Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Haiwezekani serikali kumlazimisha mtu asifunge kiwanda. Wakilazimisha usifunge si unakiacha kijifie chenyewe yaani unaacha mali ghafi zilizopo ziishe na wafanyakazi unawaambia kuna hali mbaya ya kiuchumi wanaopenda kuendelea kujitolea bure kwa manufaa ya nchi waendelee wanaotaka malipo haitawrzekana.
 
Haya ni matatizo ya uchumi mdogo, usio na ushindani, usio na ufanisi, usio na uhuru, unaoingiliwa sana na serikali.

Kwenye uchumi ulio na ushindani na ufanisi, serikali haiwezi kumbembeleza mtu asifunge kiwanda chake, kwa sababu wafanyabiashara wengi watakuwa wanaililia nafasi hiyo kufanya biashara.

Kauli ya Bashe inaonesha udhaifu mkubwa katika ufanisi wa uchumi wa Tanzania.

Biashara ambayo inatakiwa kuwa huria, ikiwa na sifa za biashara huria za wafanyabiashara kuweza kuingia na kuondoka katika biashara muda wowote wanapoona sawa kufanya hivyo, inaingiliwa na vikwazo vya serikali kumkatalia mfanyabiashara asiondoke kwenye ulingo wa biashara.

Kwa maneno aliyoyasema Bashe, ukiyachukulia moja kwa moja, ni kama vile Bashe kavunja kanuni za kuruhusu biashara binafsi kuamua kuingia na kutoka katika biashara, na kavifanya viwanda vya Mo, vya kampuni ya mtu binafsi, viwe kama vya serikali.
Daaaah !
 
Mambo si mepesi hivyo. Kama serikali imekuambia njoo tuzungumze tatizo unaenda kuzungumza.
 
Haya ni matatizo ya uchumi mdogo, usio na ushindani, usio na ufanisi, usio na uhuru, unaoingiliwa sana na serikali.

Kwenye uchumi ulio na ushindani na ufanisi, serikali haiwezi kumbembeleza mtu asifunge kiwanda chake, kwa sababu wafanyabiashara wengi watakuwa wanaililia nafasi hiyo kufanya biashara.

Kauli ya Bashe inaonesha udhaifu mkubwa katika ufanisi wa uchumi wa Tanzania.

Biashara ambayo inatakiwa kuwa huria, ikiwa na sifa za biashara huria za wafanyabiashara kuweza kuingia na kuondoka katika biashara muda wowote wanapoona sawa kufanya hivyo, inaingiliwa na vikwazo vya serikali kumkatalia mfanyabiashara asiondoke kwenye ulingo wa biashara.

Kwa maneno aliyoyasema Bashe, ukiyachukulia moja kwa moja, ni kama vile Bashe kavunja kanuni za kuruhusu biashara binafsi kuamua kuingia na kutoka katika biashara, na kavifanya viwanda vya Mo, vya kampuni ya mtu binafsi, viwe kama vya serikali.
Serikali imeweka wazi nia yake ni kuokoa hizo ajira. Binafsi naona wapo sawa. Tatizo la ajira lipo hata kwenye nchi zenye uchumi mkubwa.
 
Tanzania Makodi ndo Tatizo kubwa na Wanasiasa awapo Tayari kushughulikia hilo... Walio wengi wanaona sawa tu.Mitambo ufunguliwa na kufungwa tena. Huko Rwanda anaweza pokelewa na kupewa King size treatments na malighafi zikapita hapa hapa Dar... Sisi tukawa tuna import MO Energy toka Rwanda. Tanzania Umeme bei juu.Kodi zipo nyingiii na zipo juu,Garama za Logistics zipo Juu kutokana na Bei ya Diesel na Petrol... Mfanya Biashara anaponaje??Ipo haja ya Serikali ya Tanzania kujifunza India juu ya Maswala ya Kodi na Pia kuja na mikakati ya kuongeza Walipa Kodi..... Tanzania inauwezo wa kuongeza walipa kodi zaidi ya 10M kwa mwaka 2024-2026 ,Tatizo Wahusika kwa kuwa wanapata Mishahara kila Mwezi na Marupurupu they dont care! Kuna Kampuni ilikujaga hapa TZ kushauri TRA njia za kuongeza idadi ya walipa Kodi.... Wakaambulia za uso.
Kampuni hiyo ilishauri njia zipi mkuu
 
Zipo taarifa kwamba Serikali ya Tanzania imekataa ombi la Mohamed Dewji la kutaka kufunga kiwanda chake cha chai.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amemuomba Bwana Dewji kufanya majadiliano na Serikali kwanza kabla hajachukua uamuzi huo, ambao unatarajiwa kuathiri watu wengi wanaofanya kazi kwenye kiwanda hicho.

