Kwanini Mwl. Nyerere alishindwa kuhamia Dodoma?

Alipima vipaumbele vya muhimu zaidi kuliko kuhamia Dodoma. Ishu ya Dodoma ni sawa Na MTU mwenye nyumba moja yenye kila kitu anaamua kujenga nyumba nyingine the same ya kuishi hali angeweza kuwekeza kwenye vipaumbele vingine.
Asili ya wazo la Dodoma nyerere alilicopy toka Kwa wakoloni ambao wao key point waliona kiutawala ni center sababu ya dunia ya zamani ambayo ilikuwa imejifunga.
Kwa ulimwengu wa sasa uliofunguka ni matumizi mabaya ya kodi zetu kuhamia Dodoma badala ya fedha zile kuwekezwa kwenye kutatua tatizo kuu LA ajira ambalo ni Bomu kubwa kwa awamu hii ya kuzalisha umasikini nchini ijiandae nalo sababu yenyewe ndio imelitengeneza kimakusudi ya kuwataka watu Waishi kishetani.
Kama ukibahatika kwenda Dodoma leo na kuwaona na kuwasikiliza
Hata aliehamia dodoma bado yupo dar, nani atahama dar akakae porini.
Ukiwaona na kuwasikiliza wafanyakazi waliohamia Dodoma unaweza kutoa machozi bila idadi.
 
Mkuu Dodoma kama capital ni gharama,ilishindikana enzi za Raisi Mwl.Nyerere tena baada ya yeye aliekuwa driving machine kuhamia Dodoma kuacha ghafla,sababu hazikuwekwa wazi mara tu baada ya kujengewa Ikulu hapo Chamwino na kukabidhiwa funguo!!!.

Japo tulikuwa na mfumo wa chama kimmoja, baraza la mawazi na bunge lilipinga kwa nguvu mmoja kuhamisha makao makuu,lakini Mwl.Nyerere alitishia kulivunja bunge ndipo walisalimu amri kuhamia Dodoma.
Utaratibu wake ulikuwa hivi
1.Iliundwa wizara ya ustawishaji wa makao makuu likiongozwa na Chief Adam Sapi Mkwawa.
2.Likaundwa Capital Development Authority CDA ikiongozwa na Sir George Kahama kama CEO
3.Wakahamisha ofisi ya makamu wa pili wa Raisi na waziri mkuu Mzee Rashidi Mfaume Kawawa akahamia Dodoma rasmi Jan 1975
4.Ikajengwa Ikulu Dodoma Chamwino ili Raisi akishahamia hapo ndipo wizara nyingine nazo zianze kuhamishiwa Dodoma.

Lakini cha ajabu mwaka 1975 Mwl.Nyerere alikaa siku kidogo pale hakuhamisha ofisi yake,nakumbuka picha ya gazeti la Daily News front page alionekana Mwl.Nyerere hakuwa na furaha,alikuwa na mawazo mengi.

Kilichofuata sote tunakijua alirudi Magogoni na Msasani akipunga upepo wa bahari ya Indi hadi pale alipostaafu 1985.
Mimi niliwahi kusema humu kama Magu yupo committed kuhamia Dodoma basi achukue miezi 6 bila kugusa Dar-es-salaam lakini hakustahimili so sad.
 
Inaweza kuwa kweli,ila mambo mengi yaliingiliana na kusababisha nchi kuyumba kiuchumi. Mojawapo ni vita vya kagera na fitina za mabeberu.
 
Wazo la kuhamahamishia serikali Dodoma lilikuwa la Mwl. Nyerere wakati ya awamu ya kwanza. Lakini hata baada ya kuliongoza taifa kwa muda mrefu alishindwa kuitekeleza mdoto yake ya kuhamia Dodoma.

Ndoto ya kuhamia Dodoma pia haikutimia kwenye awamu zingine 3 (miaka 30) zilizofuata na ikatekelezwa awamu hii ya tano?

Swali ni ni nini kilisababisha mwalimu asiweze kuitekeleza Ndoto yake mwenyewe ya kuhamia Dodoma?

