Kwanini mbwa hugongwa sana na magari barabarani?

Kuna Mbwa wa Afrika wana taabu sana. kwanza anafungwa mnyororo unamkaba shingo,analazimishwa kuvuta bangi na ugoro awe mkali,anakula mabaki ya bar walevi wasipobakiza analala njaa,akienda kujitafutia jalalani anapigwa mawe bila sababu,anajikuta na mawazo anagongwa gari anakufa.
 
Kuna Mbwa wa Afrika wana taabu sana. kwanza anafungwa mnyororo unamkaba shingo,analazimishwa kuvuta bangi na ugoro awe mkali,anakula mabaki ya bar walevi wasipobakiza analala njaa,akienda kujitafutia jalalani anapigwa mawe bila sababu,anajikuta na mawazo anagongwa gari anakufa.
huko mbinguni waafrica wote back-bench
 
Moja ya sababu ya kugongwa kwa mbwa ni la kibaiolojia zaidi tena wanaogongwa ni mbwa dume ipo hivi,mbwa jike anapokua katika heat period kwa binadamu wanawake tunasema wanapokua ovulation( yani siku tayari ya kupata mimba) mbwa majike uwa wanatoa harufu kama ishara yakuwa tayari kwa hilo tendo hivyo kutokana na uwezo wa mbwa kunusa mbwa dume anaweza akaisikia hiyo harufu toka mbali na inapelekea kuanza kutafuta mwelekeo wa hiyo harufu akitumia hisia zaidi na msukumo wa homoni bila kutumia akili katika matendo yake hivyo kutokujali uwepo wa barabara au magari ilimradi lengo lake litimie kwenye mwelekeo wa harufu kwenda kutimiza haja yake hapo ndipo huwa wanapogongwa!
Hili ndilo jibu. Asilimia 95 ya mbwa wanaogongwa huwa madume.
 
Ni kwa sababu ya kuhisi kuwa yeye ni rafiki wa binadamu kuliko mnyama yoyote kufikia hatua ya kumwamini binadamu akijua dereva akimwona atachukua tahadhari na umakini kwa kupunguza mwendo au kusima kama anavyofanya kwa binadamu mwenzake
 
jibu ni kwamba mbwa huwa anakosa maamuzi sahihi inapotokea amepigwa na mwanga mkali wakati wa usiku,ikumbukwe uoni wa wanyama ni tofauti kabisa na ule wa binadamu na kila mnyama anaona kutegemea na macho yake yamekua programmed kuona vipi.

mbwa akipigwa na mwanga anapata uoga…hata kama siyo barabarani,sasa ikiwa ni barabarani ule uoga unamfanya kukosa maamuzi ya haraka na kupelekea kukanyagwa.

hata ikitokea akaamua aende wapi mbwa huwa anaamua kurudi alikotoka,hicho kitendo kinapelekea kugongwa sababu hana speed na siyo flexible kama paka.

lakini sababu nyingine ndio hiyo mentality watu wako nayo kwamba ukiona mbwa wewe gonga tu sababu anaweza kuwa ni uchawi,kwahiyo madereva wengi wanawapitia bila huruma.

kuna sababu umeikataa hapo juu lakini ni ya msingi…population ya mbwa wanaozurura nje ni kubwa kuliko paka,mbwa wengi wanafugwa kiholela tu mitaani tofauti na paka ambao zaidi wanafugwa ndani na hawana zile safari ndefu kwa ajili ya mating.

mbwa dume hata umfuge ndani ya wigo ila akawa free siku akisikia harufu ya jike atalifuata akalipande hata kama liko wapi,ila asubuhi utakuta kesharudi

akigongwa huko njiani ndio inakua ajali tu
 
Mbwa wengi wanagongwa wakati wa usiku na sio mchana na wakati wa usiku mbwa ndio anaona vizuri sana,wakati wa giza macho ya mbwa rods (scotopic vision)zake huwa active sana kuliko cones(photopic vision),hivyo humchukua muda mrefu kubadilishana mawasiliano ,hivyo ikitokea mbwa anavuka katika giza na gari ikatokea maana yake macho yake yatashindwa kuona hivyo mara nyingi wanalazimika kusimama ama kuendelea na safari kitu ambacho ni hatari kwao
Unamaanisha mbwa ni aina ya wanyama nocturnal
 
kuna mtu alijaribu kukutetea hapo kwenye bold akidhani hukumaanisha hvyo
"Nilishuhudia mbwa 6 wamegongwa", hii ni sentensi inayowakilisha tukio lililotokea wakati uliopita, ambapo wakati linatokea, mimi sikuwepo. Laiti kama ningesema: "nilishuhudia mbwa 6 wakigongwa", hii sentensi nayo inawakilisha wakati uliopita, ila safari hii tukio limetokea nami nikiwepo. Ni Kiswahili cha kawaida tu!
 
"Nilishuhudia mbwa 6 wamegongwa", hii ni sentensi inayowakilisha tukio lililotokea wakati uliopita, ambapo wakati linatokea, mimi sikuwepo. (hapa hukushuhudia bali ulishuhudiwa[/coror])
Laiti kama ningesema: "nilishuhudia mbwa 6 wakigongwa", hii sentensi nayo inawakilisha wakati uliopita, ila safari hii tukio limetokea nami nikiwepo. Ni Kiswahili cha kawaida tu!
hatujuwi kiswahili.. Any way tusitoke nje ya mada
 
Afrika, hasa Tanzania, tunapenda sana kupiga wanyama hasa mbwa na paka. Dereva akiona mbuzi au nguruwe anavuka barabara, atapunguza mwendo na kumuacha avuke.

Ila akionekana paka au mbwa, hapo speed itaongezwa maradufu.
Inasikitisha sijui kifanyike nini ili jamii hii
Ulitegemea kukuta mizoga ya mbuzi na kondoo waliogongwa magari ikiwa barabarani?

Ile ni mboga,wanagongwa na kubebwa tofauti na mbwa.
Inasikitisha sana,wenzetu wanasimamisha magari ili ndege bata na watoto wake wapite, sisi dereva ndio kwanza anamfuata mnyama akamuuwe,na abiria wanashangilia... Yaani maisha yetu ni mtihani mtupu unaweza kuwa na hamu ya kwenu ila ukifika hamu yoote inakimbia,ukitoka kwenda masokoni uchafu mtupu na harufu mbaya,watu wenyewe kutwa matusi, ukirudi bila kutukanwa umshukuru Mungu.. huruma na wanyama itatoka wapi wakati maisha yetu afadhali ya wao.
 
Akigongwa mbuzi mapema sana ataokotwa kufanywa kitoweo. Mbwa akisha kufa hana matumizi mengine kwa binadamu ndio maana unawakuta barabarani
 
Kuna siku nilikuwa na gari na dereva wa gari moja. Alifyatua kama mbuzi sita wakafa pale pale. Kesho yake narudi hata damu hamna. Mbwa haliwi labda fisi akibahatika kupita hapo
 
Back
Top Bottom