Kwanini serikali inatoa ajira nyingi kwa wahitimu wa dilpoma kuliko degree?

opondo

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
527
1,312
Nilikua napitia ajira za TAMISEMI za mwaka jana kwanini ajira zinakua na upendeleo sana? Unakuta pdf nzima imejaa wahitimu wa diploma au ni kwamba serikali inakwepa kuajiri wahitimu wenye degree ili kutoa mshahara mdogo?

Wanahisi wakichukua wenye degree basi itawatoka pesa nyingi?.

Mfano ajira za ualimu mwaka Jana zilizotoka waliochukuliwa wengi 2019 kwenye masomo ya physics na chemistry na mathematics wahitimu wa degree ya ualimu walikua 300 tu wakati wa diploma walikua zaidi ya 800.

Nawasilisha!
 
jibu ni simple, tuanzie hapo Tamisemi,
ajira nyingi za tamisemi lazima ziwe ni cheti au diploma kwasababu hao ndio wanahitajika wengi huko

mfano kada ya afya huwezi ukachukua daktari ukampeleka afanye kazi zahanati daktari anafiti hospitali sasa wilaya unakuta ina hospitali kubwa moja tu lakini zahanati inazo hata 20 kule zahanati hakuna magonjwa complicated sana na ikitokea ni ugonjwa mkubwa mgonjwa anapewa rufaa kwenda hospitali kubwa, ndio maana huko zahanati wanawekwa wa cheti na diploma,

kwa upande wa elimu pia vile vile shule za msingi ni nyingi sana kuliko za sekondary hivyo ndio maana walimu wa Grade IIIA wanakua wengi kwani we ulishaona mwalimu wa cheti anapangiwa sekondari?

Au unataka daktari bingwa apangiwe kufanya kazi zahanati?
 
Sisi tamisemi tuna ajili kulingana na mahitaji na sio unavyo taka wewe
 
Sawa
jibu ni simple, tuanzie hapo Tamisemi,
ajira nyingi za tamisemi lazima ziwe ni cheti au diploma kwasababu hao ndio wanahitajika wengi huko...
Nimekuelewa kuhusu madakatari/upande wa afya wala sijazungumzia grade A ..nimeongelea kwenye ualimu upande wa secondary kwa masomo yalio sawa, mfano physics wanachukuliwa Sana dip kuliko degree.
 
Nilikua napitia ajira za TAMISEMI za mwaka jana kwanini ajira zinakua na upendeleo sana? Unakuta pdf nzima imejaa wahitimu wa diploma au ni kwamba serikali inakwepa kuajiri wahitimu wenye degree ili kutoa mshahara mdogo...
Hatuajiri Cheti.tunaajiri Ujuzi katika kazi
 
jibu ni simple, tuanzie hapo Tamisemi,
ajira nyingi za tamisemi lazima ziwe ni cheti au diploma kwasababu hao ndio wanahitajika wengi huko

mfano kada ya afya huwezi ukachukua daktari ukampeleka afanye kazi zahanati daktari anafiti hospitali sasa wilaya unakuta ina hospitali kubwa moja tu lakini zahanati inazo hata 20 kule zahanati hakuna magonjwa complicated sana ndio maana wanawekwa wa cheti na diploma,

elimu pia vile vile shule za maingi ni nyingi sana hivyo ndio maana walimu wa Grade IIIA wanakua wengi kwani we ulishaona mwalimu wa cheti anapangiwa sekondari?


au unataka daktari bingwa apangiwe kufanya kazi zahanati?
Hapa umemaliza.
 
Back
Top Bottom