Kwanini mawaziri na manaibu wanapongezwa kabla ya kufanya lolote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini mawaziri na manaibu wanapongezwa kabla ya kufanya lolote?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 28, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nimekaa na kushangaa kuona picha za mawaziri wakiwa wamepewa maua na kuvishwa mashada na kupewa pongezi za kuupata uwaziri/unaibu. Mara swali likanijia hivi wanapongezwa kwa ajili gani? Unapomuambia waziri "hongera" unampa hongera ya kitu gani alichofanya? ukizingatia:

  a. Hawakufanya lolote kuteuliwa kwani kuteuliwa ni prerogative ya Rais
  b. Hawakuomba kuteuliwa au kutuma maombi
  c. Hawakushindanishwa na wao wakashinda (kama ilivyokuwa kwenye kura za maoni au uchaguzi)
  d. Hawajafanya lolote kuweza kuwafanya watu wasifie kazi yao na kuwapa hongera


  Yaani, wamepewa tu uwaziri!!! Kwanini tusisubiri kuwapa pongezi wakimaliza kazi zao aidha baada ya miaka mitano au baraza linapovunjika au kuvunjwa?

  Binafsi naamini mawaziri wanaomaliza miaka mitano kwa mafanikio ndio wanastahili pongezi na kama wamefanya vizuri kwenye wizara zao kiasi cha kuonesha matokeo katika kubadilisha maisha ya wananchi basi wapongezwe na pongezi hizo ziende na kitita kizuri cha mamilioni ya fedha kama bonus! Siyo wao tu hata watendaji wengine wakuu. Kwanini tusiwapime kwa matokeo halafu tuwapongeze kwa matokeo hayo?

  Kwa mfano, Waziri wa Ardhi anapoingia sasa (hastahili pongezi yoyote) lakini akimaliza muda wake akatuonesha kuwa alipoingia 2010 kulikuwa na migogoro ya ardhi 1000 na ninapotoka ni migogoro kumi tu imebakia; au waziri wa ujenzi anapoingia anatuambia mifereji ya maji machafu jiji la Dar yote haifanyi kazi na kusababisha mafuriko na anapotoka 2015 akatuonesha jiji ambalo mifereji yake inafanya kazi?


  Kwanini tusiwapongeze kwa matokeo tunapongeza kwa kutangazwa!?

  Ndio maana mwenzenu hadi sasa sijampongeza yoyote na sina mpango wa kumpongeza yoyote hadi nione matokeo ya kazi zao. Hatuwezi kupongeza wachezaji kwa kuingia uwanjani wakati hata mechi haijaanza!!! tukifungwa!?
   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  There you go again, huwatakii mema kwa kazi nzuri ya ushindi waliofanya na sasa wanapokea malipo manono!
   
 3. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkubwa dalili za mtu mwenye uchungu na nchi hii utazijua tu. Wengi kati ya hao Mawaziri wako hapo kwa kwa ajili ya matumbo yao tu. Kwa hiyo ni lazima wapongezane kwa ulaji walioupata kwa miaka mitano ijayo! Mtu yoyote muwajibikaji hawezi kutoa pongezi au kukubali pongezi kabla hata ya kazi kuanza! wacha kumalizika!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Reverend.. sasa kama tunawapongeza kabla ya kufanya lolote kweli tutaweza kuwaangalia machoni wakiharibu? Mimi nadhani tungeaambia "kazi njema" na siyo "hongera". May be I need that vacation to Tahiti!
   
 5. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yaani wewe hujui y wabapongezwa??? try to ask yourself nani anawapongeza then utajua kwa nini wamepongezwa....

  1. Familia ya waziri husika, hawa ni lazima wampongeze Baba/mama/shangazi au Mjomba kwa sababu ana uhakika wa kula. then jina litakua mtaani kuwa "Mtoto wa waziri flani huyu" kwa hapa nyumbani ni heshima flani hivi

  2. Mafisadi, hawa wamepongeza koz now wanajua where wanaweza kupitisha dealz zao za kupiga pesa mingi koz tayari wameshapata signatories wa doc zao za mikataba minono itakayofanya waishi kwa raha mjini.( Fancy cars, Houses na Madem wa adabu)

  3. Wapambe, hawa wamepongeza koz wana uhakika wa ahadi walizopewa kabla waziri husika hajateuliwa. Ahadi hizi ni kama ajira katika wizara husika

  Kwa sababu kama hizi ndo maana wamepongezwa na si kwa sababu ya utendaji ambao bado hawajautenda. Labda kuna watakaopongezwa coming 2015 au kama itatokea Baraza kuvunjwa. Its a matter of time so lets wt n c....
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Questt.. kwa maneno yako ni kuwa wenye kustahili kutoa pongezi ni watu wa karibu na wanufaika wa uwaziri huo? Wananchi wa kawaida hawatakiwi kutoa pongezi siyo?
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Anayempongeza mtu kwa kupewa dhamana ya uongozi serikalini hata kabla ya kuanza kazi lazima anayo maslahi na hiyo dhamana!
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  MM kweli huwezi kumpongeza waziri aliyeteuliwa tu kwani hakuna kigezo cha utendaji wake; lakini je wale waliokuwa mawaziri kabla na utendaji wao umeturidhisha na rais ameona hivyo na kuwateua tena, hawa nao hawastahili kupongezwa kwa kupata ulaji mara nyingine?
   
