Kwanini Serikali imesamehe Shilingi Trilioni 424?

Tupe ufafanuzi ni n jinsi gani tungeweza kuzipata hizo Trilioni 424 na bado tukaendelea kuwekeza nao hao Barrick au Accacia...?

Hatuna shida ya kumkumbatia mwizi.

Hizo Trilion zetu 424 ni nyingi kuliko pesa zote tutakazozipata kwa muda wote huo ambao hao Barick wataendelea kuchimba madini hapa nchini
 
Hivi wewe mpaka leo hajaelewa tu ni usanii wa hali ya juu ule.

Accacia waliosema haijasajiliwa mpaka leo sijaona kama imesajiliwa toka hii kasumba ianze. Na inaendelea kuchimba maadini. Makinikia nayo yanasepa kama kawa.
 
Ndugu zangu
Kwa mujibu wa uchunguzi na utafiti ulioendeshwa na wataalamu wetu profesa Mruma na Profesa Osoro ilibainika wazi kabisa kuwa Watanzania tulikuwa tukiibiwa na kampuni ya ACACIA katika madini yetu hususan kupitia mchanga wa makinikia.

Kwa mujibu wa Utafiti huo ilibainishwa kuwa pamoja na dhahabu walizokuwa wakikomba, walikuwa wakikombana madini mengineyo kama vile copper, chuma, cobalt na mengineyo yenye thamani.

Uchunguzi ulionyesha kuwa kwa muda mzima walio-operate nchini, ACACIA wametuibia takriban dola bilion 190 ambazo ni takriban sawa na shilingi Trilion 424.

Hizi ni pesa nyingi, nyingi, nyingi mno. Cha kushangaza ni kwamba serikali hii iliyounda tume na kubaini haya IMESAMEHE HIZI PESA!

Mtu unajiuliza kama siyo Uhujumu Uchumi hii ni kitu gani?

Tulichoambulia eti ni kupewa asilimia 16 ya hisa kwenye madini yetu wenyewe huku Mabeberu yakiendelea kukomba asilimia 84 na kutuachia vijisenti vya Dola milion 300 ambayo haifiki hata TRLION moja, Yaani Tumesamehe Trilion 424 ili Tupewe vihela ambavyo havifiki hata TRILION 1, Tumerogwa?

Katika vitu ambavyo serikali inayokuja inapaswa kufanya baada ya awamu hii kutoka madarakani ni kuwachukulia hatua wale wote waliosamehe hizi Trilion 424.

Mimi najiuliza, Bajeti yetu ya kila mwaka haifiki Trilion 40, Halafu leo hii unasamehe Trilion 424 ambayo ni bajeti ya nchi ya miaka 10 na tena hapo bila kutembeza bakuli kwa wahisani!

Serikali itupe majibu, Isijifanye kuweka Ukimya ili kutusahaulisha

KWA NINI IMUACHIE MWIZI ASEPE NA TRILION ZETU 424?
Turkish ambiwa kuwa ccm ni ukoo wa panya, kilatu ni mwizi, kisha utasikia wajinga wanasema chizi ananyosha nchi
 
Tanzania sio wa kwanza ku-negotiate na mabeberu.

Na kwenye negotiations kuna win-lose; give and take.

Hatujapata Tril zaidi ya 400 kama fine na penalty.

Tumepata 16% ya hisa kwenye kampuni mpya.

Tumepata kishika uchumba USD 300mil

Ofisi mpya inajengwa Mwanza kama makao makuu.

Watz kuwa sehemu ya management.

Fedha za mauzo kuwekwa kwenye bank za ndani.
Manufaa ya kiuchumi ya 50/50.

ZZK anaepinga na kukandia alikuwa kwenye kamati ya Bomani; wao walitupa nini baada ya kuzunguka nchi nzima?

JPM kajitahidi sana sana kuliko mrahaba wa 3% na baadae 4% ya taarifa ya Fedha wanayoandaa wawekezaji.

Kwa sasa Watanzania tunakuwa sehemu ya bodi hali kadhalika kwenye management.
Changamoto ni kupata watu waaminifu ambao wakiwa kwenye bodi na management; walinde maslahi ya Watanzania.
 
Ukiingia Mkataba wowote ule na Mzungu hakikisha na Wewe Mswahili ( Mtanzania ) uwe na IQ iliyotoshelezeka la sivyo utaumia tu.
 
Kwanini usimsaidie kujibu maana hata majibu amekuwa hayaamini Ila anachoamini nikwamba watawala waliitangazia Dunia kuwa wanawadai mabeberu wa madini matrilion ya pesa ndio swali jamaa lilipo badala yakupata mipesa zimegeuga kuwa porojo
Unauliza swali wakati jibu umeshajibu kwenye mada yako!

Yaani unaiuliza serikali wakati hapo hapo unasema jibu litapatikana ikija serikali nyingine! Sasa unataka jibu gani zaidi ya ulilojijibu?

