Kwanini Polisi walishindwa kuifichia aibu familia ya Mzee David Makerege? Yesu aliwaambia "asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza kumtupia jiwe"

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Kwanza kabisa ninaomba kuanza kwa kunukuu maneno machache ya waziri wa mambo ya nje mzee wetu professor Palamagamba Kabudi. Pia kabla ya yote ikumbukwe ninaandika haya nikiwa sina "vested interest" undugu, ujamaa wala urafiki na mzee Makerege wala familia yake. Hawanijui wala siwajui "personally" lakini mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.

Kuna siku moja nikiwa ninatazama video za zamani za vikao vya bunge huko mjini Dodoma, katika mtandao wa youtube nilipata fursa ya kutazama clip moja ambayo mchangiaji alikuwa ni mzee Kabudi.

Katika mchango wake ule mzee Kabudi alipata kusema maneno haya "Katika Wizara ambazo zinapaswa kuongozwa kwa hekima na busara kubwa ya hali ya juu basi ni Wizara tatu tu ambazo ni katiba na sheria, mambo ya nje pamoja na wizara ya mambo ya ndani"

mzee.JPG

Mimi sio mzee Kabudi na wali siwezi kuisemea nafsi yake lakini sidhani kama alimaanisha wizara zingine zinapaswa kuongozwa na mawaziri ambao ni "vilaza" lakini wizara ya mambo ya ndani ni wizara inayogusa maisha ya watanzania wote kila siku pasipo kujali umri, hali yake ya kipato ama jinsia.

Kwa nchi ambazo zimeweka sheria inayokataza vitendo vya utoaji wa mimba (sijui hapa Tanzania kama hii sheria ipo au la), Wizara ya mambo ya ndani inagusa hata maisha ya mtoto aliyepo tumboni mwa mama yake leo hii nikiwa na maana kwamba mama yule anaweza kushitakiwa endapo atajaribu kufanya kitendo cha utoaji mimba (abortion) ambacho kitaathiri maisha ya mtoto aliyepo tumboni mwake.

Kuna habari zimetapakaa sana katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Mzee David Makerege (umri miaka 80) aliyefariki dunia akiwa chumbani kwenye hoteli jijini Dar es Salaam. Kwa mila, desturi na tamaduni zetu sisi waafrika ipo hivi;

Kuna uzito mkubwa uliowekwa juu ya kuwaheshimu wazee katika tamaduni zetu sisi waafrika, ambao ni sehemu kubwa zaidi ya mila na desturi zetu na ni moja ya maadili ya kimsingi katika jamii. Katika umri mdogo unafundishwa kusalimiana, kuongea na suala zima la ku-interact na wazee kwa njia fulani za kistaarabu na zenye staha.

Kwa mfano, unapofika nyumbani kwa mtu, utoaji wa salamu utaanzishwa na yule aliye mdogo, ambaye baada ya hapo lazima aulize hali ya kila mtu aliyepo (mmeshindaje hapa). Kwa wasichana au wanawake, hii inaweza kuhusisha kupiga magoti, kisha kuuliza kila mtu juu ya afya yake (jamani mnaendeleaje humu). Wavulana na wanaume watafanya vivyo hivyo, lakini kwa kumpa mkono mzee.

Kushindwa kufanya hivyo kunaonekana kuwa ni dharau, na inachukuliwa kama ishara ya malezi duni au ukosefu wa heshima. Ndani ya kaya, babu na bibi wana ushawishi mkubwa. Heshima hii kwa wazee inapaswa kuenea nje zaidi ya familia zetu. Mwanamke yeyote mzee au mwanamume anapaswa kupewa heshima vivyo hivyo hata kama sio ndugu yako.

Sasa ni kipi alichokosea Mzee Makerege mpaka mnashindwa kumfichia aibu ya namna hii? Vp kuhusu familia yake (mke na watoto) mtaani na huko ofisini? Vipi kuhusu wakwe zake na wakamwana?

Vipi kuhusu wajukuu zake huko mashuleni wanaposoma na mtaani wanapoishi? Hawa woooote kwa ujumla wao wataificha wapi aibu hii? Wataweka wapi macho yao?

Leo mzee David kafia Hotelini na mpenzi wake, sasa kesho na kesho kutwa wamekufa wazee wenu kwa namna hii, mtawaanika hadharani?

Kuna kipindi fulani niliwahi kusikia wanasiasa wakipigia kelele sana hili suala la sera ya matibabu bure kwa wazee. Yaaani mzee akiwa anaumwa na kufika katika kituo cha afya atibiwe bure pasipo malipo yoyote au alipie gharama kidogo sana tofauti na yule asiye mzee.

Je, sera hii ililenga katika kulinda utu na heshima ya mzee kama mtanzania aliyekwisha litumikia taifa lake kwa miaka mingi sana na sasa umefika muda wa Taifa kumuangalia yeye.

Kama tunashindwa kulinda heshima za wazee kama akina Makerege ni kweli tutaweza kutekeleza heshima ya kumpa mzee matibabu ya bure?

Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania yangu. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu.

Polisi niliwatetea sana katika sakata la Akwilina (Muhimu Sana: Polisi wakikosea kidogo, isitufanye tukasahau mazuri na mema yote wanayoyatenda) lakini katika hili la mzee Makerege mmeniangusha na mmekosea sana.

TUWE WAZALENDO TUHESHIMU WAZEE WETU. TUSICHAFUE TASWIRA ZAO NJEMA. USTAWI WA NCHI YETU WALIUFANYA WAKIWA BADO VIJANA KWA KUTIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hata kibiashara pia jina la hotel or logde linaharibiwa kiasi navyoona. Kuwa lodge ile kuna mtu alifia ndani. Haijakaa poa, sio?

Wafanye uchunguzi kimya kimya then ripoti wapatiwe viongozi wa familia, najua mitandao ipo lakini kasi ya kusambaa habari haiwezi kufananishwa na habari official kwenye press release ya RPC
 
Back
Top Bottom