Rais Magufuli amebadilisha siasa za mkoa wa Kigoma

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
713
1,136
Kugoma ni muongoni mwa mikoa ambayo raia wake ni wabishi sana kwa maana ya kujenga hoja na kutokukubali kuburuzwa na kuonewa. Ni miongoni mwa mikoa ya mwanzo kabisa kuthubutu kuchagua wabunge wa upinzani wakati siasa za vyama vingi ziliporudishwa tena mwaka 1992.

Toka wakati huo siasa za mkoa wa Kigoma zimekuwa zikitaborika sana hasa majimboni kuwa nani atakuwa mbunge kila mara uchaguzi mkuu ulipowadia.

Kulikuwa na wababe wa siasa za Kigoma kiasi kwamba ilikuwa ni vigimu sana mtu mwingine kuingia ndani kwani walikiwa wamejifungia humo hao wababe na hawakuta mtu mwingine kuingia.

Lakini toka rais Magufuli aingine na kushika madaraka sasa siasa za mkoa wa Kigoma zimebadilika kwa kiasi kikubwa sana.

Na zimebadilika sana mara baada ya rais Magufuli kuwateuwa wabunge wawili kutoka Kigoma kwa maana ya Dr Mpango na Prof Ndalichako na kuwapa uwaziri.

Kuanzia hapo ndipo siasa za mkoa wa Kigoma zikaanza kubadilika.

Kabla ya wakati huo kulikuwa na wabunge sugu ambao ilikuwa ni vigumu sana kuwaona wakishindwa kwenye kura za maoni kama vile Albert Ndibaliba wa Buhigwe na Daniel Nsanzugwako wa Kasulu mjini. Lakini sasa mambo yameenda tofauti kwani wawili hao wote wamegaragazwa kwenye kura za maoni kwenye mchalato ndani ya CCM, huku mbabe mwingine wa Kigoma Kaskazini na Kigoma mjini bwana Serukamba akipita kwa mbinde.

Kule Buhigwe ambako jimbo hilo linaundwa na tarafa za Manyovu na Muyama ilikuwa ni vigumu sana kwa mbunge mwenye asili ya Muyama ambako watu wake si wengi kama wa Manyovu kushinda kwenye kura za maoni.

Na hicho ndicho kilimfanya Obama awe na uhakika wa kushinda kura za maoni kwani alitegemea wajumbe wote wa ukanda wa Manyovu wangempigia kura. Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo sijui ni kwa kuwa alikuwa akishindana na waziri mwenye dhamana ya fedha au ni kuchokwa tu kwani amehudumu kwa mihula miwili mfurulizo.

Hoko Kasulu nako Ndalichako kambwaga Nsanzugwako, sijui ni kwa kuwa ni waziri au wajumbe walimchoka sana Nsanzugwako nae pia kahudumu kwa muda mrefu sana.

Natarajia pia Kafulila kurudi japo kwenye kura za maoni hakushinda lakini CC ya chama inaweza amua vinginevyo.

Hata Kigoma Kaskazini inaweza kuwa hivyo kwani mbunge wake ana miaka 15 kwa maana 10 aliyotumikia jimbo la Kigoma mjini na 5 aliyotumikia Kaskazini. Kama akipata tena mwaka huu itakuwa 20. Sijui kama jina lake litarudi ama la.

Lakini kusema ukweli ningependa kuona wabunge wapya wakiapishwa kama wabunge kutoka Kigoma. Na kwa hili rais Magufuli amesaidia sana ku-shape siasa za mkoa wa Kigoma.
 
Kigoma ilikuwa ni ya akina Lord Jabu Hussein, Jairos Bidyanguze na William Bidyanguze, na Lake star ya akina Hamis Askari Aloo Mwitu wewe mleta mada unaniambia Kigoma gani?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom