Wazo la kuhamisha makao makuu lilianza wakati wa ukoloni wa Wajerumani hasa wakati wa vita ya kwanza ya dunia walipohamishia makao Tabora kwa muda mnamo mwaka 1916. Mwaka 1959 Kupitia LEGCO Waingereza walipendekeza makao yahamie Dodoma lakini hatua hazikuchukuliwa tokana na gharama kuwa kubwa. Mwaka 1966 Joseph Nyerere mdogo wake Mwalimu alipeleka muswada bungeni kuhusu serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, lakini pia haikufanikiwa kupitishwa. Mwaka 1972 kamati kuu ya TANU ilifikia maamuzi ya kuhamishia makao makuu ya TANU Dodoma kwa sababu kuu tatu.
Mosi, Kwa kuwa Dodoma ni katikati na inaweza kufikiwa kirahisi tokea pande zote za Tanzania.
Pili, kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo na kuwa kwa kuhamishia makao ya chama kungechangamsha uchumi, na
Tatu. Ni kwa ajili ya Usalama kwa kuwa bara kulionekana kuwa salama kuliko ukanda wa pwani.
Mwaka huohuo serikali pia ilichagua kampuni tatu za kimataifa ili kupendekeza sehemu na master plan ya mji mkuu wa nchi. Uamuzi wa kuhamisha mji mkuu ulifikiwa katika mkutano mkuu maalum wa TANU Oktoba 1973. Na baadae Mwalimu alitangaza kupitia redio kuwa serikali na chama vitahamia Dodoma katika kipindi cha miaka 10.
Serikali ilichukua hatua kadhaa. Kwanza ni kwa kuunda Wizara ya Maendeleo ya mji mkuu Chini ya Ofisi ya Rais na pia kuunda Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) .Waziri wa kwanza akiwa Chifu Adam Sapi Mkwawa na Mkurugenzi mkuu wa CDA wa kwanza akiwa Sir George.
Majukumu ya kwanza ya Mamlaka ilikuwa ni:
Mosi, Kutafuta wana Mipango miji (Master planners) ambapo waliitisha tenda ma kampuni toka Canada Project Planning Associates ilichaguliwa
Pili, Ku recruit wafanyakazi wa mamlaka ampapo Sir George alianzisha kurugenzi tisa na kila kurugenzi ikiwa na Mkurugenzi na timu yake.
Kazi nyingine ilikuwa ni kuainisha eneo ambapo mji mkuu utajengwa na waliainisha maeneo sita tofauti na hatimaye wakachagua eneo moja karibu na mji wa zamani.
Kazi ya kutengeneza Master plan ilichukua miaka miwili na jopo la majaji likiongozwa na mtaalam Sir John Overal aliyekuwa Mkurugenzi wa Australian National Capital Development Commission walipitisha master plan mnamo Februali 1975. Master plan ilikuwa imegawanywa katika maeneo 4 yakiwemo Eneo la mjini (Downtown) ambapo pangekuwa na ofisi za serikali, bunge, mahakama na maeneo ya biashara,
Eneo la makazi ambapo makazi yalipangwa kwa mujibu wa mtindo wa TANU wa nyumba kumi. Eneo la tatu ilikiwa Maeneo ya wazi na bustani za kupumzikia na Eneo jingine ilikuwa miundombinu ya usafirishaji.
Mwalimu alipendezwa sana na mpango huo uliokuwa ukiakisi siasa ya ujamaa.
Ilikuwa imekadiriwa kuwa ujenzi utachukua miaka 10 kuanzia mwaka 1976 hadi 1986 na ungegharimu shilingi bilioni 3.6 au dola za Marekani milioni 53.
CDA Pia ilikuwa na jukumu la kuweka miundombinu kama maji, barabara,
Pamoja na malengo mazuri hali ya uchumi baada ya hapo haikuwa nzuri kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta, Vita vya Kagera nk. CDA ikaambulia kupata 10% tu ya makadirio ya gharama hata hivyo walifanikiwa kujenga baadhi ya maiundombinu ikiweko barabara; mfumo wa maji machafu na salama. Pia walijenga ikulu ya Chamwino na baadhi ya ofisi za serikali.
Sent using
Jamii Forums mobile app