Subiri hiyo serikali yako mpya ikija utapata jibu lako!
 
Mkuu hapa unahamisha magoli
Unaiuliza serikali hii wakati una serikali yako inakuja madarakani?

Hizo nguvu za kuuliza serikali ambayo unadhani imefanya makosa ungezitumia kuhakikisha serikali yako inayokuja madarakani inakuja kweli kuwachukulia hatua wale wote waliosamehe hizi Trilion 424 labda kama huiamini pia hiyo serikali yako!
 
Tanzania sio wa kwanza ku-negotiate na mabeberu.

Na kwenye negotiations kuna win-lose; give and take.

Hatujapata Tril zaidi ya 400 kama fine na penalty.

Tumepata 16% ya hisa kwenye kampuni mpya.

Tumepata kishika uchumba USD 300mil

Ofisi mpya inajengwa Mwanza kama makao makuu.

Watz kuwa sehemu ya management.

Fedha za mauzo kuwekwa kwenye bank za ndani.
Manufaa ya kiuchumi ya 50/50.

ZZK anaepinga na kukandia alikuwa kwenye kamati ya Bomani; wao walitupa nini baada ya kuzunguka nchi nzima?

JPM kajitahidi sana sana kuliko mrahaba wa 3% na baadae 4% ya taarifa ya Fedha wanayoandaa wawekezaji.

Kwa sasa Watanzania tunakuwa sehemu ya bodi hali kadhalika kwenye management.
Changamoto ni kupata watu waaminifu ambao wakiwa kwenye bodi na management; walinde maslahi ya Watanzania.

hisa 16% na wao 84%

Yaani unamaanisha tumenunua hivyo vi hisa kiduchu kwa Trilion zetu 424?. Pesa ambayo thamani yake ni bajeti ya nchi yetu kwa miaka zaidi ya 10 bila kuhitaji kusaidiwa na wahisani
 
Unaiuliza serikali hii wakati una serikali yako inakuja madarakani?

Hizo nguvu za kuuliza serikali ambayo unadhani imefanya makosa ungezitumia kuhakikisha serikali yako inayokuja madarakani inakuja kweli kuwachukulia hatua wale wote waliosamehe hizi Trilion 424 labda kama huiamini pia hiyo serikali yako!
Unashauri Serikali ijayo iwafungulie magufuri na kabudi kesi gani? ya uhujumu uchumi kama anavyopendekeza jamaa?
 
hisa 16% na wao 84%

Yaani unamaanisha tumenunua hivyo vi hisa kiduchu kwa Trilion zetu 424?. Pesa ambayo thamani yake ni bajeti ya nchi yetu kwa miaka zaidi ya 10 bila kuhitaji kusaidiwa na wahisani

shares za hiko kikampuni zitakuwa na hidden value kubwa katika historia ya dunia.
 
Siyo sifa za kisiasa, amepata kitu. kuliko kukaa tu hapo na kumkenulia mzungu meno eti mkataba. Rais amejitahidi sana kuyakomalia mabeberu majizi, tumpe credit anazostahili.
 
Unashauri Serikali ijayo iwafungulie magufuri na kabudi kesi gani? ya uhujumu uchumi kama anavyopendekeza jamaa?
Mkuu;
Hilo swali ungewauliza wenye ''serikali inayokuja'' kwa sababu wao ndio wanajua makosa yaliyofanyika!
 
kwa mujibu wa lisu zile ripoti za akina mruma ni professorial rubbish
He almost lost his life aise
Na mimi namuunga mkono, thamani ya kampuni ya barrick aliyekuwa na hisa nyingi haifiki hizo dola za marekani 190 bilioni. Kama ripoti zile zingekuwa za kweli basi acacia ingekuwa ndio most profitable company duniani. Ikumbukwe pia kampuni mama, barrick, inaoperate nchi kadhaa ulimwenguni na sio Tanzania tu. Sasa utaona ni jinsi gani hicho kiasi hakikuwa sahihi na hio ni gawio pamoja na kodi tu ikiwa na maana kuwa faida walioingiza kwa Tanzania pekee ni bilioni nyingi zaidi ya huo mgao wetu na hio ni kwa migodi ya Tanzania pekee. Hakuna faida ya namna hii duniani.
 
Tupe ufafanuzi ni jinsi gani tungeweza kuzipata hizo Trilioni 424 na bado tukaendelea kuwekeza nao hao Barrick au Accacia...?
Ni Tanzania kuiwekea Canada vikwazo vya kiuchumi na kijamii ili nchi hiyo ilazimishe Barrick ilipe deni hilo la mtoto wake ACACIA😃😃😃😃😃. Ikumbukwe lile beberu kubwa linalomiliki Barrick Gold linaishi Toronto na ndipo ilipo makao makuu ya kampuni hiyo pia
 
Back
Top Bottom