MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Kama sio uhasi wa Luther uenda haya makanisa ya wapiga dili na ibada za kutoa mapepo yasingekuwep.. Ok, yeye alijitoa kanisa Katoliki, mbona na yeye anapingwa na jamii ya walokole?
Endelea kuabudu sanamu kuombea wafu, kumwachia padre ajinonze mvinyo mwenyewe , kumtumaini Bikira Maria ataenda kukuombea na midhambi yako, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe endelea kuabudu rozari nimezunguka ndani ya Biblia sijaona bado leta mistari labda sikuiona
 
Tunataka maandiko ndani ya Biblia Takatifu yaliyoandikwa mtu ukifanya dhambi ukatubu lwa binaadamu mwenzi pengine na yeye ana mizigo kukuzidi eti Maria Mtakatifu utuombee kasema nani? Utavuna ulichopanda leta maandiko acha kupotosha
Limesema Kanisa Katoliki na Ndo lenye mamlka hayo na Ndo maana Biblia Ilitoka Huko... Kwani Yesu aliagiza Mjenge Makanisa? Ni wapi pameandikwa Mjenge kanisa.. yeye si Alikuwa anaabudu Yerusalem
 
Kanisa Katolik limekuwepo hata kabla ya uislam. Hivyo maktaba ya Vatican imeshiba
Nikuambie kitu ndani ya Biblia imeandikwa wa mwisho atakuwa wa kwanza na as kwanza atakuwa wa mwisho na kwa kukusaidia kanisa ama hekalu ni mwili wako unapo fanya maovu unaliaharibu hekalu la Mungu na kwa kukusaidia hayo mahekalu na makanisa hata ukeshe ukisali asubuhi , mchana na usiku kama huna Imani na hutendi yale yanayo mpendeza Mungu ni kazi bure soma Biblia Takatifu sio ile ya Biblia yenu utajua mambo makuu na magumu isiyoyajua.
 
Mtoa post nimpotoshaji mkubwa ningekuona ningekuhukumu kwa Sheria ya Mussa kukufungia jiwe jiwe la kilo 70 shingoni nakukutumbukiza baharini.

Sasa nakujibu Mnamo mwaka 333 kabla ya kuzaliwa Yesu nchi ya Palestina (Israeli) ilitawaliwa ns Wagiriki.Iliopopita miaka 70 yaani mwaka 403 Ndipo ilitolewa tafsiri ya kwanza ya torati na vitabu vya manabii katika lugha ya Kiyunani(Kigiriki).

Tafsiri hiyo iliitwa SEPTUAGINT,viliingizwa vitabu 11 ambavyo havikuwa katika orodha rasmi ya maandiko matakatifu ya Wayaudi wa Parestina.Vitabu hivyo vya nyongeza vilikuwa vimetafsiriwa kuanzia mwaka wa 363 ikiwa nimiaka 30 wa utawala wa Kagiriki na vilitokea Iskanderia (Alexanderia) ambavyo vilikuwa vikitumiwa na watu waliojiita Wayahudi.Kuingizwa vitabu hivyo kwenye SEPTUAGINT kulifanya Wayahudi waitishe mkutano mkuu wa wazee 70 wa Palestina.

Kikao kile kilijadili suala la maandiko ya Iskanderia yasiyokuwa matakatifu kuingizwa kwenye SEPTUAGINT ya Palestina.

Kikao hicho kijulikanacho kwa jina la Canon na ndicho kilichoviondoa vitabu 11 vya Iskanderia nakuvithibitisha kuwa ni batili.

Swari apo Martine Ruther alikua ameishazaliwa?
Kwamujibu wa maelezo ya Padre J.Bouguet des Chaux mwandishi wa kitabu cha JIFUNZE BIBLIA TAKATIFU,mnano karne ya 5 baada ya Yesu Kristo yahani karibu miaka 700 ya mkutano mkuu Canon,Papa Augustno aliamua aliamua kuongeza vitabu 6 kati ya vile 11 vya Iskanderia vilivyoondolewa na wazee 70 katika agano la kale.

