akitendea wengine ukatili na kupora haki ya watu kupata viongozi wawatakao, hakujua kuwa iko siku atakuwa marehemu?
 
Wanaotaka kuimba nyimbo za kumsifu,na waendelee.Na wanaoona bado wana dukuduku na marehemu nao waendelee kumsimanga.Msiingiliane wala kuoneana gere katika utendaji wenu.
 
Ukiwa kiongozi ata utende mema vipi, baya 1 tu litakuondolea sifa nzuri utaonekana ww mbaya.

Hawajui kuwa yule anaonekana mbaya ndiye hufanya juhudi kubwa ya kuiokoa nchi na yule anayeonekana mzuri ndiye mtu wa 1 kuiangamiza nchi, pindi mkijua nyendo zake.

Watanzania hawajawahi kumkubali kiongozi wao kutwa kuwakosoa tu, Kila aliyeingia madarakani., ilhali Ayo ni mapungufu tu ya kawaida ya Kila mwanadamu.
 
Dunia hiihii usikosolewe?Watu wamepagawa na maisha.Halafu,kusimangana kunajenga afya kwa kuondoa visirani moyoni.
 
Hao wanaompenda nao waje wamsifie au kumtetea, wale waliokuwa wanaona ni ibilisi ngoja wampe ukweli wake.
Hakuna ukweli hapo,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni jamaa kafanya mengi mazuri.Kama mtu alikufa kama wanavyodai ni uzembe wake mwenyewe V8 ipo speed 180 full light kitamba chekundu hewani unaleta mzaa barabarani utagongwa tu hakuna namna
 
Ukiwa kiongozi ata utende mema vipi, baya 1 tu litakuondolea sifa nzuri utaonekana ww mbaya.

Hawajui kuwa yule anaonekana mbaya ndiye hufanya juhudi kubwa ya kuiokoa nchi na yule anayeonekana mzuri ndiye mtu wa 1 kuiangamiza nchi, pindi mkijua nyendo zake. Watanzania hawajawahi kumkubali kiongozi wao kutwa kuwakosoa tu, Kila aliyeingia madarakani., ilhali Ayo ni mapungufu tu ya kawaida ya Kila mwanadamu.

Ukifanya vizuri inamaanisha utapingana na maslahi mengi ya watu wanaoilimiki nchi.

Uhalisia ni kwamba matajiri wa ndani na nje ndio wenye uwezo, wenye kumiliki rasilimali zetu nyingi, media, sekta zote muhimu.

Ni wachache ukilinganisha na wengi wa Watz maskini.

Ukitaka kuzigawanya hizo pesa, nafasi, rasilimali, ajira, vipato vya wengi kiuhalisia utapingwa na wenye nguvu.
 
Hao wanaompenda nao waje wamsifie au kumtetea, wale waliokuwa wanaona ni ibilisi ngoja wampe ukweli wake.
Ukiona mtu yeyote alimpenda Magufuli au anamtetea basi ujuwe ni mnyonya damu muabudu mizimu na mtu asiyestaarabika wala hajui dunia ya wastaarabu watu wanaishi vipi.
 
Wazalendo na wajamaa popote ulimwenguni ndio walivyo,hakuna namna tukubaliane na hali tuachane na jamaa kafanya mengi mazuri.
Dunia hiihii usikosolewe?Watu wamepagawa na maisha.Halafu,kusimangana kunajenga afya kwa kuondoa visirani moyoni.
 
Ukifanya vizuri inamaanisha utapingana na maslahi mengi ya watu wanaoilimiki nchi.

Uhalisia ni kwamba matajiri wa ndani na nje ndio wenye uwezo, wenye kumiliki rasilimali zetu nyingi, media, sekta zote muhimu.

Ni wachache ukilinganisha na wengi wa Watz maskini.

Ukitaka kuzigawanya hizo pesa, nafasi, rasilimali, ajira, vipato vya wengi kiuhalisia utapingwa na wenye nguvu.
Na huo ndiyo ukweli
 
Kwa hiyo jumba bovu umeangushia watumishi wa umma, anyway hawajalalamika kihivyo sana ingawaje aliondoka bila kuwatimizia ahadi ya nyongeza kubwa aliyoahidi....
 
Ukiona mtu yeyote alimpenda Magufuli au anamtetea basi ujuwe ni mnyonya damu muabudu mizimu na mtu asiyestaarabika wala hajui dunia ya wastaarabu watu wanaishi vipi.

Kwa hiyo jumba bovu umeangushia watumishi wa umma, anyway hawajalalamika kihivyo sana ingawaje aliondoka bila kuwatimizia ahadi ya nyongeza kubwa aliyoahidi....
watumishi wengi salary slip zao zimesinyaa jamaa alipobana mianya ya pesa za chap chap balaa likaanzia hapo...wapotezee maisha yasonge tu.
 
Wazalendo na wajamaa popote ulimwenguni ndio walivyo,hakuna namna tukubaliane na hali tuachane na jamaa kafanya mengi mazuri.

Tofautisha wajamaa na Wanaojali maisha ya wengi. Wapo wengi wanapenda mixed economy lakini ni waadialif u na waaminifu.
 
Back
Top Bottom