Kwanini Mwl. Nyerere alishindwa kuhamia Dodoma?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Wazo la kuhamahamishia serikali Dodoma lilikuwa la Mwl. Nyerere wakati ya awamu ya kwanza. Lakini hata baada ya kuliongoza taifa kwa muda mrefu alishindwa kuitekeleza mdoto yake ya kuhamia Dodoma.

Ndoto ya kuhamia Dodoma pia haikutimia kwenye awamu zingine 3 (miaka 30) zilizofuata na ikatekelezwa awamu hii ya tano?

Swali ni ni nini kilisababisha mwalimu asiweze kuitekeleza Ndoto yake mwenyewe ya kuhamia Dodoma?

Hebu tukumbushane hapo.
 
Priorities alitaka mikakati ifanyike kwa step bila kukurupuka maana kunamambo mengi ya muhimu kuliko kuhamia dodoma.
mfano mpaka enzi ya Mkapa Rais alikuwa akienda nje kuomba chakula kisingizio ukame sasa unaanzaje kuhamia Dom.
Sasahivi hata chanjo za watoto ni zashida,ajira hamna,elimu/shule siobora,kilimo hasa cha biashara kimefail lkn mtu mmoja ana force ili aweke historia
 
Alipima vipaumbele vya muhimu zaidi kuliko kuhamia Dodoma. Ishu ya Dodoma ni sawa Na MTU mwenye nyumba moja yenye kila kitu anaamua kujenga nyumba nyingine the same ya kuishi hali angeweza kuwekeza kwenye vipaumbele vingine.
Asili ya wazo la Dodoma nyerere alilicopy toka Kwa wakoloni ambao wao key point waliona kiutawala ni center sababu ya dunia ya zamani ambayo ilikuwa imejifunga.
Kwa ulimwengu wa sasa uliofunguka ni matumizi mabaya ya kodi zetu kuhamia Dodoma badala ya fedha zile kuwekezwa kwenye kutatua tatizo kuu LA ajira ambalo ni Bomu kubwa kwa awamu hii ya kuzalisha umasikini nchini ijiandae nalo sababu yenyewe ndio imelitengeneza kimakusudi ya kuwataka watu Waishi kishetani.
 
Wazo la kuhamahamishia serikali Dodoma lilikuwa la Mwl. Nyerere wakati ya awamu ya kwanza. Lakini hata baada ya kuliongoza taifa kwa muda mrefu alishindwa kuitekeleza mdoto yake ya kuhamia Dodoma.

Ndoto ya kuhamia Dodoma pia haikutimia kwenye awamu zingine 3 (miaka 30) zilizofuata na ikatekelezwa awamu hii ya tano?

Swali ni ni nini kilisababisha mwalimu asiweze kuitekeleza Ndoto yake mwenyewe ya kuhamia Dodoma?

Hebu tukumbushane hapo.
Kwani awamu hii ya tano imeshahamia Dodoma?
 
Mwl. JK Nyerere alikuwa na akili nyingi sana.. Alibaini kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia hakukuwepo na haja tena ya kuhamia Dodoma bali kuwajengea uwezo wananchi ili waweze kupambana na umaskini, maradhi na ujinga!

Kwa akili ya kawaida tu... Ukihamia Dodoma ni lazima uendelee kuilinda zaidi Dar (gharama maradufu).

Jiulize, unahamia Dodoma ghafla ghafla bila kuwekeza kuboresha miundombinu yake ya barabara, maji safi, maji taka, n.k.... Je, umefanya tafiti ukajua itachukua muda gani kufikia mkwamo kama ule uliopo Dar??

Unaweka nguvu nyingi kuhamia Dodoma unaokoa nini? Au unaleta utofauti gani? Au bado unatafuta katikati ya nchi ndo uweke makao makuu??

Hiki ni kipindi ambacho badala ya kuzilundika idara, taasisi na wizara za serikali sehemu moja (centralization) ilitakiwa zitawanywe kwenye kila jiji hapa nchini kwa uwezo, nguvu na juhudi zile zile... Mfano Wizara ya Ardhi ijengwe Dodoma, Madini Mwanza, Utalii Arusha, Usafirishaji, Bandari Dar, Gesi Mtwara, n.k... Yaani kila jiji na kila Kanda ipate uwekezaji wa maana wa makao makuu ya ofisi, idara na taasisi za serikali...
Hatua hii ingechochea maendeleo ya miundombinu na mzunguko wa fedha kwenye shughuli mbalimbali za uchumi mikoani...!! Ikumbukwe kuwa kwenye nchi kama hii serikali ndo mwajiri kiongozi na mwenye job security nzuri... Badala ya kusambaza rasilimali watu na rasilimali fedha mikoani... Tunazitoa Dar na kwenda kuzilundika tena Dodoma...

Huu utawala wa sasa umeshindwa kabisa hayo mapambano. Badala yake wamekuja na vita wanavyoviweza vya maendeleo ya vitu... Yes, mtajenga sana vitu lakini ni vyema mkafahamu kuwa grafu ya ujinga, umaskini na maradhi inazidi kupanda juu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom