Kwanini Mkoa wa Kigoma unakosewa heshma?

Kwanini Mkoa wa Kigoma unakosewa heshma?

Ubumwe Bwa Banya Gigoma Nibwo Dushaka Mwiki Igihugu Chatanzania, Dabakunda Cyane Ncuti Zanje, Imana Ibe Namwe Mwese..!!
 
Nakwambia Watu Wa Kigoma Ni Watu Wenye Akili Nyingi Kama Watutsi, Hebu Chek, Pamoja Na Kutengwa Na Serikali Yao Lakini Wanatusua Tu.. Kigoma People Are Genious..!!
 
Mods tafadhari naomba usiunganishe uzi huu. Katika hali ya kusikitishwa napenda kusema kuwa wanakigoma wanadharaulika sana japo sina nia ya uchochezi ila nasema ukweli.

Kigoma imetajwa na wengi kuwa ni mkoa unaotoka wasaliti hasa humu jf, waha wajinga, wanatumikia ccm, sio watanzania etc. Sasa cha kujiuliza mbona mikoa inajinasibu kuwa ndio wapinzani wa kweli hawaongozi kwa kura za kumpa mgombea urais wa upinzani? Na iongoze kigoma 2010?.
Msmamo wa ukawa kuhusu s3 umetokana na maoni mengi kutoka kigoma? Mnataka upinzani upi tofauti na huo wenye tija? Tujenge misingi ya kuaminiana. Wasira nae kaongezea.

Poti, achana nao. Kigoma ndo mwisho wa reli, mwisho wa ujinga. Huwezi kutaja historia ya upinzani katika nchi hii bila kuitaja Kigoma. Waache watukane, wadharau, wabeze-chochote kile, lakini hapa ngo wamefika. Leka dutigite!!
 
Waha wa Kigoma wanaakili sana! ila kinachotuponza watu wa Kigoma hatuna ile tabia ya kulamba visigino vya viongozi wetu wa juu; kiongoz yeyote akikosea anaambiwa ukweli hapohapo! Muha huwa hana unafiki wa kusema "NDIYO MZEE" Mkigoma hatongozeki kirahis na ndio maana uchaguz wa 2010 kura nyingi za urais SLAA alipata kura nyingi mno (alimzidi mbali sana BABA RIZIONE) licha ya kwamba kuliwepo na mgombea urais kutoka Kigoma wa chama flani cha siasa; wabunge wote wa NCCR kutoka Kigoma walinyimwa fursa ya kugombe ndani ya CDM wakahamia NCCR tukawafuata hukohuko kwa kuwapa kura. CDM iliweka wagombea wenye uwezo mdogo; mfano Kafulila Vs yule mwarabu. Mikoa ming hapa TZ inayojifanya wananchi wake wanaakili imekua ikiongozwa na MAGAMBA, ujanja wenu uko wapi nyie. Nyie wa kaskazini na wengine MIDEBWEDO tulieni wenye nguvu za kufanya kazi tuwaingizie kitu cha moto. Binafsi watu wa mkoa wa Mara nawakubali sio walamba visigino/misukule. R.I.P Chacha Wangwe, you'll always be remembered.
 
Acknowledgment to bibikuku

Soma hii msariti itakusaidieni, watu wa Kigoma.

Makala hii iliandikwa Mwaka Juzi kwenye Gazeti moja kuhusu tabia za wanasiasa wa mkoa wa Kigoma. Niliamua kuihifadhi bila kujua kama haya yatatokea leo. Hebu soma kisha tujadiliane, Ingawa ni ndefu kiasi lakini very interesting kuisoma:

MKOA WA KIGOMA NA HISTORIA YA WANASIASA WAKE

Sina shaka utakubaliana nami kuwa mkoa wa Kigoma ni kitovu cha upinzani nchini Tanzania. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa kipindi cha karibu miaka 20 sasa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania, mkoa huu umekuwa chachu ya mafanikio katika upinzani.


Kwa haraka haraka, sina shaka wapo wanaokumbuka namna Dr Aman Walid Kabourou alivyokisumbua Chama cha Mapinduzi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, ambapo wakati huo akiwa Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) alipambana vikali na Azim Premji kuanzia katika sanduku la kura hadi mahakamani.


Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, ulishuhudia mkoa wa Kigoma ukiwa moja ya mikoa iliyotoa wabunge wengi kuwakilisha upinzani. Bila shaka ni kutokana na kile kinachoonekana kama mkoa huu kutengwa katika mipango mbalimbali ya maendeleo inayowekwa na serikali ya CCM.


Haikuwa ajabu kwa Dr Kabourou hatimaye mwaka huo kutinga bungeni akiwakilisha CHADEMA kwani tayari alikuwa ni moto wa kuotea mbali na alionekana kama mkombozi wa kweli wa matatizo ya watu wa Kigoma mjini.


Moto huo wa upinzani mkoani Kigoma mwaka 1995 ukasambaa zaidi na kutinga jimbo la Kasulu Mashariki ambapo Daniel Nsazugwako alichaguliwa kuwa mbunge akipitia NCCR-Mageuzi, chama ambacho kwa mwaka huo, ndicho kilichopata wabunge wengi zaidi wa upinzani kwa upande wa Tanzania Bara.


Kutokana na kukomaa huko kwa hisia za mapinduzi ya kisiasa kwa wana-Kigoma, haikushangaza kwa CHADEMA kumpa cheo kikubwa Dr Kabourou ambaye alikuwa Katibu mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa.


Safari ya kuikomboa Kigoma kupitia upinzani iliendelea mwaka 2000 ambapo Jimbo la Kigoma Kusini lilimchagua GulamHussein Kiffu kuwa Mbunge wake na wakati huo akiwakilisha chama cha NCCR-Mageuzi. Kiffu alikuwa mmoja wa wabunge wachache sana wa NCCR ambao walichaguliwa mwaka huo wa 2000 ikiwa ni baada ya chama hicho kupigwa na kombora la kisiasa na kuanza kupepesuka. Hata hivyo, ubunge wa Kiffu ulikoma miaka miwili baadae baada ya kuondolewa na mahakama.


Mwaka 2005 Kigoma iliyumba kidogo, lakini safari hii naweza kudiriki kusema mkoa huu ulilamba dume kwa kumpata mwanasiasa kijana na machachari (sana) Zitto Zuberi Kabwe aliyechaguliw akuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA.


Ni dhahiri kwamba kuingia kwa Zitto bungeni pamoja na Marehemu Amina Chifupa (CCM), ilikuwa chachu kwa vijana wengi kujiona kuwa kumbe wanaweza kuwa wabunge na hatimaye wengi kujitokeza kugombea nafasi hiyo mwaka 2010. Haya ni moja ya mafanikio ya uwepo wa Zitto bungeni kuanzia mwaka 2005.


Moto ambao ulionekana kufifia mwaka 2005, uliwaka kwa kasi ya ajabu mwaka 2010 ndani ya mkoa huo wa Kigoma baada ya majimbo matano kuangukia mikoni mwa wapinzani. CHADEMA ikapata jimbo moja na NCCR ambao ni kama watawala wa upinzani mkoani humo wakaibuka na majimbo manne.


Kati ya majimbo ambayo wapinzani walitwaa mwaka 2010 ni pamoja na Muhambwe ambapo Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) aliibuka mbabe, Kigoma kusini ikachukuliwa na rafiki yangu David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Zittp akiendela kutawala Kigoma Kaskazini.


Naamini hadi hapo utakuwa umekubaliana name kuwa Kigoma ni kitovu cha upinzani hapa Tanzania. Hii ni kutokana na kila uchaguzi kuhakikisha kuwa mkoa huu haukosi mbunge ama wabunge wa upinzani tena wa kuchaguliwa na wananchi wenyewe. Lakini waswahili husema ‘kwenye msafara wa mamba, hata kenge wamo.’


Wapinzani wengi kutoka mkoa wa Kigoma wamekuwa wakileta mkanganyiko mkubwa katika siasa za Tanzania. Mkanganyiko huu umekuwa ukijitokeza ama ndani ya vyama vyao vya siasa ama hata kuhama toka chama kimoja kwenda kingine (na wengine kurudi CCM).


Dr Kabourou namchukulia kama alikuwa mwamba wa upinzani mkoani Kigoma miaka ya 90. Dr Kabourou alishika nafasi kubwa ya uongozi ndani ya CHADEMA miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni. Dr Kabourou ni msomi aliyebobea. Lakini kisiasa leo hii Dr Kabourou ni mwana-CCM imara na anakiwakilisha chama katika bunge la Afrika Mashariki. Je, huyu bwana alikuwa mpinzani wa kweli, au alikuwa anapita tu CHADEMA, au alikuwa na lake jambo enzi hizo? Nauliza tu!
Bw Nsazugwako alikuwa mwana-NCCR mzuri na aliwawakilisha vizuri wananchi wake bungeni kuanzia mwaka 1995. Lakini mwaka 2005 huyu bwana akaibukia CCM kuwania ubunge na hatimaye akapata hadi uwaziri mdogo. Akitokea kulekule Kigoma, nauliza huyu Nsazugwako naye alikuwa mpinzani wa kweli ama pia alikuwa ana lake jambo?


Gulamhusein Kiffu naye hayuko nyuma katika mkumbo wa wenzake. Alionja ubunge kwa miaka miwili kupitia NCCR Mageuzi kabla ya Mahakama kumuondoa. Kuona hivyo akaamua kujaribu tena kurudi bungeni 2010 lakini kupitia CCM ambako hajafaulu. Hii ni adhabu anayoipata kwa kuusaliti upinzani au? Ah, nauliza tu!


Hao ni wana-Kigoma ‘waliotesa wakiwa wapinzani’ ambao kwa sasa wote wamejiunga na CCM. Wapo wale ambao bado ni wapinzani, lakini wamekuwa wakizua mkanganyiko kila uchao ndani ya upinzani.


Tunakumbuka vema kuwa David Kafulila, kwa sasa mbunge wa Kigoma Kusini NCCR mageuzi, alikuwa CHADEMA hapo awali, na akajiondoa ndani ya chama hicho muda mfupi baada ya kufuliwa cheo chake cha uafisa habari. Waswahili husema ‘ Mjasiri haachi asili.’ Hata baada ya kwenda NCCR na kupata ubunge, Kafulila amekuwa na asili ile ile ya u-Kigoma ambayo imeuweka ubunge wake (na uanachama wa NCCR pia) rehani hadi sasa ukisubiri uokovu wa mahakama.
Felix Mkosamali kutoka Mhambwe, naye alianza kufuata nyendo zile zile za ‘mzoefu’ Bw Kafulila. Lakini NCCR imemfunga ‘speed governor’ mapema na walau kwa sasa anaonekana kama ametulia. Labda pia na umri ulikuwa bado.


Zitto Kabwe! Nashindwa hata nianzie wapi kuelezea. Amekuwa haishiwi vituko kila wakati. Ilianza kama mzaha alipokuwa anautaka uenyekiti wa CHADEMA taifa, jambo lililoleta mkanganyiko mkubwa na hatimaye busara za wazee wa chama hicho zikaokoa jahazi ili chama kisimeguke.


Uhusiano wa karibu baina ya ‘mpinzani Zitto’ na Ikulu ya JK nao umekuwa ukileta sintofahamu ya lengo hasa la mwanasiasa huyu. Ikumbukwe kuwa kati ya majimbo ambayo JK hakutia mguu wakati wa kampeni za 2010 ni jimbo la Kigoma Kaskazini na hii inadaiwa na wadadisi wa maswala ya kisiasa kuwa inatokana na uswahiba wa wawili hawa. Hii inaonyesha nini na inatupa picha gani kwa mpinzani na mtawala kuwa maswahiba kiasi hiki? Nauliza tu!


Hivi majuzi Zitto kaja na mpya ambapo ameeleza wazi kuwa anautaka urais wa Tanzania! Anataka siku moja atambulishwe kama ‘Rais wa Jamhuri ya muungano (kama utakuwepo) wa Tanzania Mheshimiwa Zitto Kabwe.’ Duh!
Kama ilivyokuwa wakati ule alipodai anautaka uenyekiti wa CHADEMA, naamini sio masihara na halitaisha leo jambo hili, litaendelea kuitafuna CHADEMA na vigogo wake na kuwagonganisha vichwa hadi 2015! Labda tujiulize kwanini Zitto amesema haya leo huku chama chake kikisaka kura kwa udi na uvumba kule Arumeru? Je, kuna agenda ya siri ndani yake ama ndi wakati muafaka kwake?


Hao ndio wapinzani kutoka mkoani Kigoma. Leo NCCR Mageuzi kufa, kesho CCM damu! Wengine wanakula na kulala leo Chadema, kesho wanaamkia CCM ama NCCR Mageuzi! Nahisi mwanamuziki Jaguar hakukosea katika wimbo wake aliposema “Nimtazame nani nimuamini nani, wananigeukia, vigeugeu wananigeukia. Paka wangu kigeugeu, bibi yangu kigeugeu, na wanasiasa vigeugeu……. ”!
============================== ===========================

Nimeikopi makala hii kama ilivyo, je waweza kumuon doa Zitto kutoka katika kundi hili la wanasiasa watokao Kigoma? TAHADHARI; HATUZUNGUMZII UKABILA HAPA!

Duuh ndefu sana aisee ila ina logic sana..
 
Last edited by a moderator:
Waha wa Kigoma wanaakili sana! ila kinachotuponza watu wa Kigoma hatuna ile tabia ya kulamba visigino vya viongozi wetu wa juu; kiongoz yeyote akikosea anaambiwa ukweli hapohapo! Muha huwa hana unafiki wa kusema "NDIYO MZEE" Mkigoma hatongozeki kirahis na ndio maana uchaguz wa 2010 kura nyingi za urais SLAA alipata kura nyingi mno (alimzidi mbali sana BABA RIZIONE) licha ya kwamba kuliwepo na mgombea urais kutoka Kigoma wa chama flani cha siasa; wabunge wote wa NCCR kutoka Kigoma walinyimwa fursa ya kugombe ndani ya CDM wakahamia NCCR tukawafuata hukohuko kwa kuwapa kura. CDM iliweka wagombea wenye uwezo mdogo; mfano Kafulila Vs yule mwarabu. Mikoa ming hapa TZ inayojifanya wananchi wake wanaakili imekua ikiongozwa na MAGAMBA, ujanja wenu uko wapi nyie. Nyie wa kaskazini na wengine MIDEBWEDO tulieni wenye nguvu za kufanya kazi tuwaingizie kitu cha moto. Binafsi watu wa mkoa wa Mara nawakubali sio walamba visigino/misukule. R.I.P Chacha Wangwe, you'll always be remembered.

Waha kwani ni watanzania? si ni wanyarwanda wale.
 
Duuh ndefu sana aisee ila ina logic sana..

Hiyo habari imedangaya kwa kiasi flani. Mfano imedanganya kuwa Nsanzugwanko aliwahi kuwa mbunge wa Kasulu kupitia NCCR! Daniel Nsanzugwanko hajawahi kuwa mbunge wa NCCR! ila alikua mgombea kuptia NCCR kabla ya kuwa mbunge 2005-2010 (CCM). Wabunge waliowahi kuiwakilisha Kasulu ni wafuatao; Mh Teddy Kilenza (marehem)(CCM) 1995-2000, David Musatti (marehem) CCM 2000-2005; Daniel Nsanzugwanko(CCM) 2005-2010; Zaituni Buyogera(NCCR) Kasulu vijijin & Moses Machali(NCCR) Kasulu Mjini 2010-2015.
 
Wanakigoma wanachezewa na wanasiasa wao, wanawapiga Udalali tu, wanawatumia kama bidhaa sokoni! Mnawapa dhamani halafu wanawapiga bei!
 
nafikiri kwa kuwa wachawi na washirikina wengi wanatoka kigoma. usaliti umejengwa ktk misingi ya uchawi na ushirikna.
 
Hakuna anaeichukia wala kuitenga kigoma Tatizo mnachagua wapinzani ambao hawana serikali, 2015 chagueni CCM muone utekelezaji wa Ilani.

Serikali ya CCM imekuwepo Kigoma tangia mwaka 1977!
Ilishindwa nini kutekeleza ilani yake?
Na sasa inyotekelezwa si ni ilani ya hao CCM?
 
Back
Top Bottom