Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Mkuu tafadhali tuombe radhi ndugu yangu....! Yaani unataka kufananisha siasa na taaluma? Workload ya mwanataaluma ni nzito kuliko mwanasiasa....! Think twice..!

nimekupenda bure hapa
 
ushabiki unaouzungumizia sijauona
kuna upungufu wa Wanataaluma pale UDS. sasa why not take Baregu????

Mkuu tatizo langu sio specifically kwa Baregu.....ila ni hii justification ya upungufu wa wanataaluma. Recruitment katika vyuo vyetu vya Umma iko very poor, sasa kila anayestaafu wanamuongezea muda.....why? Ukienda baadhi ya departments pale UDSM au hata SUA utakuta mvi tupu wote senior lecturers hakuna hata ka-tutorial assistant kamoja! Wakati ilipaswa kuwe na sustainable recruitment ie tutorial assistants, assistant lecturers, lecturers, senior lecturers etc. Hii inasaidia katika kuridhisha ujuzi wako kwa wale unawaandaa kushika nafasi hizi muhimu za kitaaluma.

Sasa kuendelea kung'ang'ania watu mpaka meno yatoke mdomoni wawe vibogoyo sio tija! Halafu pia suala la financial gain tusilikwepe....wengi wanataka kuongezewa muda waendelee kupata ulaji....iwe Baregu, mimi, wewe au hata yeyote. Nakumbuka SUA kulikuwa na registra pale Prof. Lwoga, alipostaafu alichoka mbaya ilibidi wakuu wazuge wampe mkataba wa kufundisha angalau ku-rescue hali yake...lakini Mungu mkubwa mwishoni mwa mwaka jana JK kamkumbuka...! Sometimes siasa pia zimo...sikatai
 
nimekusoma mkuu wangu!! tupo sambamba sasa!!
 
He must go, y is trying to stay,let fresh blood take over.We don't need him
 
Well done Mrs Ghasia, Baregu is too old to stay . He must go.Unemployment rate is too high to keep his job.
 
haya sasa unadrain brain!!!!!!!!!!! yaani wewe kwako wafe njaa upeleke mkate kwa jirani???

Of course kama kufa kwa njaa ndio mnakokutaka ni bora mfe kabisa..Mtu ni professor lakini bado mnaleta siasa kwenye education why not...AENDE KWA KAGAME TU HUKO WATAMJALI SANA.
Ndio maana mimi kwetu ni bongo lakini sirudi huko ng'oooo.Hiyo brain drain na iwe tuu ...huoni kuna watu hapa wanamlinganisha na Kingunge How??????Professor na Kingunge?????mmmhh haya banaah.
 
Mkuu tafadhali tuombe radhi ndugu yangu....! Yaani unataka kufananisha siasa na taaluma? Workload ya mwanataaluma ni nzito kuliko mwanasiasa....! Think twice..!
Nahisi umedandia treni kwa mbele Kwetu ni Kwetu!

Hakuna cha workload wala nini, zote ni kazi zenye dhamana kubwa kwa Jamii. Hujui kuwa maamuzi ya mwanasiasa ndio yanayoamua hatma ya nchi? Hujui ushauri wa Kingunge ndio uliotufikisha hapa tulipo (especially kama anaendelea kushauri hadi sasa)?.

Kuna wasomi kibao walipitisha umri wakastaafu na bado wakaendelea kutumikia taifa kwa mkataba na mafanikio makubwa. ndio maana nikasema, wanaoshabikia Baregu atundike daruga, wanamtazamo gani kuhusu kingunge kuendelea kuwepo kazini hadi sasa?

Nije kwako sasa, kwakuwa workload ya Siasa ni ndogo kuliko ya taaluma (kwa mtazamo wako), kwahiyo ni sawa kwa wanasiasa kuzeekea maofisini?
 
Na mi pia namshauri Prof. asing'ang'anie UDSM aende vyuo vingine, kwa sasa Tanzania ina vyuo vingi sana.
 
Na mi pia namshauri Prof. asing'ang'anie UDSM aende vyuo vingine, kwa sasa Tanzania ina vyuo vingi sana.
Baregu si kwamba ameng'ang'ania, yeye amepeleka maombi ya kuongeza mkataba. Unatakiwa ujue ameng'ang'aniwa na wanataaluma wenzake (UDASA + Idara ya Sayansi ya Siasa & Utawala) ambao wameona umuhimu wake. Si kwamba kuwepo kwake kutawabania vijana, kwani hao vijana wengi wao wapo masomoni.
 
Mimi sina pingamizi na hilo nami ningependa sana Prof awepo UDSM kwa sababu anatufaa sana na ndio maana hata hao wote wanamtaka lakini panaonekana kuna wakubwa fulani wanaona kwao ni mwiba yeye kuwepo na ndio maana nikashauri hivyo sina maana kwamba anawabania vijana.Katika Institution kubwa kama UDSM ukasema eti wazee sijui vyevyote utavyoweza kuwaita waondoke na wabadili vijana watupu sidhani kama chuo kinaweza kwenda vizuri na hasa tukizingatia Taaluma na hekima na heshima ya kimataifa walionayo hawo watu ukizingatia kwamba vyuo vikuu husifika sana kutokan na Maprof. wliopo. Kwa hiyo ushauri wangu uli base hapo. Tuko pamoja.
 
Of course kama kufa kwa njaa ndio mnakokutaka ni bora mfe kabisa..Mtu ni professor lakini bado mnaleta siasa kwenye education why not...AENDE KWA KAGAME TU HUKO WATAMJALI SANA.
Ndio maana mimi kwetu ni bongo lakini sirudi huko ng'oooo.Hiyo brain drain na iwe tuu ...huoni kuna watu hapa wanamlinganisha na Kingunge How??????Professor na Kingunge?????mmmhh haya banaah.

nimekusoma!!!!

hapo kwenye bold mkuu unahasira duh!!! rudi bana mbona hata rais kila akija huko anawasihi sana mrudi tuone matunda yenu??
 
nimekusoma!!!!

hapo kwenye bold mkuu unahasira duh!!! rudi bana mbona hata rais kila akija huko anawasihi sana mrudi tuone matunda yenu??

Matunda gani zaidi yakutaka kutufisadi tukirudi??mfano mzuri Dr.aliyerudi kuanzisha hospitali ya kutibu mioyo....sana sana amejazwa mifrustrations tuu.Acha tujilie kuku bana tukichoka tutarudi tu si kwetu.
Nchi gani watu wamekazana kujenga maghorofa tu bila kudumisha miundo mbinu.
 
hahaaa lol!!! discouraging jamaa wanampa mifrastasheni kweli lakini!!!! anaujutia uzalendo wake sasa!!!!

nimestuka kuna memba mmoja signature yake inasomeka 'I hate Tanzani' (naweza kuimajini anachojisikia ndani mwake)
 
Katika vitu ambavyo JK alichemka ni kumuweka Mkandara kuwa VC pale UDSM-Chuo kilikuwa kinahadhi sana ndani na nje ya Tz.Mkandala anchukulia urafiki wake na JK kama fimbo ya kuamulia mambo hata kama ni ya kipuuzi.Chuo kinaanza kufulia na ndo maana watu kibao siku hizi wanakwenda Mzumbe,SUA,UDOM,ARU na kwingineko ili kupisha uoza uliopo UDSM usiwaambukize!Mkandala na wenzako wa CCM....."let us agree to disagree...."!
 
Nahisi umedandia treni kwa mbele Kwetu ni Kwetu!

Hakuna cha workload wala nini, zote ni kazi zenye dhamana kubwa kwa Jamii. Hujui kuwa maamuzi ya mwanasiasa ndio yanayoamua hatma ya nchi? Hujui ushauri wa Kingunge ndio uliotufikisha hapa tulipo (especially kama anaendelea kushauri hadi sasa)?.

Kuna wasomi kibao walipitisha umri wakastaafu na bado wakaendelea kutumikia taifa kwa mkataba na mafanikio makubwa. ndio maana nikasema, wanaoshabikia Baregu atundike daruga, wanamtazamo gani kuhusu kingunge kuendelea kuwepo kazini hadi sasa?

Nije kwako sasa, kwakuwa workload ya Siasa ni ndogo kuliko ya taaluma (kwa mtazamo wako), kwahiyo ni sawa kwa wanasiasa kuzeekea maofisini?

Kama uwezo wa kupima nilichoongea huna basi......!
 
8th January 2010

Baregu%282%29.jpg

Profesa Mwesiga Baregu

Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, ameitaka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma iweke wazi sababu za kukataa kumwongezea mkataba wa ajira chuoni hapo na amesema kuna nia ya makusudi ya kumdhalilisha.
Alisema alishangaa na kupata mshituko baada ya kuona kati ya majina ya wahadhiri 23 walioombewa kuongezewa mikataba ya ajira na chuo hicho kwa menejimenti hiyo ni jina lake tu lilikataliwa.
Akizungumza jana na Nipashe, Profesa Baregu alisema mwanzo hakuamini alichokiona na alidhani ni matatizo ya uchapishaji yaliyosababisha jina lake lisionekane, lakini baadaye alibaini kuwa kilichotokea ni cha kweli.
"Hii ni aibu kweli, maana katika wahadhiri 23 walioombewa mikataba 22 walikubaliwa isipokuwa mimi tu, niko hapa Mlimani kwa miaka 15 nafundisha na kwa utumishi wangu sikutarajia kabisa kukataliwa na kibaya zaidi sikupewa maelezo yoyote, sasa kama sababu ni kuwa Chadema basi waseme," alisema.
Profesa Baregu ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
Aliongeza kuwa katika miaka yake yote ya utumishi chuoni hapo hakuwahi kulalamikiwa na wanafunzi anaowafundisha au wakuu wa idara hivyo anashangaa kukataliwa kuendelea kufundisha.
Alisema kuwa litakuwa jambo la aibu itakapokuja kubainika kuwa kukataliwa kwa mkataba wake kumechangiwa na sababu za kisiasa kwa kuwa chuoni hapo kuna wahadhiri ambao ni wafurukutwa wa CCM, lakini wanafundisha bila matatizo.
"Silazimishi waniajiri ila ninachotaka ni maelezo ya sababu ya kukataa kuniongezea muda mkataba wangu, kuninyima mkataba mimi kuna watu wengi unakuwa unawakomoa maana huenda wanahitaji mchango wangu...Wanafunzi wangu na wenzangu ambao tunasaidiana kitaaluma," alisema na kuongeza kuwa haamini kuwa iwapo angekuwa CCM angekutwa na mkasa huo.
Profesa Baregu alisema mwaka jana uongozi wa chuo hicho ulimweleza kuwa umepeleka majina ya wahadhiri 23 likiwemo lake kwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuomba waendelee na utumishi wao chuoni hapo baada ya kustaafu.
Alisema lakini ilipofika Septemba mwaka jana chuo hicho kilimpa barua kikimweleza kuwa Utumishi wamekataa kumwongezea mkataba.
"Tangu nipewe barua nimekuwa nikihoji sababu za kukataliwa mkataba wangu sipati majibu, Makamu Mkuu wa Chuo alisema yalienda majina 23 yakarudi 22, mimi tu ndiye jina langu halikurudi, nataka kujua nini kilitokea," alisema Profesa Baregu, ambaye amebobea katika mahusiano ya kimataifa.
Hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya chuo hicho, Dk. Benson Bana, alisema Menejimenti ya Utumishi wa Umma imekataa maombi ya Baregu kuendelea kufundisha katika chuo hicho.
Rehema Mbulalima wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano katika Menejimenti hiyo, alisema juzi kuwa wamepekua orodha hiyo tangu Juni mwaka jana, lakini hawakuona ombi la Profesa Baregu.
Dk. Bana alithibitisha kuwa ombi la Profesa Baregu lilishafikishwa Utumishi.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alipoulizwa iwapo ombi la Profesa Baregu lilipelekwa utumishi na majibu waliyopata ni yapi, alisema atatoa jibu la nini kinachoendelea baada ya wiki mbili.
Dk. Bana alisema kuwa bado anamhitaji Profesa Baregu katika Idara yake kwa asilimia 150 na hata chuo kikuu kizima kinatamani arejee kazini.
Hatua ya kutomwongezea mkataba wa ajira Profesa Baregu kumesababisha malalamiko kutoka kwa Chama cha Wanataaluma wa chuo hicho (Udasa), ambao hivi karibuni walitishia kuwa kama hataongezewa mkataba wataandamana.

CHANZO: NIPASHE
 
Kocha wewe, refa wewe! duh, hausaidiki. Ungejibu hoja zangu basi ningeona kweli una uwezo!

Nimeshatoa mawazo yangu kwenye hili, sasa kuendelea kubishana tu ilimradi kujaza maneno kwenye forum sio tija. Kama unafikiri mwanasiasa na mwanataaluma workload yao ni sawa hayo pia ni mawazo yako anaeyakubali atayapokea. Unapofananisha Kingunge na Wanataaluma sijui unatumia vigezo gani? Kwani kwenye siasa kumewekwa kikomo cha umri? Unafikiri waliotoa wazo la kuwepo kikomo cha utumishi kwa kutumia umri walikurupuka tu na kuweka? Kwanini kwenye siasa hakuna hicho kikomo...? Mugabe leo ana miaka zaidi ya themanini bado yuko madarakani.....unafikiri hicho ndio kipimo kwa kuwa Mugabe bado yupo kwenye siasa basi hata mwanataaluma mwenye umri huo aendelee kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri akiwa mwajiriwa kwenye vyuo vyetu?
 
Back
Top Bottom