Kwanini Serikali inaogopa wachunguzi wa Kimataifa?

Mkuu kwanini cdm isilete mchunguzi wke kutoka huko uk afanye uchunguzi kimyakimya na kutoa jibu ili tujue ukweli kma kijana mwenzetu nani kamfanyia ubaya

Hauwezi kuleta wachunguzi bila serikali kuwakubali na kamwe hii serikali haiwezi kukubali wachunguzi kutoka nje ya nchi.
 
Mkuu kwanini cdm isilete mchunguzi wke kutoka huko uk afanye uchunguzi kimyakimya na kutoa jibu ili tujue ukweli kma kijana mwenzetu nani kamfanyia ubaya

Unafikiri watapata ushirikiano mzuri kama Serikali imekataa??Unadhani kwanini serikali imekataa unafikiri AG na WM hawajui nani yuko nyuma ya kupotea kwa Ben??
 
kama ben kafichwa na chadema wenyewe bc waruhusu intelejisia za kimataifa waje wachunguze tujue chadema ndio wamefanya na km wamefanya wao wewe hauoni n mtaji tosha kwa CCM kwenye chaguzi zijazo...

Mtekaji akubali kuchunguzwa,labda awamu iwe nyingine
 
Ujinga gani umeandika ,utumbo tu uchunguzi wa nje kwani umeambiwa vyombo vya usalama nchini vimeshindwa au unaandika tu na we we uonekana umeandika acha uvivu wa kufikiri na kutukuza wageni huo in utumwa na ukosefu wa afya ya akiri na umasikini wa elimu huku ukisumbuliwa na njaa ndio maana unaikibidhi akiri yako kwa wenyewe uwezo wa kfkr ukiamini watakutatulia shida zako hao wachunguzi hatuwataki vyombo vyetu ni imara na kazi zake vina compliance

Ni kweli kabisa vyombo imara uchunguzi Miezi sita na bado kuna utata hata kutoa habari.Ni kweli wakija wachunguzi toka nje siri za Serikali zitatoka na watekeaji kujulikana na serikali siyo rahisi kukubali siri za mauaji yanayofanywa na kitengo maalum kujulikana kikishirikiana kwa karibu na baadhi ya UVCCM chini ya Green guard.

AG na WM wanaujua ukweli macho,masikia na lugha ya miili yao inajionyesha.Ila kikubwa hakuna siri ya watu wawili
 
Wewe unatakiwa kukamatwa na kusema Ben alipo kwani kwa maneno yako inaonekana unajua alipo au alipelekwa wapi au nini kilimpata.
Basi waanze na Mbowe atwambie siku hiyo alimtuma wapi au alimuaga anakwenda wapi? Aliposhindwa kurudi alifanya nini? Na kwanini alishindwa kutoa taarifa polisi saa ishirini na nne toka alipopotea? Mpaka baada ya mwezi ndipo wanakuja kujitoa kimasomaso.
 
Jumamosi April 15 mwaka huu umoja wa kizazi cha kuhoji nchini (UTG) ulifanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea juu ya matukio mbalimbali ya watu kupotea, kutekwa na wengine kuuawa. Katika mkutano huo tulieleza baadhi ya hatua tulizochukua kuhusu hali hii ya kuogofya inayoendelea nchini kwa sasa.

Moja ya hatua hizo ni uongozi wa UTG kukaa mezani na uongozi wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini (LHRC) kuomba kituo hicho kupeleka malalamiko rasmi Umoja wa mataifa (UN) juu ya matukio ya watanzania kupotea, kutekwa na kuuawa.

Tuliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa kituo hicho Dr.Hellen Kijo Bisimba ambaye alishiriki mkutano wa umoja wa mataifa wa taasisi za kiraia zinazoshughulika na masuala haki za binadamu ambapo aliweza kupenyeza hoja kuhusu watanzania kupotea katika mazingira ya kutatanisha akihusisha suala la Ben Saanane ambaye ni Katibu Mkuu wa UTG Tanzania.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo Umoja wa mataifa ulimtaka Dr.Kijo kuwasilisha kwa maandishi malalamimo hayo ili waweze kutuma wataalamu wake kuja kuchunguza. Ieleweke kwamba Umoja wa mataifa una chombo huru cha uchunguzi kiitwacho "The Observer" na kina uwezo wa kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi yoyote mwanachama (Tanzania ikiwemo).

Hivyo basi UTG tulishirikiana na LHRC kuhakikisha kuwa barua hiyo inaandikwa na kufika katika utaratibu rasmi ili waweze kutuma wataalamu hao kuja kuchunguza. Tayari barua hiyo imeshaandikwa na tunasubiri majibu.

Dhumuni la kufanya hivyo ni kwa sababu hatujaridhishwa na utendaji wa vyombo vyetu vya ndani. Tunaamini vyombo vya kimataifa vinaweza kuwa huru zaidi kuchunguza mambo haya ya watanzania kupotea, kutekwa na kuuawa bila hatia.

Leo kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mhe.Freeman Mbowe ameonesha dhamira ileile iliyooneshwa juzi na UTG ya kukosa imani na vyombo vyetu vya ndani. Mhe.Mbowe ameomba serikali iruhusu makachero wa Uingereza maarufu kama "Scottland Yard" waje nchini kufanya upelelezi kuhusiana na matukio ya watanzania kupotea, na Mbowe amekua specific kwa Ben Saanane.

Lakini katika hali ya kushangaza Waziri Mkuu amejibu swali la Mbowe kwa majibu mepesi mno. Amesema vyombo vyetu vya usalama vinaendelea na uchunguzi. Katika kuonesha hakubaliani na kuja kwa vyombo vya kimataifa Waziri Mkuu amesema kwa sasa tuviachie vyombo vyetu vya ndani na serikali ikiona kuna haja ya kuita vyombo vya nje basi itafanya hivyo.

Maana yake ni Kwamba Waziri mkuu hadi sasa haoni haja ya kuita vyombo vya nje. Bado anaamini vyombo vyetu vya ndani vinaweza kuchunguza. Mi nadhani Mheshimiwa Waziri Mkuu anapaswa kutafakari upya. Huu sasa ni mwezi wa 6 tangu Ben apotee serikali inasema bado inaendelea na uchunguzi. Kweli?

Hivi waziri mkuu anajua kwamba katika miezi yote 6 hivyo vyombo anavyovitaja vimeshindwa kukamata hata mshukiwa wa suala la Ben, Vimeshindwa kutrace hata simu moja kati ya simu zilizompigia Ben mwishoni, Vimeshindwa kumhoji hata mwandishi aliyesema Ben anaonekana mtaani, vimeshindwa kufuatilia hata mtu aliyefuta baadhi ya post za Ben kwenye ukurasa wake wa facebook (zilizokua zikihoji PhD ya JPM). Hivi ndio vyombo ambavyo Waziri mkuu anasema tuendelee kuviamini.

Hivi Wairi Mkuu najua kwamba yombo hivyo anavyosema tuviamini vimetuhumiwa hadi bungeni kuhusika na njama za utekaji na utesaji? Waziri Mkuu anajua kamba Wabunge wake wa CCM akiwemo Mhe.Bashe wamevituhumu vyombo hivyo waziwazi kuwa vinahusika na kuteka raia wasio na hatia na kuwatesa hata kuwapoteza?

Sasa ikiwa tuhuma za kina Bashe ni za kweli, Waziri mkuu anapata wapi moral authority ya kutuambia tuendelee kuviamini vyombo hivyo? Kama vyombo hivyo vinatuhumiwa kuteka raia, vinawezaje kujichunguza vyenyewe na vikaleta ripoti ambayo tutaiamini?

Kanuni za msingi za sheria zinazuia mtu/taasisi/chombo kuwa hakimu wa kesi yake yenyewe (Nemo judex in causa sua). Sasa kwanini Waziri mkuu anatushinikiza tuviamini vyombo hivyohivyo vinavyotuhumiwa? Yani chombo kinatuhumiwa kuteka watu, halafu chombo hichohicho kinapewa kazi ya kuchunguza watekaji. What do u expect??

Hata kama tuhuma hizo si za kweli lakini kitendo cha kutuhumiwa tu kinavindolea vyombo hivyo sifa ya kuendelea na uchunguzi.

Kwanini Waziri Mkuu asiruhusu vyombo vya kimataifa vije kuchumguza ambavyo tunaamini vitakua fair and objective zaidi kuliko hivi vya ndani vyenye tuhuma lukuki?

Maazimio ya UTG ni uchunguzi wa madai ya watu kutekwa/kupotea/kuuawa yafanywe na vyombo vya kimataifa. Na tayari UTG kwa kushirikisna na LHRC wameshaandika barua Umoja wa mataifa kuomba wachunguzi hao. Leo mheshimiwa Mbowe naye kaomba makachero wa Uingereza waje kuchunguza. Lakini majibu ya Waziri mkuu yanaonesha serikali haipo tayari kwa wachunguzi hao. Swali la msingi ni kwanini serikali inaogopa wachunguzi wa kimataifa?
1+1-_2 wanahusika.
 
Jibu ni rahisi sana , Wachunguzi wa kimataifa hawapokei maagizo yoyote kutoka juu , wakifika watatufunua waziwazi .
 
Wachunguzi wa kimataifa kwa ajili ya Ben Sanane? Una roho ngumu sana. Police na vyombo vyetu vingine wanaiweza hii kazi haihitaji hayo. Tutawakamata tuuu.
Mpumbavu wew usiyejielewa..gharama za scotland yard zitalipwa na wew?? Unajua ni kiasi gani familia yake inaumia kumkosa kijana wao na serikali haitoi majibu..wakati mwingine funga kombo gani usioneshe watu how stupid you are
 
UTG ni Union of Tutokeje Group. Mkasome hata Ultimatum za Austria-Hungary na mjiulize why ile ya external investigators ilikaliwa.
Mnaleta brah brah hata OUR NATION form One ulifeli kudefine Sovereignty?
Au unataka iwe chance ku-claim kuwa hamna trust na dola ya nchi even in other issues?
Mmefeli.
 
Mpumbavu wew usiyejielewa..gharama za scotland yard zitalipwa na wew?? Unajua ni kiasi gani familia yake inaumia kumkosa kijana wao na serikali haitoi majibu..wakati mwingine funga kombo gani usioneshe watu how stupid you are
Unahisi ni Ben tu aliyepotea? Au aliyejiteka? Tunza ujinga wako wewe.
Tunaanzaje kuruhusu huo ujinga? Nchi ina maslahi mapana kuliko kelele zenu na michezo ya kitoto.
[HASHTAG]#TunzaUjingaWako[/HASHTAG]
 
Unahisi ni Ben tu aliyepotea? Au aliyejiteka? Tunza ujinga wako wewe.
Tunaanzaje kuruhusu huo ujinga? Nchi ina maslahi mapana kuliko kelele zenu na michezo ya kitoto.
[HASHTAG]#TunzaUjingaWako[/HASHTAG]
Kwani wakifanya utafiti wew ina kuuma nin?? Tatizo humo kichwani umejaza kinyesi cha mavi ya kuku...huo ujinga wako peleka huko instagram kwa watot wenzako wa sekondari maana naona likizo yenu ya pasaka haijaisha...choko wew usiyejielewa..
 
Embu tuwekeee majina na pembeni sababu za.hao uliosema eanatekwa sijui nini a kwa sababu zipi?

Yaani hata list hamuweki isomeke kutetemesha nchi, mnataka tu kutisha watu. Hamna sera zingine za kupambana na serikali? Raisi kuwabana kwenye mengi wanakalia kusukuma mambo ambayo wakikaa chini na kuangalia yaliyotokea nchi zingine matatizo wanayosukuma kuwa yapo nchini kwa uongo, basi wangekuwa wameshachimba maandaki kujificha hayo yasiwatokee.

Wote muache kutaka kuchafua serikali ya Mh. JPM, kama wanataka kufanya vikao wapate posho waje na mengine na sio haya yasio na kichwa wala miguu wala proof. Watu wameripoti waache uchunguzi uendeleee kwa aliyepotea na wanaopotea na kurudi. Hakuna lililotendwa na serikali hawana proof kabisaa bali kusingizia, waheshimu uchunguzi ufanyike ipasavyo. Eti kwa sababu watu wanaoisoma namba wanayaongelea na kusingizia basi na wao wanadakia.huku mapaparazi wakipokea bahasha kuchochea issue ambazo hazitusaidii wananchi wengi sie wa huku vijijini.