Hebu tukumbushane hapo.
Nani kaweza kuhamia Dodoma ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wa awamu ya 5 walienda kupiga show tu lakini wamerudi wote Dar na wamehamishia hadi wanyama wa mikoani ikulu. Wataondoka kweli????
Wazo la kuhamahamishia serikali Dodoma lilikuwa la Mwl. Nyerere wakati ya awamu ya kwanza. Lakini hata baada ya kuliongoza taifa kwa muda mrefu alishindwa kuitekeleza mdoto yake ya kuhamia Dodoma.

Ndoto ya kuhamia Dodoma pia haikutimia kwenye awamu zingine 3 (miaka 30) zilizofuata na ikatekelezwa awamu hii ya tano?

Swali ni ni nini kilisababisha mwalimu asiweze kuitekeleza Ndoto yake mwenyewe ya kuhamia Dodoma?

Hebu tukumbushane hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhamia Dodoma karne hii ya 21 ni upungufu mmkubwa wa kufikiri. Ile ilikua idea ya Nyerere na aliitoa lwa wakoloni ya kuongoza kutokea makutano makuu(center) ili kuwarahisishia watu waoatoka Bukoba, Musoma, Mbeya, Songea kufika kwenye ofisi za serikali kwa urahisi maana enzi hizo ilikua nyaraka lazima uzipeleke kwa mkono.

Leo hii mtu hana haja ya kutoka Bukoba kuja Dar kufuatilia nyaraka au kufuatilia mafao yake, ofisi ziko kila mkoa, nyaraka zinatumwa kwa mtandao. Ndio maana nashangaa hadi sasa wizara zinakaa sehemu moja zote kama kumbikumbi. Enzi za Nyerere ilikua ni lazima iwe hivyo ila leo sio.

Kuhamia Dodoma kwa serikali ilikua ni kukurupuka ila wamejikuta hilo jambo haliwezekani na limeongeza gharama za uendeshaji wa serikali zaidi ya mara 2.

Mabalozi walipewa ardhi na viwanja kule hajaenda hata mmoja, leo hii Marekani akajenge jengo jipya Dodoma kwa sababu ipi?

Mawaziri wote na makatibu wakuu wako hapa town, mzee mkubwa ndio kaogeza wanyama ikulu ale good time Dodoma inabaki kua ni jambo la kisiasa. Atakaekuja anaweza kuipiga chini mazima.
 
Inaweza kuwa kweli,ila mambo mengi yaliingiliana na kusababisha nchi kuyumba kiuchumi. Mojawapo ni vita vya kagera na fitina za mabeberu.
Kuna mambo hayakuwekwa wazi,lakini priority kwa leo ni Afya,nimeangalia China na Korea wanavyopambana na Corona Virus, wana zana nyingi na za uhakika.Sina uhakika kama hata mask inatengenezwa hapa nchini au kama ziko za kutosha.
 
Hilo la mask lipo nje ya uwezo wangu. Muulize waziri wa Afya na viwanda.
 
Bado ajajua vipaumbele vya wananchi ni vipi angeinua Kilimo akajenga vyuo vya maendeleo au ufundi kila kata yaani kugusa wananchi moja Kwa moja chadema ingejifia yenyewe wala asingehangaika nayo
Kujenga Dodoma, chato,sgr,ndege bado ajawagusa wanyonge hapa.
 
Kuhamia Dodoma karne hii ya 21 ni upungufu mmkubwa wa kufikiri. Ile ilikua idea ya Nyerere na aliitoa lwa wakoloni ya kuongoza kutokea makutano makuu(center) ili kuwarahisishia watu waoatoka Bukoba, Musoma, Mbeya, Songea kufika kwenye ofisi za serikali kwa urahisi maana enzi hizo ilikua nyaraka lazima uzipeleke kwa mkono.

Leo hii mtu hana haja ya kutoka Bukoba kuja Dar kufuatilia nyaraka au kufuatilia mafao yake, ofisi ziko kila mkoa, nyaraka zinatumwa kwa mtandao. Ndio maana nashangaa hadi sasa wizara zinakaa sehemu moja zote kama kumbikumbi. Enzi za Nyerere ilikua ni lazima iwe hivyo ila leo sio.