Miaka 1,000 baadaye (1546) uamuzi wa Papa Augustino ulipata kibali rasmi kwenye mkutano mkuu wa Maaskofu wa kanisa Katoliki mjini trent-Uingereza bila kuwashirikisha wale wazee sabini wa Kipalestina.Lakini wale wazee hawakukata tamaa kufuatia matengenezo ya kanisa (Reformation) Vitabu hiyvo viliondolewa tena na ndipo palipotokea mpasuko wa Kiprotestanti ambao hadi leo wanaitambua orodha rasmi ya vitabu vya Wayahudi wa Palestina tu nakuvichukulia vile 6 viloongeza na Papa Austino kuwa ni batili.

Kwakumbukumbu sahii kati ya mwaka 93 hadi 130 baada ya Yesu viliandikwa vitabu vingine vingi ambavyo navyo vilionekana batili .kimojawapo kilifahamika kwa jina la Protevangelium, nyaraka za Clement,Iginatius,na Polycarp ambavyo vyote havikuruhusiwa kuingizwa ata kama maandiko kadhaa yalifanana na nyaraka sahii za Biblia lakini havikuwa maandiko matakatifu kwamaana tuipotayo 2Petro1:20-21.

Kwahiyo Martine Ruther alisimamia alichokikuta siokweli kwamba alifukuzwa kwasababu ya kuondoa maandiko matakatifu.Wakatoliki kwa hofu yakupinduliwa waliongeza vitabu hivyo vya sheria zao ambavyo mpaka leo Makasisi Mapadre,Maaskofu Makardinal na Papa wanajua hili na ndonapaswa kuulizia kwanini wanaendelea kushikilia vitabu batili wakijua kuwa sio sahii?

Mwisho:Tafuta kitabu kiitwacho Je nabii issa ndiye YESU KRISTO? na kingine kiitwacho Jifunze Biblia Takatifu
Usome kwa faida ya ubongo wako.
 
Kanisa katoliki wanamuhitaji Mungu kwakwl na ndo mana wengi wanaoelewa neno huwa wanakimbia,Japo sijawahi kuwa mkatoliki lakini naskia ukifa siku ya kuzikwa padri akikuombea rehema basi unasamehewa makosa yako! Na pia mama maria ndo anawaombea wakatoliki,pia ndo dhehebu pekee ambalo pombe imehalalishwa!! Mungu atusaidie sana
Hata malaika huwa wanashangaa kwa kweli padre anapiga windok
 
Limesema Kanisa Katoliki na Ndo lenye mamlka hayo na Ndo maana Biblia Ilitoka Huko... Kwani Yesu aliagiza Mjenge Makanisa? Ni wapi pameandikwa Mjenge kanisa.. yeye si Alikuwa anaabudu Yerusalem
Embu niambie mstari ndani ya biblia ulioandikwa hivyo Hata meno katoliki tusiongeze neno wala kupunguza leta mstari.
 
Hata malaika huwa wanashangaa kwa kweli padre anapiga windok
Ni kwl mkuu nina mjomba wangu ni padri nilienda kumtembelea pale ofcn kwao kurasini nkakuta friji yake imejaa mivinyo plus bia za kutosha akawa anapga bia kama kawaida kwhyo kwa mujibu wa biblia yao pombe kwao ni halali kbsa sikushangaa hata maparoko huwa wananyonya sana mivinyo
 
Biblia ilikuwa compiled na Kanisa Katoliki(biblua ni kitabu cha kikatoliki)

Kulikuwa na Kanisa moja tuu, yaani Kanisa Katoliki.....Orthodox Church walijitenga na Kanisa Katoliki mwaka 1100..,,

Miaka ya 1500 huko, schism ilitokea na Luther alitengwa na Kanisa Katoliki...Hapo ndipo dhambi ya uasi ilianza kuenea kwa kasi na tukaanza kupata madhehebu kedekede

Maamuzi gani...?
Unajua maana ya neno Catholic?...

Kama ulikua hujui anglikana nao wanaitwa Anglican Catholic, Orthodox Catholic, na ndiyo maana hakuna dhehebu linaloitwa Catholic ila lipo Roman Catholic.. nenda kasome maana ya Catholic
 
Mbassa jr,
Umepotea sana.Bikira maria sio binadamu wa kumchukulia kirahisi namna hiyo. Umejitahidi sana kutoa maelezo marefu lakini ya kukariri. Jifunze kusoma biblia taratibu bila mihemko. Tumbo la Bikira maria lilimbeba Mwana wa Mungu ambaye ni Mungu.

