Mbona iPhone wanatengeneza simu za 256GB, hebu niambie we unatumia simu gani na internal storage ni ngapi na wewe umeweka sd ya ngapi inayopita hiyo 256GB!?
Hujaelewa somo.
Simu zinavyoelekea sasa hivi zinakwenda kuwa zinaongezewa accessories zaidi. Ndiyo maana kuna mpaka vionjo vya nyongeza kwenye camera ukitaka kupiga picha vizuri zaidi. Au unaweza kuunganisha simu yako na home security system etc.
Kwa hivyo, simu kuwa na sehemu ya kuwekea external storage ni muhimu sana kwa watu wanaotaka kutumia teknolojia ya sasa.
Simu zinataka kuwa kama computer, ushaona computer ambayo haina kabisa uwezo wa kuwa na external storage?
Nitakupa mfano kuelezea zaidi.
Mimi nina SD card kama kumi za 64 GB na kumi nyingine za 128 GB. Kuna moja imejaa documentaries za Al-Jazeera tu, kuna nyingine imejaa muziki wa Hip Hop tu, kuna nyingine zinajaa TV series tu, kuna nyingine zimejaa HD movies tu, kuna nyingine zimejaa vitabu tu (epub, pdf, mobi etc), kuna nyingine zimejaa audiobooks tu, kuna nyingine zimejaa R&B Soul muic tu, kuna nyingine imejaa classical music tu, kuna nyingine imejaa bongoflva tu, nyingine imejaa documentaries za PBS tu, nyingine imejaa documentaries na shows za BBC tu etc.
Muda wowote nikijisikia kuweka sd card yoyote kati ya hizi naweza kuweka kwenye simu nikatumia.
Wewe unayetegemea 256GB za simu yako - kama unaweza ku afford hiyo simu ya 256 GB, ambayo by the way iko ridiculously overpriced ukilinganisha na bei ya sd cards mbili za 128GB- huna uwezo wa kubadili SD cards ili uamue on the fly kuangalia documentaries za Al-Jazeera au any of the other alternate items listed above.
Choice is always a good thing, even if you are not using it,Just having it is liberating.
Inawezekana level yangu ya udadisi iko tofauti na yako na ndiyo maana wewe unaona GB 256 ni nyingi sana na mimi nakushangaa.
Unanikumbusha mwaka 2000 nilikuwa jengo la IPS hapo katikati Dar katika mizunguko ya kazi. Nilikwenda ofisini kwa jamaa mmoja. Tukawa katika mazungumzo kuhusu maisha, mapambano ya kutafuta hela na kuridhika. Basi kukawa na jamaa mmoja kama mesemja hivi wa pale ofisini, akaulizwa, hivi wewe kwa sasa ukipata kiasi gani cha fedha utaridhika kabisa?
Yule mesenja akajibu. Mimi nikipata shilingi milioni 100 nitaridhika kabisa.
Kwa mahesabu yake, milioni 100 - si hela ndogo kwa wakati ule- ilimtosha kabisa.
Basi yule bosi akashangaa sana inakuwaje mtu aridhike na milioni 100. Kwa sababu yeye alikuwa anaipigia hesabu hela ile kwa matumizi yake, kulipa kodi ofisi kubwa IPS, mafuta ya magari ya ke ya binafsi na ofisi, kodi, mishahara ya wafanyakazi etc etc. Kwake milioni 100 ilikuwa hela ndogo sana.
Sasa siwezi kushangaa unapoona GB 256 ni nyingi sana wakati mimi kila baada ya miezi miwili inanibidi niongeze angalau 2TB za storage katika network yangu.
By the way, natumia simu inayo support 1TB external storage, ingawa hizo sd card bado hazijawa widely available kwenye soko.