Waziri wa Biashara na Viwanda, Godfey Mwambe apiga marufuku taasisi zilizo chini ya Wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,706
2,000
Kwenye taarifa ya habari ITV leo ya saa mbili nimemsikia Waziri wa Biashara na Viwanda, Godfey Mwambe amepiga marufuku taasisi zilizo chini ya wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote ahimiza majadiliano badala ya funga funga. Amesema asisikie. Huo ni uhujumu uchumi

TRA na Taasisi zingine za umma mnaotembea na Makufuli na wino wa kuandika maduka na viwanda vya funga funga na mi X kibao mumesikia alichosema Mwambe?

Au huko kwenu kazi yenu kufunga biashara za watu?

====

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) amekutana na kufanya kikao na Menejimenti, wakuu wa idara, Vitengo na wakuu wa taasisi zilizochini ya Wizara hiyo kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja na kujadili utekelezaji wa bajeti hiyo katika kufikia malengo yaliyowekwa na kila taasisi kueleza malengo yake na vipaumbele vyake.

Akifungua kikao hicho cha siku mbili Waziri Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) amezitaka kila taasisi kuhakikisha zinafanya kazi kwa weredi na ubunifu mkubwa na katika bajeti yake kila taasisi ilenge katika miradi ya maendeleo na ipewa kipaumbele katika mipango ya utekelezaji wa bajeti yake.

“Nataka kila taasisi ihakikishe katika bajeti yake inalenga miradi ya maendeleo itakayosaidia kukua kwa taasisi, pia kila taasisi ipunguze kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima tunataka bajeti ilete tija” amesema Mhe. Mwambe.

Aidha amezitaka taasisi katika bajeti yake zilenge vipaumbele vichache ambavyo vitatekelezeka na sio kuweka vipaumbele vingi na bajeti ikawa haitoshi na fedha kutawanywa katika sehemu mbalimbali na mwisho wa siku hakuna matokeo katika utekelezaji wake.

Amezitaka taasisi kufanya kazi kiubunifu ambapo amebainisha kuwa Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa kuwa na fursa nyingi lakini bado hazijaleta tija kwa jamii na kuwa ni wajibu wa taasisi kuwa wabunifu nini kifanyike fulsa hizi ziwafikie walengwa hasa katika teknolojia.

“Ukiangalia katika kilimo hasa vijijini miaka nenda rudi tunatumia majembe ya mkono hiyo tija itapatikana sangapi na taasisi za utafiti zipo tu, kabla ya kuondoka katika hiki kiti nataka nizindue jembe lililobuniwa na CAMARTEC linaloleta mapinduzi” amesema.

Ameongeza kuwa “Hatuna kiwanda cha kutengeneza nguo lakini malighafi zipo na kila siku yanasafirishwa marobota mengi na mwisho wa siku tunauziwa nguo, wakati uwezo tunao wa kuwa na viwanda hapa nchini nataka hili lifanyiwe kazi haraka sababu nguvu kazi tunayo” amesema.

Ameitaka Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini TANTRADE kuja na mikakati ya kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya biashara hasa kwa wajasiliamali katika halmashauri zote ili kuwaendeleza wafanyabiashara hao kukua kutoka hapo walipo na kuwa na biashara kubwa.

Pia ameitaka TANTRADE kuwa na mikataba ya mazao ya kibiashara kama korosho badala ya kusubiri minada ambayo sio uhakika huku akitaka kuja na teknolojia inayofaa ili kuhakikisha korosho zote zinabanguliwa na sio kuuza korosho ghafi kuongeza thamani ya zao hilo.

Aidha amekitaka chuo cha elimu ya biashara CBE kubadili mtazamo wake na kuanza kutoa elimu itakayomuwezesha mwanafunzi anapomaliza chuo kwenda kuanzisha biashara na sio mtazamo wake wa sasa wa kuzalisha wasimamizi wa biashara huku akitaka kishirikiane na vyuo vingine katika kuboresha kada hiyo.

Kwa upande mwingine ameitaka tume ya ushindani kufanyakazi kwa ubunifu na si kufanyakazi kwa mazoea ili kuhakikisha inafanyakazi na wawekezaji vizuri na sio kuwa kero kwa wawekezaji hapa nchini na hasa katika kushughulikia mapungufu ya wawekezaji hapa nchini.

