Kwanini Samsung asitengeneze OS yake?

Kwanini Samsung asitengeneze OS yake?

Samsung ni moja ya makampuni makubwa duniani kwenye uwanja wa teknolojia. Kutengeneza simu zinazotumia Android OS naona kama ni embarasment kwa kampuni kubwa hivi.

Sidhani kama watashindwa kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye R&D ya kutengeneza OS yao.

Faida kubwa watakayopata ni ku-customize software na hardware kama Apple na Windows Phone wakati ule. Na hata tatizo lililoikumba Note 7 lisingetokea mwaka jana.

Faida nyingine ni kuwa na loyal customers ambao itawawia vigumu kuwahama kwasababu ya uniqueness ya OS yao. Mfano kwa sasa iphone na nokia ya wakati ule wameshatengeneza loyal customers kiasi kwamba kuhama platform zao imekuwa shida sana.

Ila kutumia android kuna wapa wateja option ya kuipata android sehemu nyingine na hata ushindani na makampuni mengine yanayotengeneza simu za Android unakua mkubwa. Ila wakiwa na OS yao watawapa ugumu loyal customers kuhama brand.

Play store imejaa malware, kila mtu anaweka app yake hata kama imekaa hovyohovyo. Wakiwa na OS yao, hawatawapa mwanya developers wanaoweka uchafu kwenye store watakayoitengeneza.

Samsung anauza mamilion ya simu, sio mbaya kuanza tayari anauza simu nyingi kwa mwaka.
Tunahitaji varieties za OS sokoni, kuwa na Os chache kunakinaisha.

Wakati unaendelea kusema bullshit kuhusu android tambuwa ya kwamba its the most polular is kuliko hata windows.

Android Beats Windows to Become World's Most Popular Operating System
 
hio ni net marketshare aka idadi ya watu wanaotumia internet, na sio idadi ya user wa operating system,

mfano naweza fungua laptop yangu nikacheza game then nikafunga, system hio hainihesabu mimi kama mtumiaji wa windows sababu sijaingia kwenye website zao ili wanihesabu,

sasa imagine zile computer za bank, Atm, server mbalimbali, mashirika mbalimbali yanayotumia intranet etc
 
Ni battle tu hyo bro microsoft wanaongoza kwenye desktop wars Ila as time goes minituarization continues embedded systems Zita take over
 
Wakati unaendelea kusema bullshit kuhusu android tambuwa ya kwamba its the most polular is kuliko hata windows.

Android Beats Windows to Become World's Most Popular Operating System
Popularity goes to those cheap products associated with Android, the likes of Tecno, Xiaomi, Samsung etc. They don't have a choice, they're caught up in only one choice.
Kama wangekuwa na 'deep pockets' wasingenunua hiyo Android. Wangekimbilia kwenye iOS au Windows. Angalia hata humu jf, wangapi wanatamani kuwa na iphone ila hawana uwezo.
 
Mi mbona nina deep pockets (kwa minajili ya uwezo wa kununua na ku maintain simu) sitaki kuwa na simu za Apple na nishawahi kupewa Apple ya bure niijaribu nikaikataa baada ya kukaa nayo wiki mbili?

Kila mwaka nanunulia watu wa nyumbani angalau wawili simu, nawauliza wanataka simu gani niwanunulie, yoyote, money is no object, hawajawahi kuitaja Apple hata mwaka mmoja.

Hiyo theory yako ya deep pocket inabidi ui revise.

Sijaelewa kwa nini mtu anayeelewa simu na electronics anunue simu ambayo haina removable battery wala micro SD card slot.
 
Siwezi kupingana na hili binadamu majority wapo fickle minded wamesha au Apple marketing imewafanya waamini kuwa iPhone ni a status symbol watu wanaona wakiwa nayo wataoneka wealthy hii ni dhahiri dunia nzima.
So sipingani na kauli yako.

Lakini kwenye swala la deep pockets sema ukweli hata kwangu siwezi poteza hela kwenye an IPhone niache kununua a Galaxy S8 nitajiona chizi.

Android fans hawapendei Android for price
tu lakini wanapendea specs na features.. Kitu ambacho iPhone inacho leo na kinaitwa "innovation" Android kilikuwepo miaka 4 iliopita.
 
Hahaha apple kwa marketing wamewateka watu wengi sana.Wako watu kibao wana deep pockets na hawakubali iPhones bro.Mi mwenyewe mara mia nitumie bidhaa za Nexus au Google pixel ila Cyo apple
 
Kwa watu waliosoma mambo ya computer na electronics wanaoelewa habari za open systems na closed systems kuwa na simu ya Apple ambayo huwezi hata kufungua ubadilishe battery, halafu useme hiyo ndiyo simu yenye innovation ni kituko.

Watu wanatafuta simu unazoweza kubadili processor kama computer, Apple wanakataza kubadili battery tu.

This is an insult to the intelligence of consumers.
 
Mi mbona nina deep pockets (kwa minajili ya uwezo wa kununua na ku maintain simu) sitaki kuwa na simu za Apple na nishawahi kupewa Apple ya bure niijaribu nikaikataa baada ya kukaa nayo wiki mbili?

Kila mwaka nanunulia watu wa nyumbani angalau wawili simu, nawauliza wanataka simu gani niwanunulie, yoyote, money is no object, hawajawahi kuitaja Apple hata mwaka mmoja.

Hiyo theory yako ya deep pocket inabidi ui revise.

Sijaelewa kwa nini mtu anayeelewa simu na electronics anunue simu ambayo haina removable battery wala micro SD card slot.
Unajitumia wewe kama SI Unit ya kupima uwezo wa watanzania?
Ingekua wote wana deep pockets kama wewe kungekuwa na Tecno na zile simu cheap za kkoo?
Majority ya watanzania hawawezi kuafford basic stuffs ukiacha mbali hizo high end phones.
Na hata hao apple wanauza sana simu zao dunia ya kwanza na ya pili. Dunia ya tatu ni wachache wenye uwezo wa kumiliki hizo simu.
 
Kwa watu waliosoma mambobya computer na elwctronics wanaoelewa habari za open systems na closed systems kuwa na simu ya Apple ambayo huwezi hata kufungua ubadilishe battery, halafu useme hiyo ndiyobsimu yenye innovation ni kituko.

Watu wanatafuta simu unazoweza kubadili processor kama computer, Apple wanakataza kubadili battery tu.

This is an insult to the intelligence of consumers.

Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
Fungua funga ubadili battery.
Fungua funga ubadili memory card.
Fungua funga sijui ubadili processor.
Sasa hiyo simu itatamanika kweli? Huo mfuniko utafananaje?
Apple wanakupa enough storage kwa kuwa wanajua huwezi kuzimaliza. Istoshe, wanajua simu sio kwa ajili ya matumizi mazito. Ile ni kwa kufanya kazi nyepesi ukiwa hauna pc kwa wakati huo.
Kwahiyo mkuu ukitoka nyumbani unabeba battery zako 4, memory card zako 10 mfukoni? Ukifika sehemu unaanza kufungua simu yako unabadili battery, mara uweke memory card uangalie documentary zako.
Badae unafungua unatoa memory card ya documentary unaweka ya movie?
Kazi unayo mkuu..
 
simu 300m kwa mwaka mkuu,

kama alivyosema mdau hapo juu samsung os yao inaitwa tizen, sasa hivi tv na smartwatch zao wanatumia tizen na simu zote za samsung kwenye series ya z zinatumia tizen, mfano samsung z2, sema anatoa low end tu, hakuna simu kubwa kubwa za tizen.

ila cha kuogopesha kwenye hii tizen ni kwamba big players wote waliokuwa wanampa support samsung wamejitoa, mfano Intel, hivyo naona kama hawapo serious kwenye simu wanataka tu iwe os ya internet of things ikae kwenye mafridge, saa, tv, mashine za kufulia etc

na kuhusu battery sasa hivi samsung achana nayo, wapo dunia ya kwao even apple anasubiria, mfano angalia hizi series zao za 2017 simu kama A3, A5 na A7 ya 2017
hii ni A3 ina 2350mah tu lakini score yake ya battery ni hii
galaxy-a3-2017.jpg

na hii ni iphone 7 yenye 1960mah
gsmarena_001.jpg

hapo hata uki adjust huo ukubwa still A3 yupo juu na zote ukitoa soc mambo mengi zinafanana kama ukubwa wa display, resolution, ram etc
Mkuu. Hiyo battery life assessment ya A3 ni reliable? Ushawahi tumia ukaipata hiyo figure?
Soc ina affect nini kwenye matumizi ya simu?
 
Unajitumia wewe kama SI Unit ya kupima uwezo wa watanzania?
Ingekua wote wana deep pockets kama wewe kungekuwa na Tecno na zile simu cheap za kkoo?
Majority ya watanzania hawawezi kuafford basic stuffs ukiacha mbali hizo high end phones.
Na hata hao apple wanauza sana simu zao dunia ya kwanza na ya pili. Dunia ya tatu ni wachache wenye uwezo wa kumiliki hizo simu.
Sijajitumia mimi kama SI Unit ya uwezo wa watanzania. Hiyo haitakuwa faira kwa watu wenye per capita income ninayotumia mara mbili katika weekend moja.

Nimejitumia mimi kupinga habari ya kwamba watu wanachagua Android kwa sababu hawana uwezo wa kununua iPhone.

Mimi nina uwezo wa kununua iPhone na sijanunua hata baada ya kupewa bure niijaribu kwa mwezi mzima.
 
