Kwanini mawaziri na manaibu wanapongezwa kabla ya kufanya lolote?

Neno linalotumika sana kwenye vyombo vya habari ni WAMEULA/AMEULA, linabeba maana nzito sana!
 
:embarrassed::redfaces::hungry::disapointed::Cry::embarassed2::sad:INAUDHI MNOOOO! KWA JINSI MAMBO YA HII NCHI YANAVYOENDESHWA NA HAWA WATU.....NAHISI KUJILIPUA KABISA!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Usijilipue ndugu yangu....WALIPUE
 
Mwakei,

Tatizo letu ni kuona teuzi kama reward za ulaji kama Companero alivyobainisha badala ya kupokelewa kama ni kuaminika kuwa mtu ana uwezo madhubuti wa kufanya kazi na kuheshimu dhamana anayopewa.

Kutokana na mazingira ya kibwanyenye na upendeleo unaotoa kipaumbele kwa "maisha bora" kwa Wateule, ni wazi pongezi hizi si kwa ajili ya kupewa majukumu makubwa bali ni pongezi za kuondokana na karaha, maudhi na mahangaiko ya maisha ambayo yanawakabili Watanzania.

Ni jadi yetu kutokupima utendaji wa kazi wa mtu, iwe ni uadilifu, ufanisi au uwezo wa kuongoza kwa haki na uhamasishaji. Hii ni kutokana na tafsiri potofu tuliyonayo kuhusu kazi na uchapakazi hasa inapotokea kwenye suala la vyeo na mvuto wa kisiasa.
 
Siku hizi uwaziri ni kazi na unatafutwa. kupongezwa ni juhudi binafsi. suala, atawafanyia nini watanzania ni la ziada-very minor
 
Kuwapongeza ni sawa na kumpongeza mtoto aliyechguliwa kujiunga kidato cha kwanza au cha tano shule ya serikali.
Unampongeza sababu

  • wapo wengi wenye uwezo wameachwa sabbu ya nafasi kuwa ni chache si kwa sababu hawakuwa na vigezo.ifupi unpongeza kwa sababu kapata bahati.
Tatizo wengine wanajisahu wandhani zile nafasi wamechaguliwa wao kwa sbabau hakukuwa na wengine wanaofaa. matokeo yake ndo kwa mfano wa shule mtoto anamaliza form for na DIV I anauja kumaliza form six na DIV IV.

Na hao wateuliwa wengi wanajisahau wandhani wakishateuliwa kazi imekwisha. na mbaya zaidi "mwalimu" wao..........
 
Kwa hiyo wenye kustahili kupongezwa ni wale wenye kurudi - kitu ambacho naamini ni fair maana ni kuwa kuna kitu labda wamefanya kuweza kustahili kurudi na hasa wale ambao wamedumu kwenye nafasi mbalimbali (kama waziri/naibu) kuanzia JK alipoingia madarakani. Lakini vipi kuhusu hilo wazo la kuzawadia matokeo kwa kutoa bonus ya nguvu na watu wakajua kuwa akimaliza miaka mitano na akiwa na matokeo yanayopimika na endelevu x,y anastahili bonus ya kiasi fulani (either fixed or a percentage of sort).. ?

MM, hata hao waliorudi hawatakiwi kupongezwa eti kwa sababu tu wamerudi. Lazima tupime utendaji wao ktk awamu iliyopita ndo tuone kama kweli wanastahili pongezi yeyote. Mtu kama magufuli naweza kumpongeza maana angalau alifanya kitu kwenye ile wizara yake ya vitoweo. Lakini mtu kama Sofia Simba natafuta angalau tujisababu vya kumpa hata pongezi za kinafiki nakosa. Si wote waliorudi eti wamerudi kwa sababu kuna kitu cha maana walikifanya. It does not work that way in TZ. Unaweza ukafanya vizuri usirudi wakati walioboronga wamerudi tena na kupewa wizara nyeti.
 
Back
Top Bottom