Kwanini ngono ni dhambi?

Kwanini ngono ni dhambi?

Kwa utashi tulionao binadam tunajua lipi baya na lipi jema hauhitaji vitabu vya dini viandike ndo utambue. Tusidanganyane eti kumuangalia tu mtu ukamtamani inakua ni dhambi ni dhambi kwa misingi ipi? Huku ndo kukaririshwa...hivi nani anaweza kumaliza siku/wiki hajamtamani mtu?! Sasa kama kweli hii ni dhambi na kama kweli kuna moto wa milele mtachomwa wote...uholanzi(amsterdam) bangi ni halali China ukikamatwa unanyongwa ukipima hapa utagundua kuna mitizamo miwili tofauti juu ya uvutaji bange...hiyo haitoshi ni dhambi kwa muislam kunywa pombe ila kanisani imebarikiwa inaitwa divai...yote 9-10 amemaliza "Housegirl na Faraja milele" dhambi ni makubaliano ya jamii fulani period
 
Ngono ni Dhambi kubwa sana. Sawasawa na kupiga KURA na watoto tuwafundishe hivyo.
 
Kwa utashi tulionao binadam tunajua lipi baya na lipi jema hauhitaji vitabu vya dini viandike ndo utambue. Tusidanganyane eti kumuangalia tu mtu ukamtamani inakua ni dhambi ni dhambi kwa misingi ipi? Huku ndo kukaririshwa...hivi nani anaweza kumaliza siku/wiki hajamtamani mtu?! Sasa kama kweli hii ni dhambi na kama kweli kuna moto wa milele mtachomwa wote...uholanzi(amsterdam) bangi ni halali China ukikamatwa unanyongwa ukipima hapa utagundua kuna mitizamo miwili tofauti juu ya uvutaji bange...hiyo haitoshi ni dhambi kwa muislam kunywa pombe ila kanisani imebarikiwa inaitwa divai...yote 9-10 amemaliza "Housegirl na Faraja milele" dhambi ni makubaliano ya jamii fulani period

Mkuu samahani

Hivi kuna tofauti gani kati ya ngono ya ndoa na ngono ya watu ambao hawajaoana.

Je, ndoa ilianzaje? Alianzisha nani?

Kwanini wanyama mfano mbuzi wanapandana tu bila kujali sheria kama za binadamu?

Naomba unijibu coz nafahamu mkabala wako ndio maana nimekuuliza.
 
*Sex is designed to happen between married people. It is an emotional and spiritual glue designed by God to bind wife and husband together for life. Making love celebrates the intimacy and commitment of marriage.

*Sex is about "becoming one" in body, but also one in soul. Sex is more than skin on skin, it's heart joining another heart. When you sleep with someone, you give part of yourself to them and take part of them into you.

*Sex is meant to be free - shame. If it needs people to keep secrets, then it's less than God's best. Sex should bring joy and peace, not fear, shame, loneliness and regrets

Ndiyo maana linaitwa "tendo la ndoa, na sio tendo la urafiki wala uchumba. Kama ngono haiwafanyi watu wawili kuwa mwili mmoja, na tena kama ngono inaondoa utakatifu wa miili yenu basi hiyo ni dhambi. "Miili yenu ni hekalu takatifu la kumpendeza Mungu".

I wakorintho 7:2, 8-9.
"Lakini kwa sababu ya zinaa, Kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe, na Kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.

8. Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane. Ni heri wakae kama mimi nilivyo.
9. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia na waoe: maana ni afadhali kuoa
Kuliko kuwaka tamaa

1 wakorintho 6:18.. Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake, Ila yeye afanyaye zinaa, hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

Waebrania 13:4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu". Kwa hiyo tukizini au kufanya uasherati tutaadhibiwa vizuri tu

Mithali 6:32 " Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa. Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.". Kwa hiyo ngono inapanda maangamizi na uharibifu kwenu. Mifano tunayo kabisa, Sodoma na Gomora ilivyoangamia kwa sababu ya uzinzi. Nuhu na gharika, kuhani Eli na watoto wake Hofni na Finehasi wote walifariki. Wana wa Israel kupigwa na adui zao Wafilisti hadi sanduku la Agano la Mungu kutekwa; yote ni sababu ya uzinzi.

Na pia zinaa huondoa ufahamu (Hosea 4:11) "uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za binadamu"

Na maandiko yanasema "basi mpingeni shetani naye Atawakimbia". Yakobo 4:7
Lakini maandiko hayasemi ipingeni zinaa; bali yanasema "Ikimbieni zinaa". Kama ambavyo Yusufu alikimbia akaacha nguo zake ili asizini na mke wa bwana wake.

2. Kwa nini ngono isiwe dhambi kwa wanyama ila kwa binadamu. Mungu ametupa "conscious" binadamu tofauti na viumbe vingine. Tuna uwezo wa kutambua mema na mabaya. Ndo maana hata kwenye uzinzi mbona hufanyi na dada/kaka zako unaenda kutafuta watu ambao si ndugu zako?

3. Kwa nini kumtamani mwanamke ni sawa na kuwa umeshazini naye. Kutamani mwanamke asiye mkeo ni kuuwashia tamaa mwili wako. Unakaribisha uzinzi. "Roho I radhi lakini mwili ni dhaifu". Roho inataka tu iishie kwenye kutamani lakini mwili utakupelekea kwenye uzinzi

Zaburi 119: 37 " Uyageuze macho yangu, nisitazame visivyofaa".

