Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,330
Hongera unayejua.Na sanamu ya maria inachukua nafasi gani kwenye utatu wenu unaoujua?
Sanamu ya Maria inatuonyesha na kutukumbusha mama wa Mkombozi wetu
Kwenye utatu mtakatifu, Mama Maria ndio Binadamu pekee aliye ishi na kuenjoy utatu mtakatifu wa Mungu, 1: Mimba yake ilikuwa ni kwa uwezo wa Roho mtakatifu, na aliambiwa mimba itatungwa baada ya kumpokea roho mtakatifu, na pia yeye ndie Binadamu wa Kwanza kumpokea Bwana Yesu, so kwenye utatu Mama maria ni kiungo kikubwa kati Mungu na Mwanadamu.
Mama Maria ni Sanduku la Agano, Sanduku la Agano ndilo liliokuwa linakaa Sheria alizopewa Musa, Na Yesu ndio Baba wa hizo Sheria na ndio Sheria yenyewe na alikaa ndani ya Mama Maria Mkingiwa wa Dhambi ya Asili,
kwenye Sanduku la Agano kulikuwa na Sanamu za Malaika wawili (makerubi) waliokuwa wanaangaliana Nyuso zao, na Mbawa zao ziklikuwa zinagusana na kila sanduku lilipokuwa linapita watu walikuwa wanasujudu, Je walikuwa wanazisujudia hizo Sanamu za Makerubi?
Wakatoliki tunapoona Sanamu ya Bikira Maria , tunalikumbuka Sanduku la Agano lililokuwa na Bwana wa Sheria (Yesu)
Napenda kusemaga hivi
KWA WAKATOLIKI BIKIRA MARIA SIO MUNGU, HASAMEI DHAMBI ILA NI BINADAMU WAKIPEKEE KABISA
jiwe la majiwe , Otorong'ong'o , MTAZAMO ,