Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Nilikuwa nimekaa na kushangaa kuona picha za mawaziri wakiwa wamepewa maua na kuvishwa mashada na kupewa pongezi za kuupata uwaziri/unaibu. Mara swali likanijia hivi wanapongezwa kwa ajili gani? Unapomuambia waziri "hongera" unampa hongera ya kitu gani alichofanya? ukizingatia:
a. Hawakufanya lolote kuteuliwa kwani kuteuliwa ni prerogative ya Rais
b. Hawakuomba kuteuliwa au kutuma maombi
c. Hawakushindanishwa na wao wakashinda (kama ilivyokuwa kwenye kura za maoni au uchaguzi)
d. Hawajafanya lolote kuweza kuwafanya watu wasifie kazi yao na kuwapa hongera
Yaani, wamepewa tu uwaziri!!! Kwanini tusisubiri kuwapa pongezi wakimaliza kazi zao aidha baada ya miaka mitano au baraza linapovunjika au kuvunjwa?
Binafsi naamini mawaziri wanaomaliza miaka mitano kwa mafanikio ndio wanastahili pongezi na kama wamefanya vizuri kwenye wizara zao kiasi cha kuonesha matokeo katika kubadilisha maisha ya wananchi basi wapongezwe na pongezi hizo ziende na kitita kizuri cha mamilioni ya fedha kama bonus! Siyo wao tu hata watendaji wengine wakuu. Kwanini tusiwapime kwa matokeo halafu tuwapongeze kwa matokeo hayo?
Kwa mfano, Waziri wa Ardhi anapoingia sasa (hastahili pongezi yoyote) lakini akimaliza muda wake akatuonesha kuwa alipoingia 2010 kulikuwa na migogoro ya ardhi 1000 na ninapotoka ni migogoro kumi tu imebakia; au waziri wa ujenzi anapoingia anatuambia mifereji ya maji machafu jiji la Dar yote haifanyi kazi na kusababisha mafuriko na anapotoka 2015 akatuonesha jiji ambalo mifereji yake inafanya kazi?
Kwanini tusiwapongeze kwa matokeo tunapongeza kwa kutangazwa!?
Ndio maana mwenzenu hadi sasa sijampongeza yoyote na sina mpango wa kumpongeza yoyote hadi nione matokeo ya kazi zao. Hatuwezi kupongeza wachezaji kwa kuingia uwanjani wakati hata mechi haijaanza!!! tukifungwa!?