Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,445
- 7,812
Dkt. Ayub Rioba jana alipata fursa ya kuongea kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC 1 na kuelezea mambo mengi yanayolihusu shirika ikiwemo kuanzisha chaneli ya kiingereza kuwakabili watu wanaoisema vibaya Tanzania huko duniani. Pia lilikuwepo swali la tetesi za yeye kuachia ngazi TBC.
Mwandishi: Kuna tetesi kwamba una mpango wa kuliacha shirika la utangazaji Tanzania, tunaomba ufafanuzi.
Dkt. Rioba: Ndugu zangu, mimi nilijua mmeniita nije kuzungumzia shirika linapoelekea. Nitakuwa mtu wa ajabu endapo nitakaa hapa halafu naanza kuzungumzia sijui kuacha, unaachaje shirika?
Mimi labda nizungumze kitu kimoja, kwanza nimshukuru Mungu, tokea redio na televisheni zilipoletwa pamoja, mimi nimekuwa mkurugenzi mkuu ambae nimekaa muda mrefu kuliko wote. Wa kwanza alikaa miaka miwili na kitu, wa pili miaka mitatu, wa tatu miaka minne, mimi nimekaa sita ikifika Machi.
Mimi ni mwanahabari nafatilia mitandao ya kijamii sana lakini kabla sijateuliwa nilikuwa najaribu kubobea sana hili la matumizi ya social media na ICT. Nilikuwa nafundisha kwa mfano kitu kinaitwa 'Fake News'
Utajuaje kwamba hii si kweli, utakumbuka hata TBC tuliwahi kuingia mkenge, tukatangaza lihabari ambalo tumeliokota huko kwenye mtandao.
Kwa mfano unasoma kitu, mtu anasema aliyekuwa, kiingereza wamesema 'former'. Hivi mimi ni 'former'? Mimi ni mkurugenzi mkuu mpaka navyozungumza hivi.
Swala la Mheshimiwa Rais kuteua mtu mwingine ni suala lake, ni mamlaka yake atakavyoona yeye, haina maana mimi nitakaa hapa milele, ipo siku nitaondoka kwa namna yoyote ile lakini nawaomba watanzania wapuuze uvumi, haukuanza leo, umeanza tokea mwaka jana, nafikiri waupuuze tu.
Nilikuwepo ofisini mwaka jana nikaenda likizo, nikiwa likizo nikapata taarifa mdogo wangu amefariki. Nikaomba niongezewe siku angalau kukaa kwasababu ya msiba lakini mimi nimekuwa kazini siku zote. Lakini nanii unamuita bosi wako halafu unaanza kuuliza maswali ya kichokozi