 9. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa Mzee Mwanakijiji... Sisi wakawaida tuliishia kuwaangalia Luningani... Ukitazama vyema waliopewa mashada mengi mengi ni wale waliorudi kwenye uwaziri... Mfano mwingine ni huyu Ndg.yetu Joel Bendera... Yupo mtaani na Corona iliyochoka sana yaani alipokuwa waziri ilikuwa vigumu kwa yeye kuipanda licha ya sasa anaiendesha... Na pia kumbuka anatakiwa kuhama kule kwenye kambi zao za REGENT na Mikocheni... Huoni Waziri akifanikiwa kurudi anastahili KUPONGEZWA!!! Nawasilisha...
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wenye kustahili kupongezwa ni wale wenye kurudi - kitu ambacho naamini ni fair maana ni kuwa kuna kitu labda wamefanya kuweza kustahili kurudi na hasa wale ambao wamedumu kwenye nafasi mbalimbali (kama waziri/naibu) kuanzia JK alipoingia madarakani. Lakini vipi kuhusu hilo wazo la kuzawadia matokeo kwa kutoa bonus ya nguvu na watu wakajua kuwa akimaliza miaka mitano na akiwa na matokeo yanayopimika na endelevu x,y anastahili bonus ya kiasi fulani (either fixed or a percentage of sort).. ?
   
 11. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mkuu, kwa sababu hata mimi nilipatwa na mshangao walipoapishwa wabunge, niliona wanafamilia na majirani huenda isitoshe na nyumba ndogo zikiwapongeza wahusika mpaka wakawa wanacheza kwenye viunga vya bunge! Nilishindwa kuelewa haraka haraka nini maana yake. Jibu umelitoa vizuri sana kwa ujumla wake ni kupongezana kwa kuwa waheshimiwa wanaingia kwenye maisha ya ukwasi na kujilimbikizia mali siyo kujenga nchi.
   
 12. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Wazo la Bonus ni zuri sana... Na litaleta changamoto mno... Ila angalizo wasimamizi wasiwe REDET,Synovate at al,bali taasisi huru kama Alexander Forbers au Delloitte wakishirikiana na wahariri wa magazeti makini hapa nchini itasaidia saaana kuwa fair...
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni sehemu ya utamaduni tuliojiwekea
   
 14. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sisi wananchi wa kawaida tutatoa pongezi vp???? Kama ni mama yangu bado analimia jembe la mkono pale kijijini ma hata mie ninapopata likizo huwa najumuika nae shamba kwa jembe hili hili ambalo tangu nimezaliwa nalitumia.

  Kwa swala la elimu bado hali ni mbaya sana. kwa sasa ni wenye fedha ndio wanapata elimu iliyo bora na wanaowapongeza ndo waitapata kutoka na marupurupu atakayopata ndg/jamaa yao ambae kwa sasa amaeukwaa uwaziri.

  maji bado ni issue nzito nyumbani. pale kijijini kuna mto ambao ndio unatusaidia na hata hivo upo kama 1.5km kutoka home. Niliwahi kupeleka pump ya maji lakini kwa sasa haitumiki baada ya bei ya mafuta kupanda so ni kutafuata kwa mguu kama zamani hakuna nafuu.

  Wadogo zangu bado wakitoka shule wanajisomea kwa kibatari as I did. Najua soon nao watanifuata katika swala zima la kuvaa miwani baada ya kuathiriwa na moshi wa kandili/kabatari. Umeme bado ni ndoto. Hakuna muokozi.

  Hao kwa sasa wana uhakika wa kuishi Mikocheni kwenye flats zao za bei mbaya lini watakumbuka taabu ninazozipata mimi.....na nina uhakika katika hali hii ndiyo tupo majority wa nchi hii.

  Pamoja na kupata elimu lakini bado mimi mwenyewe nalia na PAYE na makato kibao ninayokatwa kutoka kwenye kidogo ninachopata ilhali wao wakiwa na mishahara minono haikatwi kodi. Hii inaonyesha wao watakula bata kwa sana koz wana uwezo wa kupunguza mizinga kutoka kwa extended family members kwa kuwapa ajira hata ya kusafisha wizarani huku mimi mzigo mzima wa ndugu ukiniangalia na siwezi kuacha kuwasaidia.

