Kwanini sherehe za muungano huwa hazifanyiki Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini sherehe za muungano huwa hazifanyiki Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Apr 26, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mie tangu nakuwa naona sherehe za muungano zinafanyika Dar ktk shamba la bibi kwa nini isafanyike kwa zamu na wapige gwaride Zanzibar?

  Mwenye jibu anisaidie

  =========
  UPDATE:

  Kwa mujibu wa Pos hii, sherehe za maadhimisho ya Muungano Kitaifa hufanyika kwa kupokezana -
  Kwanini sherehe za muungano huwa hazifanyiki Zanzibar?
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wewe nadhani fanya utafiti vizuri ndio urudi hapa
   
 3. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zamani walishawahi kufanyiaga huko, ila kwa sasa hawawezi tena kupeleka ujinga wao huko. Wapemba hawataki kabisa takataka inayoitwa Muungano.
   
 4. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wewe unayejua si uniambie
   
 5. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,756
  Likes Received: 8,025
  Trophy Points: 280
  Andika barua ya maombi
   
 6. Mukhabarat

  Mukhabarat Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ikifanyikia zenj, rais wa jamhuri ya muungano atadhalilika kwa kuwa ataingia kabla ya rais wa zanzibar halafu mizinga itapigwa mara mbili yaani kwa rais wa zenj na wa muungano vilevile itabidi kuingia gharama ya kubeba watu toka bara wakajaze uwanja sababu wazenj wengi hawatahudhuria!! yaani itakuwa haileweki mkuu wa nchi ni nani.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,511
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Hivi in reality kabisa by calling a spade a spade, ni kwa nini bara tunaubembelezea muungano wakati sioni tutakachopoteza? Someone plz use simple lingua for my pretty head to understand.
   
 8. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Usianzisha jambo ambalo hujafanya utafiti wa maana.... ninichojua huwa tunapaokezana kuandaa hizi sherehe, kama mwaka huu zinafanyika Dar, basi mwaka jana sizifanyika zanzibar.... soma hii utajua

  [h=2]JK kuongoza sherehe za miaka 47 ya Muungano[/h]


  By Mwinyi Sadallah  26th April 2011  Watanzania leo wanaadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanzanyika na Zanzibar. Sherehe za kilele cha maadhimisho hayo zitafanyika katika uwanja wa Amaan.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ataongoza sherehe hizo zinazotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
  Kwa mujibu wa ratiba ya maadhimisho hayo, milango ya uwanja wa Amaan itafunguliwa kuanzia saa moja ya asubuhi ili kutoa nafasi ya wananchi kuingia uwanjani na mapema.
  Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili uwanjani saa nne asubuhi akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, ambapo atakagua gwaride rasmi na kupigiwa mizinga 21 kabla ya kupokea gwaride litakalopita kwa mwendo wa pole na haraka.
  Ratiba haikuonyesha kama Rais Kikwete atahutubia katika sherehe hizo.
  Muungano wa Tanzania uliundwa April 26, 1964 kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar chini ya waasisi wa taifa Marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
  Sherehe hizo zinafanyika huku makundi ya wanzanzibari wakitoa maoni yao kwamba Muungano unahitaji ukarabati mkubwa ili kwenda na wakati. Juzi, Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, aliwataka wazanzibari kutovunja Muungano wa Tanzania kwa visingizio vya mawazo ya Katiba mpya na kuwataka wananchi kuepuka mijadala inayotoa ushawishi wa kukataa Muungano kwa kisingizia cha Katiba mpya.
  Manispaa ya Zanzibar imepambwa kwa bendera za taifa na mabango yenye ujumbe wa kudumisha Muungano wa Tanzania.
  Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimesema faida za Muungano haziitaji tochi kuonekana kwa vile umesaidia kujenga misingi ya umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Tanzania.
  Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, alipokuwa akitoa tathmini ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Alisema tangu kufikiwa kwa Muungano huo fursa za uwekezaji katika sekta ya biashara, kilimo na elimu zimekuwa zikiongezeka na kuongeza kipato kwa wananchi wa pande mbili za Muungano.
  Hata hivyo, alisema wananchi wengi Zanzibar bado hawajatumia fursa ya kuwekeza katika sekta ya kilimo katika mikoa ya Tanzania Bara kutokana na wengi wao kuwekeza zaidi katika sekta ya biashara ya maduka.  SOURCE: NIPASHE


   
 9. kilght

  kilght JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 626
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  zanzibar hawaufahamu mungano labda dr shek
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hamna mtu anataka huu muungano zaidi ya serikali zetu, watanganyika hawautaki wazenj hawautaki, inabidi twende na wakati this is 2012 kila nchi iwe na uhuru wa kufanya inachotaka...tutasemaje sisi ni nchi moja wakati kuna bunge mbili, serikali sijui ziko mbili na kama watanganyika nini faida ya kuungana na zanzibar....what do we really gain from them?
   
 11. n

  ngulla Member

  #11
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hii...!
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  toka lini mto ukameza bahari? au dagaa akameza papa?
   
 13. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,754
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  muungano ukivunjika tutaishi kama sudan kusini na sudan kasikazini.......acheni muungano ubaki hivi
   
 14. s

  seer Member

  #14
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha woga wewe Zanzibar kuna nini cha kugombania?
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  Apr 26, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkuu Wazenj ndio wanaoubembeleza Muungano, achana na waganga njaa wachache wanaodai kuwawakilisha Wazanzibari wote na kudai kuupinga!
   
 16. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,440
  Likes Received: 9,090
  Trophy Points: 280
  JF RAHA SANA! Ama kweli HAKUNAGA
   
 17. M

  Mtanganyika mweusi Member

  #17
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeina hiyo mkuu
   
 18. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,609
  Trophy Points: 280
  Hakuna Muungano. Kuna maungano. Hakuna Muungano wenye marais wawili ulimwenguni..
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,607
  Trophy Points: 280
  Tanganyika yetu tunaitarajia soon tumechoka kumezwa twaidai Tanganyika yetu
   
 20. T

  TKO Member

  #20
  Apr 26, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu sherehe zingefanyika Znz, kungekua hamna gwaride labda maandamano ya kupinga.
   
Loading...