Kwanini Serikali inadharau sana Buza?

Kwanini Serikali inadharau sana Buza?

Hili eneo linaonekana kuwa nyuma kimaendeleo ndio maana nauliza hili swali.

Ilipotengenezwa barabara ya lami toka Jetcorner mpaka Davis corner kidogo yalikuja mabadiliko.

Lakini naona kimaendeleo bado sana. Japokuwa kuna hospital mpya imejengwa lakini siridhiki na namna serikali inavyoiangalia Buza.

Umeme unakatika mara kwa mara na kuwa kero. Maji mtandao wa dawasa haujafika.

Mradi wa maji jetbuza ni kitendawili. Na Kitila Mkumbo alisema wameshalipa bil 100+ kwa miradi ya maji ikiwemo w Buza.

Mbunge wa Temeke anakaa Buza lakini hajawahi kufanya hata mkutano na wananchi.

Hivi ndio kusema Dar es Salam ni Kinondoni tu? Japokuwa hata kinondoni kuna maeneo sio mazuri kama Buza mfano Tandale.

Basi kamilisheni mradi wa Jet Buza wa maji ili na sisi tusifikiri mnatudharau. Mbunge wa Temeke upo hata hii ishu huulizii au umehamia masaki?
Siku ukitembelea matembele ya 1, kitunda, kibeberu, mwanagati, matembele ya 2, sirali, kivule, fremu kumi, msongola, mbondole, njia nne utagundua kuwa buza ni kama TORONTO!!
 
Dar yote kama unakokaa kuna wauza miguu, vichwa na utumbo wa kuku ujue unakaa na watu wa ajabu.

Wakaanga samaki na dagaa mitaani, wala kongoro na supu za utumbo ndugu yangu weka malengo ya kuhama in case wewe si wa ajabu.

Ila kama unaona poa tu, basi we ni wa ajabu pia ukihamia sehemu nyingine utaona mizinguo, komaa kibuzabuza
Ongezea na mishikaki ya sh mia!
 
Dar yote kama unakokaa kuna wauza miguu, vichwa na utumbo wa kuku ujue unakaa na watu wa ajabu.

Wakaanga samaki na dagaa mitaani, wala kongoro na supu za utumbo ndugu yangu weka malengo ya kuhama in case wewe si wa ajabu.

Ila kama unaona poa tu, basi we ni wa ajabu pia ukihamia sehemu nyingine utaona mizinguo, komaa kibuzabuza
Kuna watu wanaishi Dar lakini kama wapo kijijini
 
Nyinyi mnaoishi huko chobingo mna mchango kiasi gani katika kuleta mabadiliko ya eneo lenu ?
 
That's the plain truth mkuu. Buza, mbagala, gongo la mboto na maeneo mengine yenye sifa kama za Buza, mbagala, gongo la mboto hazipo Dar es salaam. Hata watu wa huko wapo tofauti na watu wanaoishi Dar es salaam.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Buzz iko poa sana Ila washamba na malimbukeni hawaijui
 
Buzz iko poa sana Ila washamba na malimbukeni hawaijui
Buza inayoongelewa humu ni ya kwenye magazeti ila original buza naijua iko vzr huwezi fananisha na tandika, Tandale au Vingunguti ni tofauti sana.
 
Temeke si ndo kuna uswazi nyingi kuliko wilaya zote? Sababu Mbagala,Tandika,Buza na makolokolo mengine ni huko....Dar es salaam ni Ilala na Kinondoni kwa mbali
Dar es salaam yote ni CHAFU, kunanuka, kuna mitaro yenye vinyesi vinavyonuka, kuna idadi kubwa sana ya watu, Hewa chafu, majengo ya kiswahili yaliyojengwa bila mpangilio.

Pako hovyohovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom