Usifuge viumbe hai nyumbani kama huna muda au uwezo kuwatunza

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,723
3,366
Kuna watu wananunua wanyamahai kama mbwa, paka n.k kwa ajili ya kufuga majumbani kwao.

Cha ajabu unakuta wanyama hao wanazuruza tu ovyo huko barabarani bila uangalizi wowote na wengine wanaishia kugongwa na magari.

Mara kadhaa nimekutana na wanyama hawa tena unakuta wengine ni wale wa manyoya laini wa ndani wa bei kali.

Sasa unashangaa mtu huyu amefuga kwa mapenzi ya mnyama husika au ndo vile kwa sababu jirani anao basi lazima na wewe uwe naye mwende sawa?
 
Nilikuwa na paka wangu huyu paka hatoki kwenye geti na kula yake ni vile vyakula ya kwenye packet tu.

Kunasiku nilitoka nae akanifata nikaona acha aone nje kuna vijana kumuona wakasema duh huyu paka mzuri kweli wanani(hapa walisema kama wanataka kumuiba).

Huyu paka akawa namuachia nikitoka natoka nae nikirudi anaingia ndani(kitendo cha dakika 10 tu) sasa huyu paka kapotea mwaka sasa sijui hata ilikuwaje.
 
Samahani ninae yuko kwenye mikono salama, nunua mwingine ila awe mzuri zaidi.
 
MBWA KOKO NA PAKA SHUME WENGI SANA MTAANI SABABU YA KUKOSA MATUNZO
sure. tatizo watu wanafikiri ni rahisi sana kufuga hawa wanyama. matokeo yake wanaishia kushindwa kuwahudumia vizuri mbwa na paka wanaamua kuingia road
 
Back
Top Bottom