Kwanini Serikali imesamehe Shilingi Trilioni 424?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,818
Reaction score
62,032
Ndugu zangu
Kwa mujibu wa uchunguzi na utafiti ulioendeshwa na wataalamu wetu profesa Mruma na Profesa Osoro ilibainika wazi kabisa kuwa Watanzania tulikuwa tukiibiwa na kampuni ya ACACIA katika madini yetu hususan kupitia mchanga wa makinikia.

Kwa mujibu wa Utafiti huo ilibainishwa kuwa pamoja na dhahabu walizokuwa wakikomba, walikuwa wakikombana madini mengineyo kama vile copper, chuma, cobalt na mengineyo yenye thamani.

Uchunguzi ulionyesha kuwa kwa muda mzima walio-operate nchini, ACACIA wametuibia takriban dola bilion 190 ambazo ni takriban sawa na shilingi Trilion 424.

Hizi ni pesa nyingi, nyingi, nyingi mno. Cha kushangaza ni kwamba serikali hii iliyounda tume na kubaini haya IMESAMEHE HIZI PESA!

Mtu unajiuliza kama siyo Uhujumu Uchumi hii ni kitu gani?

Tulichoambulia eti ni kupewa asilimia 16 ya hisa kwenye madini yetu wenyewe huku Mabeberu yakiendelea kukomba asilimia 84 na kutuachia vijisenti vya Dola milion 300 ambayo haifiki hata TRLION moja, Yaani Tumesamehe Trilion 424 ili Tupewe vihela ambavyo havifiki hata TRILION 1, Tumerogwa?

Katika vitu ambavyo serikali inayokuja inapaswa kufanya baada ya awamu hii kutoka madarakani ni kuwachukulia hatua wale wote waliosamehe hizi Trilion 424.

Mimi najiuliza, Bajeti yetu ya kila mwaka haifiki Trilion 40, Halafu leo hii unasamehe Trilion 424 ambayo ni bajeti ya nchi ya miaka 10 na tena hapo bila kutembeza bakuli kwa wahisani!

Serikali itupe majibu, Isijifanye kuweka Ukimya ili kutusahaulisha

KWA NINI IMUACHIE MWIZI ASEPE NA TRILION ZETU 424?
 
Unauliza swali wakati jibu umeshajibu kwenye mada yako!

Yaani unaiuliza serikali wakati hapo hapo unasema jibu litapatikana ikija serikali nyingine! Sasa unataka jibu gani zaidi ya ulilojijibu?

Subiri hiyo serikali yako mpya ikija utapata jibu lako!

Kanuni za majadiliano ni pamoja na kupata mwafaka kwa pande zote mbili kwa faida ya muda mfupi au mrefu. Majadiliano hayana sheria bali yana mwongozo.

Msingi wa majadiliano ni chukua nikupe (take and give)! Sasa ulitaka serikali ichukue vyote kwenye majadiliano?

sheria/mwongozo wa chukua vyote uko mahakamani na sio kwenye majadiliano.
 
Unauliza swali wakati jibu umeshajibu kwenye mada yako!

Yaani unaiuliza serikali wakati hapo hapo unasema jibu litapatikana ikija serikali nyingine! Sasa unataka jibu gani zaidi ya ulilojijibu?

Subiri hiyo serikali yako mpya ikija utapata jibu lako!

Nimeiuliza serikali hii itupe majibu kwa nini imesamehe Trilion zetu 424 ambazo ripoti ya uchunguzi ya profesa Mruma na Osoro ilibaini ACACIA kutuibia ktk madini yetu.
 
Unaiuliza serikali hii wakati una serikali yako inakuja madarakani?

Hizo nguvu za kuuliza serikali ambayo unadhani imefanya makosa ungezitumia kuhakikisha serikali yako inayokuja madarakani inakuja kweli kuwachukulia hatua wale wote waliosamehe hizi Trilion 424 labda kama huiamini pia hiyo serikali yako!
 
Tena Serikali ijayo iende mbali zaidi kudai fidia kwa wakoloni kuitawala nchi yetu bila ridhaa yetu!
 
na tutambue kuwa hii kesi in a long term tutaathirika mno,maana wawekezaji wa madini wame I RED FLAG nchi yetu na tumo namba 2 kutoka chini kwa nchi ambazo ni HIGH RISK KUWEKEZA KWENYE NYANJA HII YA MADINI.
 
Unaiuliza serikali hii wakati una serikali yako inakuja madarakani?

Hizo nguvu za kuuliza serikali ambayo unadhani imefanya makosa ungezitumia kuhakikisha serikali yako inayokuja madarakani inakuja kweli kuwachukulia hatua wale wote waliosamehe hizi Trilion 424 labda kama huiamini pia hiyo serikali yako!

Serikali ni taasisi endelevu

Ikitoka ya awamu ya tano itakuja ya awamu ya sita.

Kwa vyovyote serikali lazima itoe majibu kwa nini imesamehe trilion 424

Tunaanza kuihoji hii kwa sababu ndiyo iliyoko madarakani kwa sasa na ndiyo iliyochukua uamuzi huu wa ajabuajabu
 
Kwani ya sasa hivi imeishatoa majibu ya awamu ya NNE!
 
Ndugu zangu
Kwa mujibu wa uchunguzi na utafiti ulioendeshwa na wataalamu wetu profesa Mruma na Profesa Osoro ilibainika wazi kabisa kuwa Watanzania tulikuwa tukiibiwa na kampuni ya ACACIA katika madini yetu hususan kupitia mchanga wa makinikia.

Kwa mujibu wa Utafiti huo ilibainishwa kuwa pamoja na dhahabu walizokuwa wakikomba, walikuwa wakikombana madini mengineyo kama vile copper, chuma, cobalt na mengineyo yenye thamani.

Uchunguzi ulionyesha kuwa kwa muda mzima walio-operate nchini, ACACIA wametuibia takriban dola bilion 190 ambazo ni takriban sawa na shilingi Trilion 424.

Hizi ni pesa nyingi, nyingi, nyingi mno. Cha kushangaza ni kwamba serikali hii iliyounda tume na kubaini haya IMESAMEHE HIZI PESA!

Mtu unajiuliza kama siyo Uhujumu Uchumi hii ni kitu gani?

Tulichoambulia eti ni kupewa asilimia 16 ya hisa kwenye madini yetu wenyewe huku Mabeberu yakiendelea kukomba asilimia 84 na kutuachia vijisenti vya Dola milion 300 ambayo haifiki hata TRLION moja, Yaani Tumesamehe Trilion 424 ili Tupewe vihela ambavyo havifiki hata TRILION 1, Tumerogwa?

Katika vitu ambavyo serikali inayokuja inapaswa kufanya baada ya awamu hii kutoka madarakani ni kuwachukulia hatua wale wote waliosamehe hizi Trilion 424.

Mimi najiuliza, Bajeti yetu ya kila mwaka haifiki Trilion 40, Halafu leo hii unasamehe Trilion 424 ambayo ni bajeti ya nchi ya miaka 10 na tena hapo bila kutembeza bakuli kwa wahisani!

Serikali itupe majibu, Isijifanye kuweka Ukimya ili kutusahaulisha

KWA NINI IMUACHIE MWIZI ASEPE NA TRILION ZETU 424?
Tupe ufafanuzi ni jinsi gani tungeweza kuzipata hizo Trilioni 424 na bado tukaendelea kuwekeza nao hao Barrick au Accacia...?
 
Back
Top Bottom