Eva aliishia kutenda dhambi kwa sababu ya macho yake. Yule nyoka mwerevu alimdanganya Eva " mwanamke alipoona ule mti wafaa kwa chakula, WAPENDEZA KWA MACHO, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa...... (mwanzo 2:6)

Mwanzo 6:2 " wana wa Mungu WALIWAONA hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri
; wakajitwalia wake wowote waliojichagulia". Mwisho wake ni gharika ya Nuhu

Kwa hiyo macho yako yana nguvu kubwa sana ya kuchochea tamaa ndani yako. Yazuiye macho yako yasione wala kufurahia yale maovu

Credit: sister Judith, Mwl Mwakasege et al
 
All questions referred to the Holly Qur'an.lakini mim so mjuzi kivile wafwate walobobea watakueleza kwa nini zinaa zambi,nalogaauti afu ntalogini.
 
Last edited by a moderator:
All questions referred to the Holly Qur'an.lakini mim so mjuzi kivile wafwate walobobea watakueleza kwa nini zinaa zambi,nalogaauti afu ntalogini.

Hehehe nimefurahi tu ulivyoaga mapema lol
Sio kwa kujihami huko👆👆
 
Last edited by a moderator:
"Niliyowafunulia ninyi ni ya kwenu ninyi na watoto wenu" asema Bwana Mungu wa Majeshi.
Kuna vitu ukijiuliza huwezi kupata majibu. Jibu lake ni mstari huo, kuwa kuna mengine hukufunuliwa kuyajua.
 
Unamhoji Mungu? Vitu vingine havina logic. Believe and follow.
 
vipi khusu ili ?Tunafundishwa ukimtazama nkeo kwa matamanio ya kumwingilia na akikutazama,kisha mkifanya mapenzi mnakuwa mnasamehewa madhambi yenu(madhambi yanadondoka kupitia vidole).Hivi hili tendo lina siri gani??
 
Ni Mambo ya kibanadamu katika kujifanya wao wako kinyume na nature, kufanya mapenzi{Ngono} ni tendo la lazima katika kuleta uzazi wa viumbe duniani, Mwanaume na Mwanamke wanazalisha mbegu na mayai katika miili yao kwa wakati husika, na ni lazima mbegu na mayai zikisha pevuka ni lazima zitoke kwenda kutengeneza mtoto.eti wanasema kufanya mapenzi ni dhambi kabla ya ndoa, ndoa ni nini hasa, mbona kuna watu wengi wamezaliwa bila ya ndoa na wanaishi kama binadamu wengine, tena utakuta wana mafanikio kuliko watoto wa ndoa, nendeni mkazaane siyo nendeni mkaoane
 
Mkuu samahani

Hivi kuna tofauti gani kati ya ngono ya ndoa na ngono ya watu ambao hawajaoana.

Je, ndoa ilianzaje? Alianzisha nani?

Kwanini wanyama mfano mbuzi wanapandana tu bila kujali sheria kama za binadamu?

Naomba unijibu coz nafahamu mkabala wako ndio maana nimekuuliza.

Bila samahani mkuu

Naomba unijuze haya kisha tuendelee

Kwanza tujue ndoa ni nini? Je ni kuvishana pete? Je ni kukaa na mwenzi wako chini ya paa moja? Na Je sheria za nchi zinasemaje kuhusu ndoa?
 
Bila samahani mkuu

Naomba unijuze haya kisha tuendelee

Kwanza tujue ndoa ni nini? Je ni kuvishana pete? Je ni kukaa na mwenzi wako chini ya paa moja? Na Je sheria za nchi zinasemaje kuhusu ndoa?

Ndoa katika mazingira gani mkuu!
Ya dini?
Kwangu naamin ndoa ni maridhiano baina ya watu wawili (me na ke) walioridhia kuishi pamoja na kushirikiana kwa mambo tofauti kama yakimwili... kwa makubaliano waliyojiwekea.
 
Hapo red hili ni swali gumu sana. Kwanini alikataza hilo swali alipaswa aulizwe mwenyewe. Huku ni kuingilia uhuru wa kimahakama ya Mungu.

Baada ya hapo tutajiuliza kwanini Mungu alikataza watu kulana tigo? Je kulana denda ni halali?? Je kunyonyana vikojoleo (kwa wanandoa) ni halali/haramu? Mungu alikataza wapi???

Huyu Mungu tumwache tu aendelee kuitwa Mungu.

....Kwa hili jibu Mi hoi coz nimecheka sana vile,..kitufe cha like sikioni vile...Hahahahaaaaaa..
 
vipi khusu ili ?Tunafundishwa ukimtazama nkeo kwa matamanio ya kumwingilia na akikutazama,kisha mkifanya mapenzi mnakuwa mnasamehewa madhambi yenu(madhambi yanadondoka kupitia vidole).Hivi hili tendo lina siri gani??

Mhhh mkuu hilo darasa mlifundishwa wapi? Hizo dhambi zinadondokaje kwenye vidole?
Cc aretasludovick ulipata kusikia hii? Bennie 369 hebu pita hapa uje ushushe nondo
 
Last edited by a moderator:
Ndoa katika mazingira gani mkuu!
Ya dini?
Kwangu naamin ndoa ni maridhiano baina ya watu wawili (me na ke) walioridhia kuishi pamoja na kushirikiana kwa mambo tofauti kama yakimwili... kwa makubaliano waliyojiwekea.

Mkuu nimekuelewa sana naona tuna share idea moja mimi pia naamini vivyo hivyo...

Ndoa ni matokeo ya kustaarabika kwa wanadamu(civilisation) kuvaa pete, kwenda bomani, kushirikisha mambo ya ki imani na kadhalika zote hizi ni mbwembwe zilizo ongezeka kutokana na mahitaji ya wakati husika
 
Ndoa ilianzaje? Aliianzisha nani? Mbona jamii karibia zote duniani zina huu utaratibu? Je waliigana kwenye suala la ndoa au walijikuta wanapractice ndoa kila mmoja kwa wakati wake?
 
Back
Top Bottom