Kwanini Rais hajiungi JamiiForums?

Kwanini Rais hajiungi JamiiForums?

Ukiweza kujijibu wewe mwenyewe kwamba kwanini ajiunge kwenye jamii forums? then, huna haja ya kuuliza hadhira hii swali hapo juu. Kingine labda, ingekua vyema ufanye tafiti ili uweze kujua je hadhira hii inamuhitaji mueshimiwa Raisi?
 
Boss Red Giant Heeeheeee, Umenichekesha sana. WaTanzania tuna akili sana ila sijui kwanini bado tunasuasua kwenye Maendeleo. Ulikuwa unafikiria nini?

Itakuwa ameshauriwa asijiunge na ID yake ila natumaini yupo humu na ID fake.

Tatizo WaTanzania hawatamkopesha. Watamjia na Evidence na Source za nguvu.

My Take: Wazo lako ni Zuri, Hope Wasaidizi wake watamfikishia hizi habari na atajiunga Rasmi na ID yake ambayo si fake. Rais umeombwa ujali Vitu vya ndani. Jiunge na ID yako humu JF.

Serikali imekuwa ikihubiri kuhusu kutumia vitu vya nyumbani kwanza, sasa iweje yeye kama Rais anaenda kutumia Twitter na kuacha jamiiforums. Yote hii ni mitandao ya kijamii na changamoto zake zinafanana sana. Rais angeiunga mkono JF ingeweza kukua sana kwa watu wengi kujiunga.

Kwa kusema tuache kukimbilia bidhaa za nje naomba Rais na baraza lake waonyeshe mfano kwa kuanza kujiunga jamiiforums. Karibu sana mheshimiwa John Pombe Magufuli.
 
Siku nyingi tu si ndiyo sababu huwa anatokwa na povu zito na kudai ni mitandao ya hovyo hovyo, mara anatamani mashetani yashuke yaje kufunga mitandao yote nchini. Yumo humu ila anaingia kwa kificho sana hatakI ID yake mtu yeyote hata pale Ikulu aigundue. Hupenda kuingia humu usiku wakati pale Ikulu pametulia.

Ha ha ha ha ha ha, Mbona yupo humu.
 
Nguvu mnazotumia hapa mngejikita kufanya kazi basi Taifa lingepiga hatua..

Mniombee
 
unataka aache kuingia MMU na kutoa visa vyake huko?
yupo humu
 
Rais hatakiwi kujificha. Au naye anataka kutumia haki ya kudare to talk openly🙂
hapa jf wengi tunajificha. Yupo humu kila siku hata ID yake naijua. tena anapatikana sana kwenye jukwaa flan hivi sio SIASA.
 
Hakuna mwana siasa wa tanzania asiyekuwa na ID hapa JF wote wapo umu kutwa tunakwaruzana nao humu
 
Yupo humu au watu wake wanampa za humu...wewe toa ushauri tu wa kitaifa na maendeleo itamfikia..
 
Mh.. Rais yupo humu nafikiri ID yake itakua imeandikwa kisukuma
 
Back
Top Bottom