“Tume ya ushindani msiwasumbue wenye viwanda kuna njia nyingi badala ya kufunga biashara yake na huyo mwenye kiwanda kuona namna ya kumaliza mapungufu hayo sio kumfungia kiwanda chake” amesema.

Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amewataka watumishi katika wizara hiyo kufanya kazi kwa nidhamu na uadilifu mkubwa na kila kiongozi katika nafasi yake ajitathmini katika utendaji wake wa kazi kama anafaa kuwa katika nafasi aliyopo.

Aidha amekemea vitendo vya uchepushaji wa fedha za miradi ambapo taasisi nyingi zimekuwa zikitumia fedha kutekeleza miradi ambayo haikukusudiwa tangu awali huku akizitaka taasisi zinazotekeleza miradi inayofanana kushirikiana na sio kila taasisi inatekeleza kivyake wakati mradi ni mmoja.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amesema kikao hicho ni cha siku mbili kwa ajili ya kujadili vipaumbele vya kila taasisi na bajeti yake namna ya kutekeleza ili kuleta tija katika malengo ya kuanzisha taasisi hizo zilizochini ya Wizara ya Viwanda na biashara.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,215
2,000
Hongera Mh. Waziri ulikuwa msimamo wako thabiti tangu awali. Mara nyingi maafisa waandamizi wanatumia mianya kufunga biashara kusaka rushwa.

Mh. Biteko pata somo pia,toa nambari ipo shida wachimbaji wadogo,mialo,VAT leaching plant maafisa wako kufunga kwa vijisababu vidogo usafi mazingira, lebo usalama,uzio.... lengo wapatane rushwa kubwa.

Wanatumia seal za wizara kama silaha,bila hata muda kutoa notisi wala orodha makosa kwa wanaowakuta ,afisa ataacha nambari ya simu umfuate ofisini km kadhaa makao makuu wilaya.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,706
2,000
Hongera mh.Waziri ulikuwa msimamo wako thabiti tangu awali. Mara nyingi maafisa waandamizi wanatumia mianya kufunga biashara kusaka rushwa.
Mh.Biteko pata somo pia...
Kila wizara ijitathmini inayofungia biashara za Watu badala ya kusisitiza majadiliano zaidi
 

sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
4,573
2,000
Kwemye taarifa ya habari ITV leo ya saa mbili nimemskia Waziri wa biashara na viwanda Godfey Mwambe amepiga marufuku taasisi zilizo chini ya wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote ahimiza majadiliano badala ya funga funga.Amesema asisikie. Huo ni uhujumu uchumi....
Kwani TRA iko chini yake
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,484
2,000
Kwemye taarifa ya habari ITV leo ya saa mbili nimemskia Waziri wa biashara na viwanda Godfey Mwambe amepiga marufuku taasisi zilizo chini ya wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote ahimiza majadiliano badala ya funga funga.Amesema asisikie.Huo ni uhujumu uchumi...
Hadi sasa wengi sana washafunga na omeshawaathiri wengi sana.

Walishalalamika hawakusikilizwa
 

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
1,762
2,000
Kwemye taarifa ya habari ITV leo ya saa mbili nimemskia Waziri wa biashara na viwanda Godfey Mwambe amepiga marufuku taasisi zilizo chini ya wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote ahimiza majadiliano badala ya funga funga.Amesema asisikie.Huo ni uhujumu uchumi..
Rais anayajua haya?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,706
2,000
Hadi sasa wengi sana washafunga na omeshawaathiri wengi sana...

Walishalalamika hawakusikilizwa
Wawafungulie Biashara zao majadiliano yaendelee .Deni huwa halifungi mtu ni kesi tu ya madai .Hivi unafunga duka la mtu kisa kodi nk si mjadiliane tu ama ipunguzwe au alipe kidogodogo kwa installments Kufunga biashara that is too.much

Uchumi wa Marekani unaendeshwa kwa asilimia kubwa na small enterprises wengi humu hawajui hilo sio hayo ma big businesss ya kina Bill gates!

