Watu wanapenda majibu rahisi. Hakuna jibu rahisi.
Binadamu alivyoanza kuwa kama tumjuavyo leo, nafikiri hakuwa tofauti sana na wanyama wengine, as far as sex is concerned.
Lakini kwakuwa Binadamu ame develop intelligence, akaweza kutangatanga, kubuni vitu, kugundua na kuelezea vitu, ilifika point akawa anaelewa kitendo hichi cha Ajabu, chenye uwezo wa kuleta uhai na kuburudisha.
Muda ulienda, population Zinakua na kutengana ... .lazima kuwe na system ya kucontrol watu.....taboos zikatokea.... Traditions zikatokea.... Dini zikatokea...
mtoto anazaliwa anakua, kakuta watu wanaishi wawili wawili , na yeye akatafutiwa mke/mume anaendeleza....
Baadae ikaonekana wanawake wengi kuliko wanaume, ikabidi mvulana apewe msichana zaidi ya mmoja.
Zingine sheria za asili lakini inawezekana walifanya tu. mf.huwezi Kazaa na mzazi wako... Lakini incest ilikuwepo sana tu. Hadi badae walipogundua si salama. Basi ngono na Dada yako ni Kosa.
Baadae kwakuwa ni kiumbe kilichodevelop Ubongo hivyo Ana complex emotions.... akajigundua ni kiumbe mwenye wivu..... Labda ilitokea wavulana wanagombania wasichana sana......concept ya kila mtu na mmoja ikadevelop.
kuleta order kwenye society itabidi tu kucontrol watu. population kama wa Israeli waliobuni miji, system za uongozi, wakabuni maandishi/records. Ngono inaplay part kubwa sana hasa kwakuwa uliofanywa zaidi kwa ajili ya kuzaa. Ikawekwa sheria ili tujue Nani Kazaa na Nani, wapi, wanafanya shughuli gani.
Muda umeenda ndo imekuwa sheria sasa.
Lakini binadamu wa leo na Hali ya leo si kama miaka 6,000 iliyopita.
Leo kuna uzazi wa mpango.
Leo tuna uelewa mkubwa na matibabu ya magonjwa ya zinaa.
Leo mwanamke anaweza kuzaa akatunza mtoto peke yake sio. Hajafungwa kiuchumi.
Leo tunajua hata mwanamke hufurahia ngono.
Leo tuna uhuru wa kumchagua tumtakaye.
Leo watu wana Question tamaduni. Hawazifwati kama vipofu.
Leo hawana uoga wa tamaduni. Wakiamua haina maana hawafuati.
Nakubaliana na
farajamilele. Dhambi ni makubaliano ya jamii. Tunaelekea tulikotoka