OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,243
- 103,945
Katika maisha ya kawaida mtu unaweza kumlisha,kumpeleka chooni,kumuogesha,kumvisha nk lakini bado akakununia na kukusema vibaya kwa watu. Ndani ya familia mke anaweza kumpa mumewe kila kitu,lakini bado akadundwa na familia ikaendelea. Hizi ni principles za kawaida kabisa.
Sasa iweje katika nchi ya kidemokrasia rais alazimishe watu kumuunga mkono.
Je, rais hatambui mawazo kinzani na mbadala.Hivi kweli hakuna jema ambalo linaweza kupatikana katika kupigwa huko?Mbona Tundu Lissu akimpinga Rais lakini leo hii tunaona mnapita mlemle?
Kinachonishangaza zaidi ni rais kuhusisha "Mashehe wa Lowasa" na matukio ya Kibiti!
Sasa iweje katika nchi ya kidemokrasia rais alazimishe watu kumuunga mkono.
Je, rais hatambui mawazo kinzani na mbadala.Hivi kweli hakuna jema ambalo linaweza kupatikana katika kupigwa huko?Mbona Tundu Lissu akimpinga Rais lakini leo hii tunaona mnapita mlemle?
Kinachonishangaza zaidi ni rais kuhusisha "Mashehe wa Lowasa" na matukio ya Kibiti!
Ndugu yangu tema chini.
Siasa na madaraka sio jambo la kujidai nalo leo ni hisia na miongozo ya kibinadamu.
Miaka 20 iliyopita mtu angemuuliza Lowasa kuwa kuna siku chama cha CCM kitageuka kuwa ni mtesaji wake mkuu na watawala aliofanya nao kazi kwa umoja na kutembea kifua mbele kama marafiki na mara nyingine kuwasaidia kwenye majimbo yao mpaka wakashinda ubunge angepinga vijali na mara nyingine ungeitwa mchochezi na mfitinishi tena unataka kuwagambanisha viongozi na chama chao.
Tafakari!!!
Leo hii Lowasa na wengineo wamekua ni wahanga juu ya matamshi yao amaboyo mara nyingine wanayatoa kwa nia njema wakiamini kuwa wanawaambia watu miaka mitano iliyopita walikuwa marafiki na watawala pamoja.
Tafakari!!!!!!!!!
Usijivunie kile unachokishabikia leo hata kama kina kiuka haki za wengine. Ni bora ukae kimya mana ni wazi kuwa wanayoyasema wale usiowakubali yapo mengine yana ukweli na hekima na yanazungumzwa na jamii pana.
Suala la mtu kukaa gerezani tu bila kuhukumiwa kwa miaka nenda rudi wen lisikie tu kwa watu wengine lakini omba Mungu sana ili akuepushe na balaa hilo na pia onyesha huruma kwa hao wanaofanyiwa hivyo mana nao mara nyingine hawakupenda ila tu yamewakuta kutokana na tofauti za kiimitizamo tu.
Tofauti hizo hizo kama zitaendelea ipo siku utajikuta uko upande wa pili wa kupingana na wale usio wataka leo huku wao wakiwa na mamlaka ya kukufanyia hayo unayoona ni haki wao kufanyiwa leo.
Ndio maana watu wengi wasioamini sana katika vyama na itikadi za vyama vya kisiasa wanapigania suala la Haki za Binadamu na utawala bora wa kusimamia katiba na sheria zilizopo. Wanajua kuwa Mahakama ndicho chombo pekee cha kutoa haki na sio vinginevyo. Wanajua kuwa watu wanaweza kwa makusudi kuchochea na kuharibu tamko lenye nia njema ya mtu yeyote na hata kumuangamiza kwa makusudi kwa sababu tu ya chuki. Lakini endapo mtu atafikishwa mahakamani basi mahakama inatoa nafasi ya kusikiliaza na kuchambua ili kujua nia ovu ya mtu ya kauli au kitendo kuliko kuwaacha tu watawala wakaamua na kuhukumu juu ya wale wasio wapenda. Sio jambo zuri sana kisiasa na kijamii.
Ni vizuri kila mtu akafuata sheria na kuheshimu vyombo vya dola. Lakini pia vyombo vya dola viheshimu haki za mtu mstarabu ambaye hajafanya ukaidi. Mtu aliwa matarabu asifanyiwe ukatili kwa sababu tu ya kuwafurahisha watawala
Hayo yalifanywa wakati wa Yesu alikuwa mtu mstarabu lakini alitendewe unyama na kuuawa kwa ajili ya watawala wa enzi hizo kutaka kulinda madaraka na himaya zao.