Huku kwetu small business haziwi encouraged kuwa nyingi na kodi ndogo .Mwajiri mkubwa marekani ni small business savabu kule kilimo na ardhi kinahodhiwa na watu wachache sana na kilimo chao ni highly mechanized kinatumia mitambo zaidi sio watu hivyo kimbilio la wengi ni kwenye small business na small industries.

Hapa kwetu sekta binafsi inaonekana tu kama ipo kwa bahati mbaya hivi.Kufunga biashara ya mtu afisa anachekelea!! Leo nimefunga biashara au kiwanda!!! anasahau kuwa hiyo biashara anayofunga ndicho chanzo kinacholipa mshahara wake na marupurupu anayo enjoy .Hivyo si tu anahujumu uchumi bali pia anajihujumu akiona mishahara haipandi au marurupu hayapandi aelewe chanzo ni yeye mwenyewe.Yatapandaje wakati unafunga biashara ni simple logic.

Pia anasahau huko kufunga kuna ndugu zake watageuka kuwa tegemezi kwake mfano wengine walikuwa wafanyakazi au walikuwa na tenda fulani kwenye kiwanda au hiyo biashara.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,706
2,000
Dawa ya kuzuia kufunga funga kienyeji ni kuwa maafisa wa chini wasifanye hiyo kazi wenye nguvu hizo awe waziri tu baada ya kujiridhisha independently kwa kutumia independent source nk ndipo ifungwe wao waandike na kupeleka proposal tu kwa mabosi wao. Mabosi wao wahakiki hilo kwanza kama ni kweli inatakiwa kufungwa halafu mapendekezo yapelekwe kwa mkuu wa taasisi. Na Mkuu wa Taasisi ajiridhishe kisha ampelekee waziri. Waziri ahakiki ndipo aidhinishe

Kufunga business au kiwanda ni issue seripus haitakiwi kuachiwa maofisa wa chini wao waruhusiwa level za kutuhusu uanzishaji ili kuondoa ukiritimba lakini kwenye kufunga no ni serious matter mkono wa waziri unahitajika huko kwingine wapeleke proposal tu

Kufunga biashara aachiwe waziri mhusika na mahakama tu
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,706
2,000
Nashauri wote waliofungiwa wafunguliwe majadliano yaendelee watafutwe waambiwe wafungue
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
30,421
2,000
Ni bora unifungie nikatafute mtaji nianze nikiwa sina madeni ya ajabu ambavyo nitatakiwa nilipe milele
 

carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,632
2,000
Hii safi sana, na Mh Kitila aliwaambia zile mamlaka za udhibiti zifanye kazi ya kuchochea ukuaji wa viwanda na uwekezaji. Sio kupambana kuzuia na kudhibiti tu. Kuitwa kwao mamlaka za udhibiti kumefanya mind set zao ziwe kwenye kudhibiti tu na kufungia uwekezaji.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,706
2,000
Hii safi sana, na Mh Kitila aliwaambia zile mamlaka za udhibiti zifanye kazi ya kuchochea ukuaji wa viwanda na uwekezaji. Sio kupambana kuzuia na kudhibiti tu. Kuitwa kwao mamlaka za udhibiti kumefanya mind set zao ziwe kwenye kudhibiti tu na kufungia uwekezaji.
Mawaziri wakae kwa pamoja wajadili hili swala waje na msimamo mmoja kuwa kufunga iwe ni kazi ya waziri sio ya ofisa yeyote wa chini .Huko kwingine watoe mapendekezo tu .Hili wala halihitaji bunge kukaa kubadili sheria sababu waziri ni mkuu wa taaasisi zote zilizo chini yake .Hivyo aweza fanya hiyo kazi yeye au katibu mkuu

Kama kuna ulazima wa kubadili sheria bungeni kwenye hili upelekwe haraka chini ya hati ya dharura .Kazi ya kufunga biashara kumuachia mtu wa chini sio sahihi.Waanzishe tu kufunga waachiwe mawaziri
 

carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,632
2,000
Hawa maofisa wa chini wanafanya makusudi kufungia biashara za watu kwa kukomoa tu. Wanafunga bila kujali...mwisho wa mwezi wanapokea mishahara yao hivyo hawajali maumivu wanayopeleka kwa wafanyabiashara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom