Membe, Zitto wapanguliwa hoja mradi wa gesi Kusini kwa mikwaju 7 Kafulila

MKINGUZI

Member
Apr 17, 2015
40
85
Na David KAFULILA
2Sept.2020

Natofautiana na Zitto, Membe mradi wa gesi kusini wa $30bn. Sera zao kuhusu uwekezaji ni kuuza nchi!

#Kumekuwapo na mjadala mkubwa kuhusu kulikoni uchumi wa gesi nchini. Labda niseme tu kwamba kwa kiasi kikubwa kilichobeba agenda ya uchumi wa gesi ni mradi wa kusindika gesi mkoani Lindi, mradi wenye thamani ya dola billioni30. Uwekezaji ambao unatarajiwa kufanywa na kampuni za Shell, StateOil& Orphir.

#Nimeona mjadala huu imekuwa Agenda ya mgombea urais Bernard Membe na ikichagizwa kwa ukali jana kwenye uzinduzi wa kampeni za ACT Mkoani Lindi na Kiongozi wake Mkuu, Ndugu Zitto Kabwe, wakikosoa Uongozi wa JPM kuwa msingi wa kuchelewa kuanza kwa uwekezaji wa mradi huu.

# Pengine ndio sababu nimeona nivute kalamu kuchangia maoni yangu katika hili. Hili naomba niseme mambo saba , naamini yatanitosha kueleweka;

1.Mradi wa Dola billioni30 ni uwekezaji mkubwa kuliko uwekezaji wowote sio tu ndani ya Tanzania bali Afrika mashariki yote.

# Dola billioni 30 ni karibu nusu ya uchumi wa Tanzania au sawa na uchumi wa Uganda na mara mbili ya uchumi wa Rwanda. Hivyo ni mradi unahitaji umakini mkubwa kufikia makubaliano.

2. Ingawa ni ukweli kwamba hamasa ya mradi huu ilikuwepo tangu miaka ya 2013, lakini ni awamu hii ya tano ndani ya miezi miwili ya kwanza, Januari2016, iliyochukua hatua muhimu kama kukabidhi ardhi kwajili ya mradi kutekelezwa, suala ambalo hapo kabla kulikuwa na michezo ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa waliokamata ardhi hiyo kutegea fidia ya mabillioni....na hivyo kuzidi kuchelewesha hatua za makubaliano. Kuelewa hili, soma gazeti la east Afrika kwenye link hii..
https://allafrica.com/stories/201601180824.html

3. Ingawa mjadala wa mradi huu ulikuwepo tangu 2013, lakn ni awamu hii mwaka 2017 iliyotengeneza mwanzo wa majadiliano kimkakati ( structured and strategic discussion) kwa maana ya kuunda timu ya wataalamu ya mashauriano ya Serikali( Government Negotiation Team) ambayo ndio inapelekea hatua ya makubaliano kati ya Serikali na wawekezaji( Host Government Agreement-HGA).

#Hili limefanyika awamu hii mwaka 2017. Kuelewa zaidi soma link hii...
Government prepares new terms for talks on LNG project

# Kuanza kwa kusema hayo nimetaka ieleweke kwamba ni walau awamu hii inayolalamikiwa na ndugu zetu Zitto na Membe kuwa imechelewesha wakati ndio iliweza kuchukua hatua muhimu na kuonesha utashi kutaka uwekezaji huu.

4. Zitto na Membe wanalalamika kwamba mradi huu umecheleweshwa na utawala wa JPM, lakini ninatamani kujua umecheleweshwa kulinganisha na wapi? Maana nchi Kongwe, yenye gesi zaidi yetu, utalaamu na uzoefu zaidi yetu katika masuala ga gesi, ilifikia uamuzi kuruhusu uwekezaji ( Investment Decision) Novemba 2018, baada ya miaka7 ya majadiliano. Kulikoni Tanzania iliyoanza majadiliano mwaka 2017 uone ni kuchelewa?

#Kujua kama Canada iliwachukua miaka7 kufikia makubaliano ya uwekezaji mradi wa dola billioni 31 eneo la Kitimat soma mahojiano kati ya gazeti la Citizen la kwenye link...
Tanzania: Canada Offers Lessons On LNG Project for Tanzania

5.Hoja kwamba Msumbiji imefanikisha kusaini mikataba na kuanza uwekezaji kabla ya Tanzania sio msingi wa kumuhukumu JPM kwasababu mbili;

# Kwanza ni ukweli kwamba Msumbiji wana gesi nyingi kuliko Tanzania na zaidi gesi yao asilimia 85% ipo kina kifupi(shallow water) hivyo gharama ya kuwekeza ni kidogo kulinganisha na Tanzania ambayo zaidi ya asilimia 90% ya gesi ipo kina kirefu( deep sea)..kuelewa kuhusu gharama angalia chart kwenye link..
Drilling Cost - an overview | ScienceDirect Topics

# Kwa ufupi ni kwamba gharama ya kuchimba kisima kwenye kina kifupi cha bahari ni kati ya dola milioni 50 mpaka dola milioni 70 kulinganisha na wastani wa gharama za kuchimba kisima kwenye kina kirefu cha bahari ambayo ni kati ya dola milioni 100 mpaka milioni 120.( Goursshety 2015).

#Hili nimeliweka kusisitiza kwamba sio sahihi kulinganisha Tanzania na Msumbiji katika mazingira hayo.