Serikali haina muda kujadili udaku.

Hapa kazi tu
Siku akipotea wa damu yako ndio utajua kuwa huu mchango wako wa leo hauna maana
 
Unahisi ni Ben tu aliyepotea? Au aliyejiteka? Tunza ujinga wako wewe.
Tunaanzaje kuruhusu huo ujinga? Nchi ina maslahi mapana kuliko kelele zenu na michezo ya kitoto.
[HASHTAG]#TunzaUjingaWako[/HASHTAG]
Mungu akuwezeshe umpendae apotee utajua waliopotelewa na jamaa zao wanajisikiaje.
 
Kuna watu wajinga sana nchi hii unapoongelea uhai wa mtu halafu wanakuja humu kupost utumbo wao nachukia sana tumwangalie Ben Kama kaka yako tumwangalie Ben kama mdogo wako tumwangalie Ben kama mjomba wako tumwangalie Ben kama mtoto wako vaa hivyo viatu halafu njoo na ujinga wako unaopost msiba usikie kwa jirani mzee Focus saanane alisema Ben ni mtoto wake sio mbuzi ana haki kujua yuko wapi au kama amekufa basi wafanye matanga wamalize lakini ni mwezi wa Sita sasa mtoto wake haonekani na wala serikali haijali tunachotaka kujua hapa watanzania kama amekufa tujue tuweke msiba tumalize matanga maisha yaendelee ndio msingi mkuu uliotoa swali kwa waziri mkuu miezi Sita hakuna trace yoyote iliyofanyika hata Mimi nashawishika kuomba Scotland yard Waje kutusaidia kuondoa sintofahamu hii
 
Wachunguzi wa kimataifa kwa ajili ya Ben Sanane? Una roho ngumu sana. Police na vyombo vyetu vingine wanaiweza hii kazi haihitaji hayo. Tutawakamata tuuu.
Miezi 6 hata kutrace mawasiliano mmeshindwa.komsingi hamjaonesha nia ya kusghulika na hili suala kwa dhati.hivyo kuna kila sababu ya kuita wachunguzi wa kimataifa.Ni akili za kiBASHITE(0%) TU ndio zinaweza kuwa na mlengo WAKO.
 
Kwani wakifanya utafiti wew ina kuuma nin?? Tatizo humo kichwani umejaza kinyesi cha mavi ya kuku...huo ujinga wako peleka huko instagram kwa watot wenzako wa sekondari maana naona likizo yenu ya pasaka haijaisha...choko wew usiyejielewa..
1-Usalama wako unakuwa endanger hasa ukizingatia ni mambo yanayohusu ulinzi wako na itakuwa rahisi kujua mnavyifanya kazi
2-Kugaramia jambo ambalo lipo ndani ya uwezo ni ujinga pia
3-Hawaaminiki vile vile, they can be used either na serikali zao au institutions za kutimiza agenda zao,ee can't rely on them!
4-Taasisi zenu za upelelezi zinauwezo mkuwa na ndomana unatoa macho kwenye simu ukiwa salama kabisa, kufanya hivyo ni kuwashusha na kuwafisha moyo.
KAMA HUJAELEWA SABABU, ULIZA TENA
 
Kwani wakifanya utafiti wew ina kuuma nin?? Tatizo humo kichwani umejaza kinyesi cha mavi ya kuku...huo ujinga wako peleka huko instagram kwa watot wenzako wa sekondari maana naona likizo yenu ya pasaka haijaisha...choko wew usiyejielewa..

hii inahitaji elimu kidogo tu ya ufahamu
1-Tuna institution zinazojitosheleza na kamwe hazijasema zimeshindwa.
2-mtoa wazo hajaishia hapo kaenda mbele kwa kupendekeza *uingereza* sisi tunahoji kwanini uingereza??
3-Anapokuja kutajwa kwenye hili huoni tayar anaandaa mazingira ya kusema hana imani na uchunguzi wa vyombo vyetu??anatuandaa psychological mapema!
 
Back
Top Bottom