Kwanini "maridhiano" yanaitaja sana CHADEMA?

Neno maridhiano limeshika kasi kwa siku za hivi karibuni. Lakini mjadala upo zaidi kwa CHADEMA. Maswali niliyonayo ni nini kilitokea?

Chadema hawakushiriki uchaguzi, je watafanya maridhiano gani kama sio kuyafuata waliyohahitaji kabla ya uchaguzi?

Lakini kama maridhiano ni matokeo ya kilichotokea Octoba 2025, ni nani aliathirika? CHADEMA au wananchi? Je wananchi ni CHADEMA?

Moja ya point yangu ni kuwa kama tunaenda kwenye Maridhiano kwa kichotokea Oktoba kuna haja ya kuchukua watu ambao wana influence kwa wananchi lakini hawana ukaribu na chama cha siasa.

Lakini kama maridhiano ni ya kuingia kwenye uchaguzi bila CHADEMA basi ni kweli chadema ni wa kuangaliwa kwa uzuri. Hata hivyo kuona CHADEMA kama key katika hili ni kunasibisha na kilichotokea kuwa kilikuwa cha Chadema.

Naishia hapo.
Naona unaulizia ndevu kwa Osama.
CDM ndiyo chama kikuu cha upinzani na mtetezi mkuu wa wananchi wa Tanzania.

Bila kuishiriikisha CDM kwenye maridhiano hayo yatakuwa ni maigizo.
 
Nakwambia ukweli CHADEMA wangekubali kushiriki huo uchaguzi, hata haya maridhiano yasingeongelewa au hata kujadiliwa. Vyama vyote vilifyata mkia kwa CCM ni CHADEMA pekee yake waligoma. Kwa maana nyingine CHADEMA ndio denominator wa maridhiano. Maridhiano yoyote bila CHADEMA ni kujidanganya.
 
Neno maridhiano limeshika kasi kwa siku za hivi karibuni. Lakini mjadala upo zaidi kwa CHADEMA. Maswali niliyonayo ni nini kilitokea?

Chadema hawakushiriki uchaguzi, je watafanya maridhiano gani kama sio kuyafuata waliyohahitaji kabla ya uchaguzi?

Lakini kama maridhiano ni matokeo ya kilichotokea Octoba 2025, ni nani aliathirika? CHADEMA au wananchi? Je wananchi ni CHADEMA?

Moja ya point yangu ni kuwa kama tunaenda kwenye Maridhiano kwa kichotokea Oktoba kuna haja ya kuchukua watu ambao wana influence kwa wananchi lakini hawana ukaribu na chama cha siasa.

Lakini kama maridhiano ni ya kuingia kwenye uchaguzi bila CHADEMA basi ni kweli chadema ni wa kuangaliwa kwa uzuri. Hata hivyo kuona CHADEMA kama key katika hili ni kunasibisha na kilichotokea kuwa kilikuwa cha Chadema.

Naishia hapo.
Jana kwenye kikao cha Rais na Viongozi wa Vyama vya Siasa neno "Chadema" lilitajwa mara ngapi?
 
Chadema sio chama chadema ni mioyo ya watu wengi wapenda haki ndio maana maridhiano bila chadema ktk wingi wa watu inaonekana km kiini macho
 
Mnajidanganya tuu mbona Jana Rais wa JMT hajasema hayo? Na Maridhiano yanaanza mara moja.
Kwani umewahi kuisikia CHADEMA ikisema inataka maridhiano na wauaji wa Oct 29? Kwanza kufanya maridhiano huku wakiiweka pembeni CHADEMA, litakuwa jambo la heri. Kufanya maridhiano na wauaji ni kujitia unajisi, ni kubariki ushetani wa Oct 29. CHADEMA isimame na wananchi wanaoendelea kuomboleza, huku miili ya wapendwa wao ikiwa imetupwa kusikojulikana. CHADEMA isimame na wananchi kutaka uwajibikaji kwa wahusika wote wa mauaji na utekaji.
 
Watakoma watabakia hivyo hivyo miaka yotee! Maridhiano soon yanaanza kuna vyama 18.
 
Hayo makundi mengine ukiacha cdm hawako tayari kulipa gharama ya kupata mabadiliko. Cdm ndio wamesimama kidete kwa zaidi ya miaka 15 wakitaka mabadiliko, kwa jasho na damu. Nyie makundi mengine jitajeni tuone msukumo wenye kwenye kupata mabadiliko.
Hayo Makundi mengine yangekuwa na misimamo kama ya Chadema na kuunganisha nguvu hii nchi ingeshakombolewa kitambo sana. Na Kuna watu wangekuwa kwenye kilio na kusaga meno
 
Watakoma watabakia hivyo hivyo miaka yotee! Maridhiano soon yanaanza kuna vyama 18.
Hata kwenye uchaguzi ilisemwa hivyo hivyo kuwa kuna vyama 18, ila sasa hivi tunazungumza kuhusu maridhiano kwa kilichotokea kwenye huo uchaguzi.
 
ndicho chama kikuu kinachopendwa sana na wengi..imani na matumaini ya wengi ipo na chadema.

kina nguvu ya umma kupendwa na umma.
 
Back
Top Bottom