Lakini swali letu ni hili, kwanini MO amefikia hatua ya kufunga kiwanda chake alichojenga kwa gharama kubwa na kufunga mitambo ya kisasa? Kuna nini?

Swali jingine ni hili, kwanini jambo hili lishughulikiwe na Wizara ya kilimo badala ya Wizara ya Viwanda?

======

Serikali imegoma kuridhia ombi la kufungwa kwa Kiwanda cha chai cha Mo Enterprises na Viwanda vingine kadhaa Nchini ili kuepusha athari ikiwemo Watu kupoteza ajira.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwa Dodoma leo, amesema kama Wawekezaji wana changamoto yupo tayari kujadiliana nao ili kuzitatua huku viwanda vikiwa vinaendelea na uzalishaji.

“Nimepokea barua ya kampuni ya Mohamed Enterprise kutaka kufunga Viwanda nimewaambia hawawezi kufunga viwanda, tujadiliane njia nyingine lakini sio kufunga kwasababu kwetu bado sekta ya chai bado ni muhimu kwa ajira za Watu, binafsi naamini nikienda Rungwe kama Wakulima wangekuwa hawana mazao mengine umasikini ungekuwa mkubwa mno kwa hali ya chai ilivyo, Lupembe, Mafinga, Mufindi kote hali ingekuwa mbaya”

“Nimepokea maombi ya MO kuja kwetu Serikali kwamba Serikali tuyachukue mashamba (ili kuyaendeleza) tutaunda Timu itaenda kuyakagua tutaangalia thamani halisi ya wakati huu kwasababu hayakutunzwa vizuri mashamba wala vile Viwanda kwa muda mrefu sana kwahiyo tutaangalia njia zote lakini sekta ya chai itaendelea kuwa hai, nimeagiza hakuna kufunga kiwanda lazima waendeele na uzalishaji hilo ni la lazima kisha tutakaa chini kujadiliana mambo mengine”

“Nawahakikishia ninaendelea na majidiliano na Wizara ya Fedha ili tuwe na njia bora kupima viwango vya tozo, nimeongea na Waziri wa Uwekezaji ili hivi viwanda vipate nafuu ya kodi ya kuagiza nje kwasababu kama tunampa Mtu wa Export sehemu nafuu ya kodi, ukitazama sekta ya chai kwa ujumla bidhaa zake zinahusisha kusafirisha nje”

“Nimekaa na Timu ya Wataalamu imenifanyia uchambuzi wa bei ya majani mabichi ya chai, kwa namba inatakiwa bei ishuke lakini nimewaambia bei ya Mkulima haitoshuka tuta-mantain bei ya mwaka jana” —— amesema Waziri wa Kilimo
Acha afunge serikali yetu imezidisha sana kodi kila kona
Halafu wanasiasa wetu wakiiba hela za UMMA wanatoroshea nje ya nchi
 
Haya mambo haya... na hapo wakikaa mezani ni kwamba Serikali / Mlipa Kodi ndio atatoa Ruzuku za kufidia kama kuna hasara ili muwekezaji aendelee kuwekeza na kutoa ajira....

In reality kilichotokea baada ya Privatization na hizi Private Sectors kufanya shughuli ni vitu viwili (wakipata faida wanakula wenyewe na wakishindwa mlipa kodi anafidia) win / win for them.....

Cha maana tunahitaji na Kampuni za UMMA zipambane accordingly kwenye market na sio kuwapangia watu Binafsi wanachofanya au wanataka kufanya.... Bila hivyo hizo Kampuni Binafsi zitaendelea kuwa Binafsi mambo yakienda sawa na mambo yakienda ndivyo sivyo ni sisi ndio tutawafidia ili waendelee kuwepo / kuajiri
 
Tutashuhudia mengi sana.
Snapinsta.app_432135929_18427186045057742_2344398982620607698_n_1080.jpg
 
Attachments

  • Snapinsta.app_432135929_18427186045057742_2344398982620607698_n_1080.jpg
    Snapinsta.app_432135929_18427186045057742_2344398982620607698_n_1080.jpg
    151.5 KB · Views: 2
Hapa kazi ipo. Mara wawekezaji wanatakiwa mara ndio wengine wanaaga.
Mara serikali inahamasisha diplomasia ya uchumi mara wababe wanaleta mchele eti umewekwa virutubisho. Huku waziri wa kilimo anatoa maelekezo usitumike kule watu wa viwango wanasema wamecheki ubora
Pamoja na hayo hakuna aliewajibika wala kuwajibishwa
 
Back
Top Bottom