  Kifupi sisi wananchi wa kawaida hatuwezi kuwapongeza koz hali yetu ya maisha bado ni mbaya.
   
 15. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hata kuan waliorudi hawa deserve congratulations za aina yoyote ile " can anybody tell me alichokifanya Makongoro mahanga till apongezwe???" Coming kwa Waziri wa Nishati na madini.....Kafanya nini??? Kama ni Gas power plant ya Ubungo ambayo 100MW ilikuwa initiated na Mkapa na the same project na ile inayojengwa Tegeta 50MW. So hakuna cha msingi alichokifanya zaidi ya kutegemea Hydro power plants za Nyerere ambazo zimeshachoka thus y kunakuwa na Power breakdown every now n then.

  Madini bado yanawanufaisha wawekezaji na funny enough yeye mwenyewe hajaliona hilo jana nimemuona kupitia taarifa ya habari ya ITV kuwa bado anataka kuatract wawekezaji katika sekta ya madini. Hapo hapo akatokea jamaa anaemiliki kiwanda cha chokaa TANGA ambae ameajiri Watanzania Vijana kama 250 hana pa kuuzia chokaa yake kwani Hata BARICK wananunua CHOKAA nje ya nchi....kwa nini apongezwe??? Nani hapa hakerwi na mgao wa UMEME?????????????
   
 16. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Ni akina nani hao ambao utendaji wao umekuridhisha? kwani kurudishwa kwenye uwaziri kwenye hii serikali ya JeyKey inamaanisha kuwa ulikuwa mtendaji bora? Mbona Sittta alikuwa Mtendaji Bora kwa kias fulani lakini akatemwa kwenye Uspika na ameenda kufukiwa kwenye uwaziri wq mambo ya East Africa. Hii nchi inaangalia ushkaji tu na siyo vinginevyo. Hata hao waliochaguliwa wenye majna mapya, tutakapoanza anza kuwapekenyua tutakuja kugundua kuwa wana mahusiano ya karibu na watu fulani fulani kama RA, EL hapo baadaye....Ukishangaa ya Firauni utaona ya Mussa....
   
 17. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  :embarrassed::redfaces::hungry::disapointed::Cry::embarassed2::sad:INAUDHI MNOOOO! KWA JINSI MAMBO YA HII NCHI YANAVYOENDESHWA NA HAWA WATU.....NAHISI KUJILIPUA KABISA!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 18. G

  Gwesepo Senior Member

  #18
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni jambo la kushangaza sana nami pia sioni logic,nilikuwa nikiwaza zaidi na zaidi chi yetu saizi imegubikwa na maafa, kila kona kuna mchezo mchafu,ukiangalia Miundo mbinu sifuri na Mh Kaahidi kujenga barabara kwa kiwango cha rami kila kona na hata za juu tayari huo ni mzigo kwa wizara hukika, Wizara ya Ardhi ndiyo usiseme tayari ni mzigo huo, Wizara ya Elimu ya juu ndiyo ipo likizo ,kila Wizara ina shida sasa swali linakuja hao mawazili na manaibu wazili wanapongezwa kwa lipi hasa na wengine wanaweka masherehe makubwa makubwa ni kwamba kazi wameisha maliza tayari ? au wana pongezwa kwa masirahi yao wenyewe? hapo lazima wananchi tuhoji na ni lazima tuwe wakweli ukimuuliza mwanachi yeyote hata Msomi kuwa chi yetu sasa hv inaelekea wapi hata kujibu lolote maana ni giza tupu huko tuendako,tukumbuke usemi wa Hayati Mwl Nyerere kwamba watanzania lazima tujihoji kuwa Tumetoka wapi,Tuko wapi na tunataka kwenda wapi,pls open your mind ikione waziri anapongezwa it can be a pay back kutoka kwa Mh lakini lazima aogopwe kama ukoma maana hatatufikisha pale tunapo taka kufika.
   
 19. L

  LAT JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa kufuata ushauri wangu wa kuunganisha kwenye mkongo wa taifa sasa status inapanda.... keep it up noti
   
 20. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Wapo waliofanya vizuri... (Mnyonge mnyongeni ilihali haki yake mpeni!!!) mfano;
  MAGUFULI- Boti za doria,kukaribia kutokomeza kama sio kumaliza uvuvi
  haramu wa Mabomu,Makokoro.

  MWANRI- kupeleka madaraka ya serikali katika Grassroots level (Serikali za mitaa kwa mafanikio makubwa!) Zahanati,Shule za Sekondari kila tarafa/Kata/Vijiji...

  PINDA- Kusimamia shughuli za bunge vizuri,kupambana na Mauaji ya Albino ambayo kwa sasa yamepungua. Hao ni baadhi tu.

  ...
   
Loading...