Soma vizuri mkuu mimi nimetaka kujua marais tena marais wa nchi zinazotuzunguka sio mabalozi, pia nimetaka kujua walipanga mipango gani ya pamoja ambayo itaendeleza wananchi wa nchi husika. Hatupo hapa kukejeli la hasha nimetaka tujadili mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu bila kutake advantages zilizopo katika nchi nilizozitaja. Naomba ujikite kwenye mada mkuu sio kudefend tu bila kueleza nini kinafanyika hatutaweza kuendelea kama hatutajadili rootcauses za matatizo yetu.Jaman acheni hizo mkuu wa nchi huwa anapokea ugeni wa viongozi wakubwa toka ughaibuni mara kibao. Nafkr ndiye rais aliyepokea viongozi wengi ambao ni popular duniani zaidi ya marais waliopita.
Pia tusibeze kabila au eneo atokalo mkuu wa nchi, tatizo la mtu mmoja lisifanywe la wote. Wapo wakwere na watu toka pwani ambao utendaji wao umetukuka. So plz JK has nothing to do with wakwere and pipo from magogoni.
JK ni mkuu wa nchi na rais wetu pia aliyewekwa madarakani kwa mujibu wa katiba na demokrasia. Hivyo kama mkuu wa nchi ajengewe na kupewa heshima. Sikatai yeye kukosolewa, ila ukosoaji mwingne umevuka mipaka na maadili.
Naomba mtu aconfirm hapa kwamba, Mwai Kibaki hawajahi kukanyaga TZ toka Jakaya
awe Rais. noting that Kenya is the East African Giant Economy.
tena alikuwa na wale wazungu wa symbion power.Si juzi Hillary Clinton alikuja kukagua mashamba ya mchicha pale mlandizi hamkumwona? Acheni unafiki
Si juzi Hillary Clinton alikuja kukagua mashamba ya mchicha pale mlandizi hamkumwona? Acheni unafiki
Wamtembelee Rais wa viwango vya kina 50%, Eminem, Lil Bow Wow, Lil Wayne kwa lipi la maana?
Serikali yake haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe !!!
Nimekuwa najiuliza kwa muda sasa kwa nini raisi wetu hatembelewi na marais wenzake? Kipindi cha Mkapa tulikuwa tunashuhudia dhifa za taifa nyingi namaanisha sherehe za marais (mgeni § mwenyeji).
Najiuliza rais wetu hana joint programs/projects between countries?
Hii inatia shaka mustakabali wa taifa kwamba tuna kiongozi ambaye hana objectives katika uongozi wake. Labda Mkapa alikuwa na projects/ideas za kuendeleza nchi za Africa na ndio maana maraisi wa Malawi, Botswana, Msumbiji, nk walikuwa wanakuja kuanzisha joint projects kama Mtwara corridor ili kuendeleza wanachi wa nchi husika.
Mimi naamini katika ushirikiano wa waafrika katika kujiendeleza kuliko kuwategemea developed countries ambao hatuna common interests and similar problems.
Nipo tayari kukosolewa

Mzururaji anatembelewa?
Kama yeye anawatembelea, wao hawana haja ya kuja huku kwetu. Nakumbuka alikaa na George W Bush hapa kwa zaidi ya siku tatu. Moja ya ziara ndefu kabisa kwa Rais wa Marekani kukaa nchi moja kwa muda huo.
Mkuu unamaanisha ndie aliyekuja kuchukua wale Twiga?Ametembelewa na Gadafi! Hii ilikuwa ni mara tu baada ya ile vita ya libya kuanza! Jamaa aliingia bongoland usiku usiku akaongea na mjomba halafu akajikataa usiku huo huo!