Kwanini rais wetu hatembelewi?

Nimekuwa najiuliza kwa muda sasa kwa nini raisi wetu hatembelewi na marais wenzake? Kipindi cha Mkapa tulikuwa tunashuhudia dhifa za taifa nyingi namaanisha sherehe za marais (mgeni § mwenyeji).

Najiuliza rais wetu hana joint programs/projects between countries?

Hii inatia shaka mustakabali wa taifa kwamba tuna kiongozi ambaye hana objectives katika uongozi wake. Labda Mkapa alikuwa na projects/ideas za kuendeleza nchi za Africa na ndio maana maraisi wa Malawi, Botswana, Msumbiji, nk walikuwa wanakuja kuanzisha joint projects kama Mtwara corridor ili kuendeleza wanachi wa nchi husika.

Mimi naamini katika ushirikiano wa waafrika katika kujiendeleza kuliko kuwategemea developed countries ambao hatuna common interests and similar problems.

Nipo tayari kukosolewa

Hana mvuto wa kutembelewa.
 
Tanzania ya kikwete haivutii watu wengine kuja, nyumba yake haiko sawa mgeni gani atakuja,,aweke sawa nyumba yake kwanza na watu watatamani kuja kufanya bilateral za hapa na pale. aibu tupu. jamaa halijakomaa kiuongozi toka 1995 mwalimu alipolisema, kubavu!!!
 
Hana mawazo ya kuliendeleza taifa na Africa, yeye anajua soln ya matatizo yetu ni misaada bila misaada tutakufa si ndo anvyosema, wakati wenzake wanaotumia internal resources yeye anategemea external resources hence two different ideas. Afu wamesha mjua ni parpet wa marekani hana msaada Africa.
 
Si juzi Hillary Clinton alikuja kukagua mashamba ya mchicha pale mlandizi hamkumwona? Acheni unafiki
Mchicha unamsaidiaje mtanzania wa hali ya chini? Tunahitaji projects za ukweli katika miundombinu ya kududumu kama reli,barabara za kuunganisha nchi na nchi, makubaliano ya kibiashara kama Zuma alipokwenda Rwanda alivyofanya nk.
 
Hamkumbuki wiki mbili zilizopita Museveni alitua Dar!
Eehe tuambie wanampango gani wa pamoja labda? kama zaidi ya m7 kuja mlimani kupiga picha na SP yake ya miaka ya sabini aibu tupu!!!
 
Isije ikawa US inamtumia JK kuleta majeshi kule Uganda maana M7 kaja juzi leo tangazo la majeshi ya US yako Uganda hii imekaaje ? So ni broker jamaa baada ya kutumaliza hapa Tanzania kwa kutuuza au hii imekaaje ?
 
.....labda waje kwa meli maana AIRPORT kila siku hakuna umeme wala mawasiliano so hawako tayari ku-risk maisha yao! hata hivyo raha ya kumtembelea mwenzio umkute nyumbani, sasa kila siku mwenzio yuko kwenye viwanja vya kahawa anaganga njaa!

Mpwa kwani bandarini umeme upo wa uhakika?
 
Nimekuwa najiuliza kwa muda sasa kwa nini raisi wetu hatembelewi na marais wenzake? Kipindi cha Mkapa tulikuwa tunashuhudia dhifa za taifa nyingi namaanisha sherehe za marais (mgeni § mwenyeji).

Najiuliza rais wetu hana joint programs/projects between countries?

Hii inatia shaka mustakabali wa taifa kwamba tuna kiongozi ambaye hana objectives katika uongozi wake. Labda Mkapa alikuwa na projects/ideas za kuendeleza nchi za Africa na ndio maana maraisi wa Malawi, Botswana, Msumbiji, nk walikuwa wanakuja kuanzisha joint projects kama Mtwara corridor ili kuendeleza wanachi wa nchi husika.

Mimi naamini katika ushirikiano wa waafrika katika kujiendeleza kuliko kuwategemea developed countries ambao hatuna common interests and similar problems.

Nipo tayari kukosolewa

Labda Kila wakitaka kuja wanaambiwa kaenda Jamaica kwenye bembea
 
Rais wa kwanza wa american kuja Tanzania ni George W.Bush mwenyeji wake alikua Kikwete

Eehe tuambie waliweka program gani za kutuendeleza watanzania? Kama sio kutuletea neti na sisi kumpa migodi mingi zaidi nini tangible kwetu hasa?
 
kweli jamaa anashindwa kusoma game.
yaani yeye kutembelea tu wakati hatembelewi
na anaendelea tu kwa raha zake......
kuna tatizo hapa.....
 
Jamani mbona hivi karibuni alikuja rais wa Somali, Comoro, au mnataka mpaka aje Obama ndipo mjue rais wetu anapendwa?
 
Jamani mbona hivi karibuni alikuja rais wa Somali, Comoro, au mnataka mpaka aje Obama ndipo mjue rais wetu anapendwa?
Rais wa Somalia alikuja kuomba msaada, Commoro alikuja kushukuru kwa jeshi letu kumfukuza generali muasi hakuna cha maana kama thread inavyohitaji.
Hatumuhitaji Obama tunahitaji maraisi wa nchi za africa hasahasa nchi zinazotuzunguka kuna opportunities nyingi sana za kuchukua advantage.
Mfano sisi tuna bahari Malawi, Zambia hawana tungeweza kuimarisha usafiri wa reli kutoka Mtwara mpaka huko distance ni ndogo sana hapa, sasa na hili nalo tunashindwa?
Sisi tuna ardhi na kenya kuna njaa, congo kuna vita tungeweza kuwa na makubaliano ya kuwauzia chakula hasa mahindi yanayooza kule Rukwa.
 
Back
Top Bottom