kwanini serikali isitumie ile export levy ya korosho kuhakikisha kunakuwa na viwanda vya korosho?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Msimu uliopita wa Korosho inasemekana serikali ilichukua bilioni 250 hela ambayo ilikuwa ni ya wakulima wa korosho. Ni kama serikali iliokota hii hela au ilishinda biko maana hata haikuitarajia.
Kwanini serikali isitumie hiyo hela kuhakikisha kunakuwa na viwanda vya korosho nchi ili tuepuke habari ya kusumbuana na korosho ghafi. Ihakikishe korosho inapotoka nchini inakuwa packed na branded kabisa kwa ajili ya kuliwa.

Kuhakikisha namaanisha si yenyewe kujenga bali kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wakubwa wenye nia ya kuwekeza kwenye hivyo viwanda. Tukijenga viwanda tutaachana na kadhia nyingi sana zinazotokana na kusafirisha korosho ghafi. kama tuna sera ya viwanda basi tuionyeshe kwa vitendo.
 
Msimu uliopita wa Korosho inasemekana serikali ilichukua bilioni 250 hela ambayo ilikuwa ni ya wakulima wa korosho.
Acha kupotosha watu
Hakuna mkulima wa korosho anaeidai serikali
Hizo pesa zinakatwa ili kuendeleza zao la korosho na si kuwapa wakula kama unavyotaka kutuaminisha
 
Acha kupotosha watu
Hakuna mkulima wa korosho anaeidai serikali
Hizo pesa zinakatwa ili kuendeleza zao la korosho na si kuwapa wakula kama unavyotaka kutuaminisha
Ndiyo ilikuwa ya wakulima kwa mantiki hiyo.Kusaidia kupatikana mbolea, madawa, utafiti na kadhalik. Serikali ikaitoa huko.
 
Baaada ya hiyo pesa kuondolewa Sulphur na mbolea vimekuwa adimu na kwa bei kubwa.
Sulphur na Mbolea kaharibu Tizeba kwa kupokea kwake rushwa ili apendelee wasambazaji wake
Mwaka jana Tizeba ilibidi akurupushwe na Majaliwa akapewa siku saba kuondoa Mbolea bandarini ikabidi jeshi lisombe mbolea,watu kama hawa ni wa kunyongelea mbali
 
Wewe ni hewa.

Tusubiri kesho saa kumi jioni.
 
Back
Top Bottom