Kuhamia Dodoma kwa serikali ilikua ni kukurupuka ila wamejikuta hilo jambo haliwezekani na limeongeza gharama za uendeshaji wa serikali zaidi ya mara 2.

Mabalozi walipewa ardhi na viwanja kule hajaenda hata mmoja, leo hii Marekani akajenge jengo jipya Dodoma kwa sababu ipi?

Mawaziri wote na makatibu wakuu wako hapa town, mzee mkubwa ndio kaogeza wanyama ikulu ale good time Dodoma inabaki kua ni jambo la kisiasa. Atakaekuja anaweza kuipiga chini mazima.
Angekuwa Na nia ya kuhamia Dodoma angepeleka wanyama Dodoma. Hela iliyopotea Dodoma ingewekwa kwenye Kilimo ingeondoa tatizo LA machinga mijini.
 
Mwl. JK Nyerere alikuwa na akili nyingi sana.. Alibaini kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia hakukuwepo na haja tena ya kuhamia Dodoma bali kuwajengea uwezo wananchi ili waweze kupambana na umaskini, maradhi na ujinga!

Kwa akili ya kawaida tu... Ukihamia Dodoma ni lazima uendelee kuilinda zaidi Dar (gharama maradufu).

Jiulize, unahamia Dodoma ghafla ghafla bila kuwekeza kuboresha miundombinu yake ya barabara, maji safi, maji taka, n.k.... Je, umefanya tafiti ukajua itachukua muda gani kufikia mkwamo kama ule uliopo Dar??

Unaweka nguvu nyingi kuhamia Dodoma unaokoa nini? Au unaleta utofauti gani? Au bado unatafuta katikati ya nchi ndo uweke makao makuu??

Hiki ni kipindi ambacho badala ya kuzilundika idara, taasisi na wizara za serikali sehemu moja (centralization) ilitakiwa zitawanywe kwenye kila jiji hapa nchini kwa uwezo, nguvu na juhudi zile zile wanao... Mfano Wizara ya Ardhi ijengwe Dodoma, Madini Mwanza, Utalii Arusha, Usafirishaji, Bandari Dar, Gesi Mtwara, n.k... Yaani kila jiji na kila Kanda ipate uwekezaji wa maana wa makao makuu ya ofisi, idara na taasisi za serikali...
Hatua hii ingechochea maendeleo ya miundombinu na mzunguko wa fedha kwenye shughuli mbalimbali za uchumi mikoani...!! Ikumbukwe kuwa kwenye nchi kama hii serikali ndo mwajiri kiongozi na mwenye job security nzuri... Badala ya kusambaza rasilimali watu na rasilimali fedha mikoani... Tunazitoa Dar na kwenda kuzilundika tena Dodoma...

Huu utawala wa sasa umeshindwa kabisa hayo mapambano. Badala yake wamekuja na vita wanavyoviweza vya maendeleo ya vitu... Yes, mtajenga sana vitu lakini ni vyema mkafahamu kuwa grafu ya ujinga, umaskini na maradhi inazidi kupanda juu!!
"...Wizara ya Ardhi ijengwe Dodoma, Madini Mwanza, Utalii Arusha, Usafirishaji, Bandari Dar, Gesi Mtwara, n.k... Yaani kila jiji na kila Kanda ipate uwekezaji wa maana wa makao makuu ya ofisi, idara na taasisi za serikali..."

Safi sana, mfumo huu unatumika Suisse, Colombia, Brazil and I think China* (*If not mistaken)

Unaangazia sehemu yenye upeo au jambo fulani unapeleka (Kutupanya) mwisho wa siku utakuta kila Mkoa tayari unahodhi ofisi kuu ya kitaifa!.

Anaehitaji biashara anasogea Dar. Anaehitaji pembejeo anasogea Mbeya. Anayehitaji Leseni ya uchimbaji anasogea Geita, Mwanza, Shinyanga (Mkoa unaongoza kwa kuwa na hayo madini).... Hivyo mwisho wa siku una kuta kila mkoa tayari una administrative office ya kitaifa hata Kigoma au Morogoro unakuta Wizara ya Michezo HQs.
 
Walipa kodi tungekuwa tunashirikishwa kwenye mipango ya maendeleo ya nchi yetu tungeokoa Pesa nyingi Sana kuwekezwa pasipo tija Leo Kilimo kwanza imetupwa,uchumi wa gas imetupwa hapa ni kodi zetu tu ndio zinateketezwa lait kila ajae angekuwa anatekeleza vipaumbele vya wananchi Na sio vyake tungekuwa mbali sana.Check jengo LA machinga complex limedoda sababu hawakushirikisha machinga
Yaani vipaumbele vyao sio vipaumbele vya wananchi wanaangalia viwapavyo sifa awajali kuhusu riba
.Wananchi ushirikishwa kwenye kulipa madeni tu.
 
"...Wizara ya Ardhi ijengwe Dodoma, Madini Mwanza, Utalii Arusha, Usafirishaji, Bandari Dar, Gesi Mtwara, n.k... Yaani kila jiji na kila Kanda ipate uwekezaji wa maana wa makao makuu ya ofisi, idara na taasisi za serikali..."

Safi sana, mfumo huu unatumika Suisse, Colombia, Brazil and I think China* (*If not mistaken)

Unaangazia sehemu yenye upeo au jambo fulani unapeleka (Kutupanya) mwisho wa siku utakuta kila Mkoa tayari unahodhi ofisi kuu ya kitaifa!.

Anaehitaji biashara anasogea Dar. Anaehitaji pembejeo anasogea Mbeya. Anayehitaji Leseni ya uchimbaji anasogea Geita, Mwanza, Shinyanga (Mkoa unaongoza kwa kuwa na hayo madini).... Hivyo mwisho wa siku una kuta kila mkoa tayari una administrative office ya kitaifa hata Kigoma au Morogoro unakuta Wizara ya Michezo HQs.
Bado haijakaa sawa kumbuka kila mkoa unavitu sawa Madaraka mikoani ndio solution yaani ukitakacho unakipata wilayani
 
Mwl. JK Nyerere alikuwa na akili nyingi sana.. Alibaini kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia hakukuwepo na haja tena ya kuhamia Dodoma bali kuwajengea uwezo wananchi ili waweze kupambana na umaskini, maradhi na ujinga!

Kwa akili ya kawaida tu... Ukihamia Dodoma ni lazima uendelee kuilinda zaidi Dar (gharama maradufu).

Jiulize, unahamia Dodoma ghafla ghafla bila kuwekeza kuboresha miundombinu yake ya barabara, maji safi, maji taka, n.k.... Je, umefanya tafiti ukajua itachukua muda gani kufikia mkwamo kama ule uliopo Dar??

Unaweka nguvu nyingi kuhamia Dodoma unaokoa nini? Au unaleta utofauti gani? Au bado unatafuta katikati ya nchi ndo uweke makao makuu??

Hiki ni kipindi ambacho badala ya kuzilundika idara, taasisi na wizara za serikali sehemu moja (centralization) ilitakiwa zitawanywe kwenye kila jiji hapa nchini kwa uwezo, nguvu na juhudi zile zile wanao... Mfano Wizara ya Ardhi ijengwe Dodoma, Madini Mwanza, Utalii Arusha, Usafirishaji, Bandari Dar, Gesi Mtwara, n.k... Yaani kila jiji na kila Kanda ipate uwekezaji wa maana wa makao makuu ya ofisi, idara na taasisi za serikali...
Hatua hii ingechochea maendeleo ya miundombinu na mzunguko wa fedha kwenye shughuli mbalimbali za uchumi mikoani...!! Ikumbukwe kuwa kwenye nchi kama hii serikali ndo mwajiri kiongozi na mwenye job security nzuri... Badala ya kusambaza rasilimali watu na rasilimali fedha mikoani... Tunazitoa Dar na kwenda kuzilundika tena Dodoma...

Huu utawala wa sasa umeshindwa kabisa hayo mapambano. Badala yake wamekuja na vita wanavyoviweza vya maendeleo ya vitu... Yes, mtajenga sana vitu lakini ni vyema mkafahamu kuwa grafu ya ujinga, umaskini na maradhi inazidi kupanda juu!!

Paragraph ya tano....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom