Kwanini shirika la TBC lisianzishe channel ya wild animals?

Swizzy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
773
511
habari wanaJF!!

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kwanini Shirika la utangazaji TBC halianzishi channel inayo jitegemea itakayo kuwa inahusu WILD ANIMALS wa hapa Tanzania.

Kama imeweza kuanzisha Channel ya TBC2 inayo husu mambo ya muziki tu kwanini ishindwe kuanzisha WILD ANIMALS channel?.

Nimekuwa nikiangalia channels mbalbali za nchi za nje zinazo husu wild animals, lakini cha kushangaza asilimia kubwa ya contents hizo nyingi ni za africa hususani kwenye hifadhi za hapa Tz. Kama tuna hifadhi, mbuga, bahari, maziwa, mito, milima n.k kwanini TBC isikamatie fursa ya kuanzisha hii channel ya Wild Animals?

Endapo hiyo channel ikianzishwa shirika la utangazaji la TBC litajulikana kimataifa endapo ving'amuzi vya kimataifa (mfano Dstv n.k) vikiingia ubia na TBC kupitia hiyo channel. Pia hiyo channel itasaidia kulitangaza taifa letu na kuvutia watalii, kukuza lugha ya Kiswahili bila ya kusahau ajira zitaongezeka.

.....Naomba kama uongozi wa TBC unasoma huu uzi ujaribu kuliangalia hili kwa undani, pia kama kuna mwingine anamaoni kuhusiana na huu uzi ana karibishwa....

[HASHTAG]#Ahsante[/HASHTAG]
 
Wazo lako linastahili uliuze kwa 100 millions sema bongo watalifanyia kaz afu hutakua recognized amini nakwambia watasoma huku na watafanyia kazi. Asilimia kubwa ukiangalia animal planet documentary nyng zimerekodiwa serengeti hivyo cc tunaweza sana kumiliki hii channel na ikawa maarufu
 
Tanzania Tourist Board ( TTB), EAC na TBC wangeweza kuandaa hii channel. Lakini sasa shida ni kwamba watu wanaangalia per diem za kwenda kwenye maonyesho Berlin, ujeruman miezi 2 (siku 60 × 500 USD @ day = 30,000 USD/person Hakuna la.maana wanaoenda huko wafanyakazi wa ubalozi washindwe kufanya, zaidi ya kusaini Mikataba ya hapa na pale na wahindi wa Mauritius.
 
ni kweli mkuu mi huwa naumia sana kuona channel za wenzetu wanatumia hifadhi zetu lakini sisi tuna shindwa
 
Wanasema wanajiendesha kwa hasala,kwa hiyobwako busy na Cheleko,ili wasipate hasala ndiyo maana wakaamua kuanzisha Tbc2 isiyo na kazi na kutoonyesha Bunge Mubashara
 
mkuu kama tido angendelea kuwepo mpaka leo naamini tungekuwa na Tbc 7 maana jamaa alikuwa mwanamkakati mzuri na ndio alofanikisha Tbc 2 kuwepo
sasa kwanini hawa walio baki wanashindwa kujiongeza/kulitanua shirika
 
Tanzania Tourist Board ( TTB), EAC na TBC wangeweza kuandaa hii channel. Lakini sasa shida ni kwamba watu wanaangalia per diem za kwenda kwenye maonyesho Berlin, ujeruman miezi 2 (siku 60 × 500 USD @ day = 30,000 USD/person Hakuna la.maana wanaoenda huko wafanyakazi wa ubalozi washindwe kufanya, zaidi ya kusaini Mikataba ya hapa na pale na wahindi wa Mauritius.
ni kweli mkuu wange ungana na kushirikiana vizuri lazima kitu kingefanyika
 
Duuh, kweli aisee. Mimi natazama sana channels za wanyama kama Animaux, Viasat Nature na NatGeo hawa wote wanaonesha wanyama wetu. Inauma sana, kuona Serengeti, ngorongoro crater, Maasai Mara na wanyama wake wakiwa source ya vipindi vya TV za mataifa mengine.
 
Wangeingia ubiya na NatGeo Wild. Hawa wamerekodi documentaries nyingi sana hapa Tz,ingekua rahisi zaidi kuliko TBC kuanza kutengeneza documentary nyingine.
wazo zuri lakini kumbuka hata sisi tunaweza kutengeneza hizo documentary, mbona kuna documentary ya kiswahili huwa inarushwa TBC1 na huwa wana iludia mara kwa mara kwasababu hawana zingine......
 
Bajeti finyu, lack of creativity. Unadhani zile kamera za TBC zina uwezo wa kuwanasa wanyama wakiwa in action? Zile ni za kuchukua matukio ya kawaida kawaida kama kuzindua mbio za mwenge!
ha ha ha!! wanaweza mkuu hata kwa mkopo tu/ kuingia ubia na makampuni mbalimbali
 
Back
Top Bottom