Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,838
Nimekuwa sielewi ni kwanini Serikali yetu inatumia fedha nyingi sana kuwajengea walimu nyumba za kuishi? Ni kwanini hiyo fedha tunayotumia kujenga nyumba za walimu tusiziwekeze kwenye kuboresha Shule zetu kwa kuwanunulia Wanafunzi vitabu au hata kuwapa watoto chakula cha mchana badala ya kuwajengea Walimu nyumba?
Nasema hivi kwa maana sielewi mantiki ya kuwajengea walimu nyumba wakati wao ni waajiriwa kama waajiriwa wengine wote na wanalipwa mshahara sasa ni kwa nini jukumu la wao wataishi wapi liwe la Serikali na siyo lao walimu wenyewe?
Mbona wafanyakazi wengine wa Serikali wanajitegemea kwenye malazi?
Ni kwanini Serikali isijitoe kwenye hili na kuwaacha walimu wapange nyumba au wajenge wenyewe kwa kuchukua mkopo kama wakipenda?
Kwa Hesabu tu ya kawaida haiwezekani kwa Serikali kuweza kuwajengea Walimu wote nyumba huku ni kujidanganya na kupoteza fedha ambazo zingeweza kutumika kuwahudumia wanafunzi ambao hawana mahitaji muhimu na isitoshe wanafunzi wengi wanatoka nyumba ambazo wazazi wao hata chanzo cha kipato hawana sasa ni kwa nini Serikali iwahudumie walimu ambao wana wanalipwa mshahara?