Wazo la kuhamahamishia serikali Dodoma lilikuwa la Mwl. Nyerere wakati ya awamu ya kwanza. Lakini hata baada ya kuliongoza taifa kwa muda mrefu alishindwa kuitekeleza mdoto yake ya kuhamia Dodoma.
Ndoto ya kuhamia Dodoma pia haikutimia kwenye awamu zingine 3 (miaka 30) zilizofuata na ikatekelezwa awamu hii ya tano?
Swali ni ni nini kilisababisha mwalimu asiweze kuitekeleza Ndoto yake mwenyewe ya kuhamia Dodoma?
Hebu tukumbushane hapo.
Ni kweli Mwalimu Nyerere alikuwa wa kwanza kuhamasisha Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma.
Nilikuwa mtu mzima wakati ule na nilikuwa Chuo na nilikuwa kada mtiifu wa TANU.
Sababu alizozitoa zilikuwa nzito ambazo kwa kweli hakuna mwenye akili timamu kwa wakati ule angezipinga.
Baadhi ya sababu zilikuwa
1. Dodoma ni katikati ya nchi yetu. Kuhamia kule kungerahisisha utawala kwani wote wangeweza kufika kwa kutumia muda mfupi.
2. Usalama. Alisema Jiji la Dar Es Salaam lililoko pembezoni mwa bahari ya Hindi liko sehemu ngumu ki ulinzi kwa hiyo ingekuwa salama zaidi kama Makao yangehamishiwa katikati ya nchi.
Izingatiwe nchi yetu ilikuwa ikitishiwa na mashambulio toka kwa Wakoloni na Walowezi wa Msumbiji, Rhodesia na Afrika ya Kusini ya kibaguzi.
Mwisho alisisitiza kuhamia Dodoma si kuhamisha majumba. Na alisisitiza zoezi lile kufanywa kwa awamu, taratibu bila kuujeruhi uchumi.
Kweli mchakato ulianza na kuendelea vema hadi ilipozuka vita dhidi ya Nduli Iddi Amin ambapo fedha, mali na amali zote zilielekezwa huko.
Uchumi ulivurugwa kwelikweli baada ya vita, mdororo wa uchumi ulitatiza zoezi zima na ajenda ya kuhamia Dodoma ni kama ilisahaulika.
Kuisha kwa tawala za kilowezi na kikoloni Kusini kwetu kulipunguza zaidi uzito wa sababu ya pili. Na kwa kweli mabadiliko makubwa katika tekinohama sasa yamepunguza au kuondoa kabisa sababu ya kwanza!
Kwa maoni yangu kuhamisha Makao sasa ni kujibebesha zigo lisilo na faida kubwa!
Sent using
Jamii Forums mobile app