MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Martin Luther alishapata cheo cha , 'uaskofu' wakati huo. Dhana kwamba alifuta vitabu 7 napata shida mamlaka hayo aliyapata wapi? Mnyonge mnyonge lakini haki yake mpe
You are lying
 
Wataalamu wanasema hakuna dhehebu linaitwa Roman Catholic bali kuna The Catholic Church. na kweli hili ndilo tunaloliona huku mtaani. Unaona Kanisa katoliki na siyo Kanisa Katoliki la Roma.
nenda kwenye amri za kanisa KATOLIKI ndo utajua kuna kanisa katoliki la Roma
 
KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?

Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.


Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua nhistoria vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.
Lengo la ujumbe nini haswa ndugu
 
Nadahani wana jf sio bora kwasisi wanaimani ya kikristo kukosoana katika imani ebu y amungu tumpe mungu na kaisari apewe yake
 
Duu kumbe bible imefanyiwa EDITING.....?
Imechezewa sana. Wataalamu wanasema biblia tuliyonayo ni nakili ya nakili. Kwa imenakiliwa mara nyingi sana na imetafsiriwa sana hivyo wakti mwingine kupoteza maana ya neno. Lakini tumaini ni kwamba imeandikwa "yote yatapita lakini hata yodi moja ya toreati haitapotea". Hivyo, ujumbe wa neno la Mungu uliuokusudiwa upo pale pale.
 
Imechezewa sana. Wataalamu wanasema biblia tuliyonayo ni nakili ya nakili. Kwa imenakiliwa mara nyingi sana na imetafsiriwa sana hivyo wakti mwingine kupoteza maana ya neno. Lakini tumaini ni kwamba imeandikwa "yote yatapita lakini hata yodi moja ya toreati haitapotea". Hivyo, ujumbe wa neno la Mungu uliuokusudiwa upo pale pale.
Sasa iweje ICHEZEWE halafu maana ibaki pale pale ? kwa kifupi hicho ni kitabu cha story. .na sio cha MUNGU ...
 
VITABU VYA APOKRIFA

(Apocrypha – Hidden)

Apokrifa humanisha iliyofichika, ni maandiko yaliyokuwa yamefichika kwa maana ya kwamba hayakujulikana.

Neno Apocrypha linatokana na neno la kiyunani apokruphos ambalo ni muungano wa maneno mawil apo—mbali ya- na kruptolkruptos—iliyofichwa.

Vitabu vya apokrifa ni vitabu ambavyo Wakatoliki, na WaOthodox wa Urusi huvikubari kama maandiko makuu yanayofaa kufundishia imani.

Vitabu vya apokrifa ni maandiko ambayo yalichapishwa baada ya kipindi cha Nabii Malaki hadi kufikia mwisho wa Karne ya kwanza ya Ukristo.

Baadhi ya Vitabu vya apokrifa tutakavyo viangalia ni

1 Wamakabayo

2 Wamakabayo

Judithi

Tobiti

Wimbo wa Sulemani

Esdras

Baruch

Sira

Ombi la Manase

Hekima ya Sulemani

Walaka wa Yermia

Kutokana na Ushahidi tunaoupata katika agano jipya ni wazi kwamba Wayahudi walikuwa na Kitabu (Vitabu) ambavyo waliamini kuwa ni Sahihi na vinafaa kufundishia—CANON. Vitabu hivyo viliitwa Musa(Sheria), Manabii, na Zaburi au Torati na Manabii au Musa na Manabii. Tazama Math 5:17-18, 7:12, 11:13, 22:40. Luka 16:16-19, 24:27,44 Yohaa 1:45. Mdo 13:15, 24: 14. 28:23 na Rumi 3:2

Mwanahistoria Flavius Josephus (Karne ya Kwanza) akiandika katika mwaka wa 90 alitaja vitabu 24 vilivyokusanya historia ya Wayahudi ya kila ambacho kiliaminika kama Uvuvio.

Vitabu 5 vilindikwa na Musa, Vitabu 13 viliandikwa kati ya Musa na Mfalme Atashasta (Artaxerxes) wa Waajemi. Vitabu 4 vilikuwa vimejumuisha mashairi (vitabu vya Mashairi) na Nyimbo, Zaburi, Methali, Muhubiri, Maombolezo (Against Apion 1:38-40)

Kisha Josephus akaendelea kusema “Ni kweli kwamba Historia yetu imekuwa ikiandikwa toka wakati wa Atashasta, lakini maandiko hayo hayajachukuliwa kuwa ni maandiko sawa na maandiko ya kale ya Mababu zetu. Hii ni kwa sababu, hakuna mfuatano wa Manabii toka wakati huo.

Na ni kwa kiasi gani tumekuwa na msimamo mkali na kuaenze maandiko hayo na kuchunga asije mtu akaongeza katika maandiko—Toka wakati huo, haijawahi kutokea mtu kuongeza maandiko hayo au kupunguza au kufanya badiriko lolote ndani yake.” (Against Apion 1:38-40)

Hivyo Jusephus alishikilia msimamo wa Wayahudi wote kwamba maandiko yote yaliyoandikwa baada ya Utawala wa Atashasta (yaani baada ya Wayahudi kutoka utumwani Babeli) kuwa hayana Uvuvio kwa kuwa hakukuwa na Unbii katika kipindi hicho katika Israel.

Utagundua kuwa Sababu kubwa anayoitoa Josephus ya Kukataa maandiko hayo ni kwasabubu hakukuwa na unabii. Vitabu vyote nilivyovitaja hapo juu viliandikwa katika kipindi hicho.

Vitabu vilivyoorodheshwa na Josephus ndivyo hivyo ambavyo huunda jumla ya Vitabu 66 vilivyomo katika biblia inayokubaliwa na Waprotestant wote duniani. Sababu iliyowafanya waprotestant kuvikataa vitabu hivyo ni Sababu hiyo hiyo iliyotolewa na Josephus. HAVIKUANDIKWA NA MAANABII WALIOTUMWA NA MUNGU. NI WATU TU WALIKUWA WAKIJIANDIKIA HISTORIA NA MAMBO YA WAYAHUDI.

SABABU NYINGINE KWANINI WAPROTESTANT WANAVIKATAA VITABU HIVYO.

  1. Makosa yaliyomo
Yudith 1:17 Nebukadneza ni Mfalme wa Ashuru

  1. Tobit 5:13 Malaika alisema Uongo (Azalia Mwana wa Mzee…)
  2. Tobit 6:1-8. 14 Vinafundisha Uchawi
  3. Baruku 3:4 Baruku Mwandishi wa Yeremia ananukuru Daniel
  4. Baruku 3:4, 12:43-45 Vinafundisha Maombi kwa Wafu.
Niwazi kabisa kwamba Vitabu hivi havina mafundisho yenye Uvuvio na vinapingana na vitabu vingine 66 vya Bibli.

Ndiyo maana basi Biblia inayokubarika kwa Waprotestant wote ni ile yenye Vitabu 66.
4afeded42778d0ad5d8a36d3c9597af8.jpg


Luther did not include the deuterocanonical books in his Old Testament, terming them "Apocrypha, that are books which are not considered equal to the Holy Scriptures, but are useful and good to read."

He also argued unsuccessfully for the relocation of the Book of Esther from the canon to the Apocrypha, because without the deuterocanonical additions to the Book of Esther, the text of Esther never mentions God.

As a result, Protestants and Catholics continue to use different canons, which differ both in respect to the Old Testament and in the concept of the Antilegomena of the New Testament.





And Your protestantchurch won't tell you this..
 
Martin Luther alikuwa ni sehemu tu ya kazi ya matengenezo ya Kanisa.,Kazi hiyo ya matengebezo iliendelezwa Wanamatengenezo Wengine.

Ukitaka kufahamu vizuri soma au pitia Maandiko au vitabu vya roho ya unabii vilivyoandikwa na Helen G.White utapata majibu yote.k.m 'The Great Controversy', Daniel Na Siku Zetu n.k

Kila kitu kimeelezwa au kutafsiriwa kwa kina sana hususani Vitabu vya Daniel na Ufunuo.
 
The Son of Man,
umeandika point kabisa yaan kwa asiye fahamu historia ya kanisa ataponda tu big up sana bro kwa yeyote anayetaka kuelewa juu ya hili ni lazima asome historia ya kanisa kwa kuwa historia ya kanisa imeeleza kwa kirefu juu ya suala la waprotestant.
 
Historia ya Biblia ni kuwa ni Kitabu kilichotengenezwa na Kanisa Katoliki na kukamilika mwaka 300 Ad...Ilikamilika ilkiwa na vitabu 72/73 ila baadae Martni Luther aliondoa vitabu 7 na kubakiwa na vitabu 66.,
Hakuishia hapo, aliondoa vitabu 3 vya Agano jipya....Biblia ya Martin Luther ilikuwa na vitabu 39 vya Agano La Kale na Vitabu 24 vya Agano jipya..

Reformer mwenzake Calvin ndiye aliyemsihi kuvirudisha vitabu 3 ya Agano jipya..
Naona hoja hizi mbili hawazijibu wanarukaruka tu kama chura yaan hao wenyewe wanakinzana wenyewe kwa wenyewe
Kwa kifupi Martin luther naweza kusema alikuwa ni Opportunistic...Alipata loop hole ya kuondoa vitabu vya Agano la kale, baada ya kurejea mitaguso ya Kanisa(hasa mtaguso wa trent) masahihisho yanahitajika hapa....


Wakati Kanisa Katoliki lina-compile Bible, Kuna vitabu 7 vya Agano la Kale ambavyo vilipokelewa kwa lugha ya Kigiriki...Hivyo Wayahudi(Waisrael) hawakuvitambua vitabu hivyo simply bze of language....Hivyo Luther akatumia mwanya huo kuviondoa....

Ila alishindwa kuondoa vya Agano jipya maana hivyo vilikuwa nje ya uwezo wake.....Ila ni bahati tuu, maana alisha viondoa vitabu 3... Calvin alimsihi sana kuvirudisha...

Kituko
 
PSB - Martin Luther complete documentary ( part 1 & 2)
Excellent documentary to understand history and the separation from the catholics.
 
Back
Top Bottom