Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,993
- 144,329
"SHEREHE ZA MUUNGANO MWAKA 2011"
Mvua yasitisha sherehe za Muungano
April 26, 2011
MVUA kubwa iliyoanza ghafla jana ilisitisha sherehe za maadhimisho yamiaka 47 ya muungano waTanganyikanaZanzibarkatika uwanja wa Amaan mjiniZanzibar.Sherehe hizo zilizoanza majira ya saa 3;00 asubuhi ziliingia dosari hiyo huku tayari mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshakagua gwaride na kujumuika na viongozi wenzake katika jukwaa kuu.
Viongozi wengine waliokuwepo katika sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Dk Ally Mohammed Shein, Makamu wake wa kwanza Seif Sharrif Hamad na makamamu wake wa pili Balozi Seid Idd.
Wengine waliokuwepo ni pamoja naMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anna Makinda, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange, Mkuu wa jeshi la Polisi Said Mwema, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rais mstaafu wa awamuya sita wa SMZ Dk Salim Amour.
Vilevile walikuwepo viongozi wa vyama vya siasakamavile mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Katibvu mkuu mstaafu wa CCM Philip Mangula, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia na wanadiplomasia wanaoziwakisha nchi zao nchini.
Rais Kikwete aliingia uwanjani hapo majira ya saa nne asubuhi akiwa kwenye gari la wazi na kuwapungua mamia ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo na baadaye kukagua gwaride.
Baada ya hapo gwaride lilipita mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa kasi na mwendo wa pole.
Ulipowadia wakati wa halaiki iliyoshirikisha wanafunzi 500, ndipo mvua ilianza kunyesha na baadaye kuivuruga kabisa sherehe hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo kipindi kilichokuwa kikifuata ni ngoma za asilia. Lakini mvua ilipozidi washereheshaji walitangaza kukatisha sherehe hiyo na viongozi wakaanza kuondoka.
Kauli mbiu ya sherehe hiyo ilikuwa ni "Miaka 47, tuwaenzi waasisi wetu, Tudumishe muungano, matunda ya miaka 47 ya mapinduzi na miaka 50 ya Uhuru, amani, utulivuna maendeleo ni matokeo ya muungano wetu, zilionekana kudorora hasa kutokana na mahudhurio hafifu ya wananchi. Sehemu mbalimbali za uwanja huo zilionekana kuwa wazi huku wafuasi wa CCM waliokuwa wamevaa sare nao wakiwa wachache.
Hata hivyo sherehe hizo zilionekana kudorora hasa kutokana na mahudhurio hafifu ya wananchi. Licha ya wanafunzi waliokuwa wamevaa sare nyeupe na wale waliovaa sawa na rangi za bendera ya Taifa na wafuasi wa CCM. Maeneomengine ya uwanja huo yalikuwa wazi.
Taarifa zaidi zinasema kuwa Serikaliilituma mabasi zaidi ya 20 vijijini ili kukusanya watu kwaajili ya kuhudhuria sherehe hizo, lakini hawakufika.
Hali hiyo imejitokeza huku kukiwa na manung'uniko mengi kutoka kwawananchi visiwani humo wakitaka muungano huo ufanyiwe tathimini upya.
Wakati huo huo, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar umetoa tamko kuhusu hali ya muungano.
Huku wakitoa ushahidi wa tume kadhaa zilizoundwa ili kutafuta maoni ya wananchi kama vile Tume ya Jaji Nyalali na ile ya Jaji Kisanga, jumuiya hizo zimesema kuwa muungano kati yaTanganyikanaZanzibarumekosa kukubalika ba Wazanzibari tangu siku yake ya kwanza hadi leo.
Huku wakikilaumu CCM kwa kuhodhimuungano, wamesema kuwa nguvu zaZanzibarkatika kama mshirika mmoja kamili wa muungano huo hazipio kwa kuongezewa mambo yamuungano nay ale yasiyo ya muungano yamekuwa yakiilemeaZanzibar.
"Kwa karibu miaka yote 47 muungano huu umekuwa ni miliki ya chama kimoja cha siasa cha CCM, ukitoa miaka michache ya 1964-1977".
Jumuiya hizo zimetaka kuwepo kwa majadiliano ya muungano ambapo wametaka pia nafasi ya Rais waZanzibarkatika muunganokamamakamu wa kwanza wa Rais.
"Mjadala wowote wa muungano ule urudishe nafasi ya rais waZanzibarkatika muungano na sio ilivyovyo hivi sasa ambapo Rais waZanzibarya maana wala amri yoyote ile katika muungano" imesema taarifa hiyo.
CHANZO: ZNZ KWETU
Ahsante kwa taarifa mkuu.Hata hivyo,bado hakuna uwiano na inaonekana zilifanyika kwa bahati mbaya tu!