Fungua funga ubadili battery.
Fungua funga ubadili memory card.
Fungua funga sijui ubadili processor.
Sasa hiyo simu itatamanika kweli? Huo mfuniko utafananaje?
Apple wanakupa enough storage kwa kuwa wanajua huwezi kuzimaliza. Istoshe, wanajua simu sio kwa ajili ya matumizi mazito. Ile ni kwa kufanya kazi nyepesi ukiwa hauna pc kwa wakati huo.
Kwahiyo mkuu ukitoka nyumbani unabeba battery zako 4, memory card zako 10 mfukoni? Ukifika sehemu unaanza kufungua simu yako unabadili battery, mara uweke memory card uangalie documentary zako.
Badae unafungua unatoa memory card ya documentary unaweka ya movie?
Kazi unayo mkuu..

Wewe si mtumiaji wa simu vilivyo ndiyo maana unaridhika na hiyo simu ya Apple.

Watumiaji wa simu tunajua maana ya micro SD card na removable battery.

Wewe unatumia simu kama fashin, mapambo na "status symbol". Ndiyo maana kundi lenu mnaweza kuona mtu mwenye hela hatakiwi kuwa na simu isiyo Apple.
 
Siwezi kupingana na hili binadamu majority wapo fickle minded wamesha au Apple marketing imewafanya waamini kuwa iPhone ni a status symbol watu wanaona wakiwa nayo wataoneka wealthy hii ni dhahiri dunia nzima.
So sipingani na kauli yako.

Lakini kwenye swala la deep pockets sema ukweli hata kwangu siwezi poteza hela kwenye an IPhone niache kununua a Galaxy S8 nitajiona chizi.

Android fans hawapendei Android for price
tu lakini wanapendea specs na features.. Kitu ambacho iPhone inacho leo na kinaitwa "innovation" Android kilikuwepo miaka 4 iliopita.
Wakati Galaxy S5 zinatoka mdogo wangu alikuwa miongozi mwa watu wa mwanzo kuinunua hiyo simu. Baada ya miezi minne simu ikawa inazimazima. Akairudisha pale Samsung akabadilishiwa mother body nayo baada ya miezi 6 kadhaa ikawa slow ajabu.
Simu za Android zinabeba specs za juu ajabu mfano RAM hadi 4GB, battery hadi 4000mAH. Ila apple anabeba specs za kawaida sana ila ukiiweka kwenye geekbench unakuta iphone anamtupa mbali galaxy kwenye single na multi score test.
Android zinabeba specs nyingi na kubwa ila bado end user haifurahii simu yake baada ya muda.
 
Sijajitumia mimi kama SI Unit ya uwezo wa watanzania. Hiyo haitakuwa faira kwa watu wenye per capita income ninayotumia mara mbili katika weekend moja.

Nimejitumia mimi kupinga habari ya kwamba watu wanachagua Android kwa sababu hawana uwezo wa kununua iPhone.

Mimi nina uwezo wa kununua iPhone na sijanunua hata baada ya kupewa bure niijaribu kwa mwezi mzima.
Kwahiyo mkuu unaniambia ukifanya random sampling ya watumiaji 10 wa android ambao wakipewa iphone wataikataa kutokana na sababu ulizotoa hapo juu?
 
Mkuu. Hiyo battery life assessment ya A3 ni reliable? Ushawahi tumia ukaipata hiyo figure?
Soc ina affect nini kwenye matumizi ya simu?

mkuu soc ni kila kitu ndani kuna processor, gpu, modem, wifi, bluetooth, camera intelligence, ram, storage type etc hivyo vitu vyote humo ndani kama vinakula sana umeme ujue simu nayo haitakaa na chaji,

kikubwa zaidi cha kufanya hivyo vitu visile chaji ni manufacturing process iliotumika, zipo process nyingi hizi ni baadhi kutoka mpya kwenda zamani

-10nm hii ndio latest mfano soc ndani ya galaxy s6 imetumia hii
-14nm process latest ya mwaka jana na midrange soc za mwaka huu zinatumia hii mfano hio snaodragon 625
-16nm haina tofauti sana na 14nm
-22nm
-28nm
-32nm etc

jinsi inavyokuwa ndogo ndio jinsi inavyokula umeme kidogo na kuwa na nguvu zaidi.

pia kwenye cpu kuna ambazo hazina nguvu lakini zinakula umeme mdogo na kuna zenye nguvu na zinakula umeme mwingi mfano cortex a7 na cortex a53 hazina nguvu sana ila hazili umeme na cortex a72, a73, kyro na cortex a57 zina nguvu na zinakula charge.

kwenye hio a3 nimekupa tu mfano compare na iphone ila a5 na a7 zitakaa zaidi na charge,

pia hio test ina masharti uyajue
-mwanga wameweka 50% ukitumia mwanga zaidi haitakaa muda huo
-wanatumia wifi kubrowse na sio 3g/4g, ukitumia mobile data muda utapungua
-simu inakuwa mpya simu ya android yenye apps nyingi inakuwa na background process nyingi hivyo hula chaji zaidi.

sababu una iphone compare hizo test mbili utaelewa ni vipi itaongezeka ukaaji chaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom