Kulikuwa na faida gani ya kubadili jina la shirika letu la habari kutoka TVT (Televisheni ya Taifa) na kuitwa TBC (Tanzania Broadcasting Corporation)?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,319
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Kwanza ninaomba kuanza kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo pamoja na shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kwa kuamua kuwa Wazalendo kwa vitendo zaidi na kuamua kuboresha muonekano wa TBC.

Sasa hivi huwa nikiwa ninatazama TBC ARIDHIO ile saa moja jioni ni kama vile ninatazama CNN, BBC au Al Jazeera kwa maana camera na majukwaa ni ya kisasa, watangazaji wa kiume ni watanashati sana, hao akina dada ndio usiseme yaaani ni warembo saaaaana hususan yule dada wa kipare sijui mchagga wanamuita Elizabeth Mramba.

2583599_IMG_1312asd.jpg

I congratulate you guys once again. Huyo Elizabeth Mramba kama hajaolewa mpaka sasa ninaomba mwenye number zake anipe mara moja wakuu kwa maana sio kwa weupe ule. Hahahahahaaaa, I am joking.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kulikuwa na umuhimu gani wa kubadili jina la shirika letu la habari kutoka TVT (Televisheni ya Taifa) na kuitwa TBC (Tanzania Broadcasting Corporation)?

sdsdddddddd.jpg

Kama suala ni structual change (shake up) kwani isingeweza kufanyika bado ikibeba jina hilo hilo pamoja na logo ya TVT?

Kulikuwa na umuhimu gani wa kubadili jina la shirika letu pendwa, muhimu na la kizalendo katika kutangaza misimamo ya taifa hili imara barani Afrika lililojaa mashujaa na wachapakazi?

Ninajua kuna watu watakuja na hoja kwamba TBC ilizaliwa baada ya kuunganisha RTD (Radio Tanzania Dar Es Salaam) na TVT.

Lakini mbona kampuni ni moja ya Microsoft lakini bidhaa ni tofauti tofauti kama vile Windows, Office, Internet Explorer, Visual Studio na Xbox.

Kwanini TBC isingebaki kama TBC lakini ndani yake kuwe na TVT pamoja na Radio Tanzania? Kwanini walibadili majina? Kulikuwa na ulazima gani kufanya hivyo?

Mbona Serengeti, Manyara na Kilimanjaro ni vivutio vya kimataifa lakini bado vinabeba majina yale yale ya zamani na wazungu hawaja-ignore?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hoja yako ina logic kubwa.

Mimi binafsi ninahisi hapo kabla (kipindi cha JK) waliona TVT imekaa kisukuma sana(kishamba) wakaona bora iitwe TBC ili kuwa na muonekano wa kibeberu (kimataifa).

Sasa kwa kuwa umewashtua hapa JF, na kwa kuwa kwa sasa tuko kwenye zama za utawala wa kishamba, siku sio nyingi mzee Meko ataropoka kulikataa hilo jina la TBC na itarudishwa kuitwa TVT, halafu mataga hatashangilia.
 
TBC ilizaliwa baada ya kuunganisha RTD Radio Tanzania Dar Es Salaam na TVT Tanzania Television na kwakua vyombo hivyo viliunganishwa ili viwe chini ya shirika moja la umma ili kuleta ufanisi kwenye muundo wa utendaji na uendeshaji na uwe wa kisasa zaidi na kiushindani ndio Leo hii tuna TBC
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Kwanza ninaomba kuanza kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo pamoja na shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kwa kuamua kuwa Wazalendo kwa vitendo zaidi na kuamua kuboresha muonekano wa TBC.

Sasa hivi huwa nikiwa ninatazama TBC ARIDHIO ile saa moja jioni ni kama vile ninatazama CNN, BBC au Al Jazeera kwa maana camera na majukwaa ni ya kisasa, watangazaji wa kiume ni watanashati sana, hao akina dada ndio usiseme yaaani ni warembo saaaaana hususan yule dada wa kipare wanamuita Elizabeth Mramba.

I congratulate you guys once again. Huyo Elizabeth Mramba kama hajaolewa mpaka sasa ninaomba mwenye number zake anipe mara moja wakuu kwa maana sio kwa weupe ule. Hahahahahaaaa, I am joking.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kulikuwa na umuhimu gani wa kubadili jina la shirika letu la habari kutoka TVT (Televisheni ya Taifa) na kuitwa TBC (Tanzania Broadcasting Corporation)?

View attachment 1589921

Kama suala ni structual change (shake up) kwani isingeweza kufanyika bado ikibeba jina hilo hilo pamoja na logo ya TVT?

Kulikuwa na umuhimu gani wa kubadili jina la shirika letu pendwa, muhimu na la kizalendo katika kutangaza misimamo ya taifa hili imara barani Afrika lililojaa mashujaa na wachapakazi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mabadiliko ya kiteknolojia.
Kumbuka tulikuwa na RTD-Radio Tanzania Dar es salaam miaka ya nyuma zaidi.
 
Back
Top Bottom