Soma vizuri kitabu cha ufunuo,utagundua siri kubwa kuhusu Bikira Maria. Kwa Biblia hii tuliyonayo,ambayo maandishi yake yalikusanywa na kuwekwa pamoja na Kanisa katoliki, Huwezi kukwepa umuhimu wa Bikira maria.Labda uamue kupunguza vitabu kama alivyofanya Padre Martin Luther.
 
Kwani wewe huwezi kumuombea mtu?
Katika sala ya bikira maria kuomba atuombee, mengi ni maneno yaliyotamkwa na Elizabeth wakati ana ujauzito wa miezi sita wa kumzaa Yohane mbatizaji. Nafikiri Bikira Maria kwa 'utakatifu alionao' (according to my faith&believe) sio kosa kuomba atuombee kama tunavyofanya kwa watakatifu wengine.
tunapopishana na nyie ni hapo kwenye 'according to my faith' mwenzako nae kasema 'kutokana na mafundisho ya kanisa' leteni andiko kwenye biblia takatifu ambayo ndio msingi wa ukristo..

Kumuomba mtu akuombee sio kosa, lakini napata shaka kama maombi yako yanafika kama unaeomba akuombee nae alikufa na anasubiri siku ya ufufuo kama wewe. kwa nini usiombe moja kwa moja kwa Yesu Kristo ambae tunaamini yu hai tangu enzi na enzi na milele yote..

Any way acha nendelee ku stick kwenye swali langu la msingi,,,, katika biblia ni wapi tumeambiwa maombi yetu yapitie kwa Bikra Maria?
 
Hapa kila mwamba ngoma anavutia kwake ila kaa katika mstari zero Martin Luther alikuwa na hoja tena Roman empire walichemka

Kumbuka Martin Luther alikuwa genius akiwa na umri mdogo alimiliki masters badaye u Dr then Prof

Alifundisha theliogia ya Agano lá kale na Agano Jipya akiwa prof ktk chuo kikuu maarufu Germany

Ukiweka ukatiloki na uprosentant huwezi jua ukweli halisi
 
Bro kisandu kiukweli huna unalolijua kumhusu Martin Luther Jana nilikushauri juu ya mada unazoziandika na Leo nakushauri tena jaribu kutulia na kutafuta rejea kadhaa ya mada unayokusudia kuandika kabla hujaipost hapa jamii forum.

Unaweza kudhani unajua sana jambo Fulani lakini baada ya kulileta hapa jamii forum ndipo unagundua kuwa kumbe uliyokuwa ukiyajua ni machache sana juu ya mada yako uliyoileta

ili kupunguza hoja nyingi zitakazo kukatiza tamaa jaribu kutulia na kufanya rejea ya source kadhaa za mada unayoandika na sio kubutuabutua tu hii itakusaidia kukujengea uelewa mpana wa mambo

NB acha kuandika kwa kuegemea upande Fulani ambao una maslahi nayo au unapenda uonekane kuwa ni upande sahihi zaidi ya mwingine jaribu kuweka mizania kwenye habari yako mfano kusema hoja nyingi alizozitoa Luther zilikuwa hazina mashiko kwa sababu tu wewe ni mroma sio saw a kabisa brother
 
Endelea kuabudu sanamu kuombea wafu, kumwachia padre ajinonze mvinyo mwenyewe , kumtumaini Bikira Maria ataenda kukuombea na midhambi yako, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe endelea kuabudu rozari nimezunguka ndani ya Biblia sijaona bado leta mistari labda sikuiona

Unaongelea Biblia hii ambayo vitabu vyake vilikusanywa na kuchaguliwa na Kanisa Katoliki?.
Yaani Swala amfundishe samaki kuogelea?.Haya ni maajabu ya karne.
Hakuna Kanisa linalofuata Mafundisho ya Mungu yaliyoanishwa katika Biblia kama kanisa Katoliki Takatifu la Mitume.Hakuna.
 
Back
Top Bottom