#Ndio maana tathimini ya kampuni maarufu ya kimataifa ya WOOD MACKENZIE inataja kuwa bei ya gesi ya chini kabisa inayoweza kuleta faida kwa mradi wa LNG wa Tanzania( break even price) ni dola 9/mmBtu..kulinganisha na dola7/mmBtu Msumbiji kwa 1mmbtu( sawa na mita za ujazo 28.2)..kuelewa hili, soma link hii...
Tanzania’s LNG hopes on a knife-edge

# Katika mazingira ambayo bei ya gesi duniani imeanguka tangu miaka ya 2014, na wawekezaji ni walewale ni wazi kwamba wanaweza kuanza Msumbiji kabla ya Tanzania moja ya sababu ni unafuu wa gharama ya uwekezaji.

# Kujua bei ya gesi ilivyoporomoka tangu mwaka 2014, soma link hii...
Natural Gas Prices - Historical Chart

6.Sababu nyingine na muhimu kabisa ni aina ya Rais wa Tanzania kwasasa ukilinganisha na viongozi wengi wa bara la Afrika. JPM anaamini katika kile wazalendo wengi wa Afrika wamekiamini na kuendelea kuamini kwamba nchi zetu zinaporwa rasilimali kupitia mikataba mibovu.

# Sina hakika kama Msumbiji wana msimamo thabiti kuhusu uvunaji rasilimali hii kwani kuna kelele za kutosha kuhusu ufisadi sekta hii Msumbiji.

# Ukisoma uchambuzi kwenye tovuti ya www.petroleum-economist uchambuzi wenye kichwa Tanzania LNG Hopes on a knife edge......wanaeleza wazi kwamba kinachosumbua Tanzania ni namna Rais JPM anavyotaka uhakika wa maslahi ya nchi yake kwenye makubaliano hayo

#Nikinukuu sehemu ya makala hiyo inasema " Disagreements over terms have stymied progress .Magufuli remains keen to maximize government revenues and domestic offtake ,while IOCs have been seeking terms to make Tanzania LNG more competitive with rival supply and to put the project finances on a stable footing"

7.Watanzania tulilaumu viongozi wetu waliopata kusaini mikataba mibovu huko nyuma. Zitto na Membe wao wanapambana nchi isaini tu bila kujali maslahi mapana ya Taifa hili leo na kesho.

# Tazama nchi kama Canada, walikuwa na miradi takribani 20 ya namna hii lakn walijadiliana kwa takribani miaka7 na kampuni hizi na wakaishia kusaini mradi mmoja tu na mingine19 wakakubaliana kutokubaliana ikaachwa. Sababu ? Canada waliona maslahi waliyoyataka hayafikiwi..kuelewa hili, soma mahojiano haya tena link hii ya Gazeti la CITIZEN
LNG project on the right track: director

# Nachosisitiza ni kwamba sio lazma JPM akubali tu kwasababu Msumbiji wamekubali. Hatupaswi kuingia soko la mabeberu kushindana kuuza nchi yetu. Hatuwezi kuuza nchi yetu sababu kuna nchi zinajiuza.No!

8. Tukumbushane kauli ya Mwalimu Nyerere , kwamba madini yetu hayaozi. Naamini pia gesi yetu Lindi haiozi..JPM hafanyi maamuzi kwasababu ya uchaguzi ujao bali kizazi kijacho.Tanzania haitokuwa ya kwanza kuahirisha uwekezaji wa kusindika gesi. Kama Canada walikosa maslahi yao kwenye mikataba 19 wakahirisha. Ni akili mbovu sana kwa Viongozi kufikiri lazma tuingie mkataba wa kuvuna gesi ya Lindi awamu hiihii au kizazi hikihiki hata kama masharti ni yasawa na kuuza nchi
 
INAKUAJE UKOSE MASLAHI KAMA SUALA HILI UNALIFANYA LA KITAIFA NA KUWASHIRIKISHA WADAU WENGINE ?

WAPINZANI NI SEHEMU MUHIMU YA TAIFA NA WSHAURIWAZURI TUU KWENYE MAMBO MBALI MBALI

Pale Raisi anapojiona yeye na timu yake ndio peke yao wenye akili na maamuzi bora ,hapo ndipo tunapokwama.

Ipo nja ya kujipatia maslahi kwenye rasilimali etu , kama CCm wameshindwa ,mundhani ndio na wengine watashindwa kufikiri kama nyinyi?

Huo ni Ukiritimba kama ule wa Mwalimu.

Alipo mzee mwinyi akafungua milango na nchiikafunguka, na Mkapa akja akaendeleza ,mpaka Nyerere akajiona Pimbi pale serikali ilipouza mashirika yake yote na kushughuika na kukusanya kodi tuu.
tazamaleo tulipofika.
 
Ulishaambiwa wapinzani wao ni watu wa kupinga tu..hawajawahi kuunga mkono hoja yoyote hata bungeni..kuwashirikisha ni sawa na kuchukua kiroba cha sukari na kwenda kumwaga baharini ukitegemea maji ya sukari.
 
Yote hayo yanafanyika chini ya utawala wa serikali ya CCM na kila siku CCM wanakuja na Ngonjera za kila aina ya sababu za kwa nini hiki hakiwezekani au la ... adui yaetu watanzania si mwingine, ni CCM kungangania kubaki madarakani kwa miaka 59 na bado wanataka tu kuendelea kubaki... yafaa sawa kuwepo na ukomo wa vyama kukaa madarakani kama ilivyo kwa Uraisi...
 
INAKUAJE UKOSE MASLAHI KAMA SUALA HILI UNALIFANYA LA KITAIFA NA KUWASHIRIKISHA WADAU WENGINE ?
WAPINZANI NI SEHEMU MUHIMU YA TAIFA NA WSHAURIWAZURI TUU KWENYE MAMBO MBALI MBALI
Pale Raisi anapojiona yeye na timu yake ndio peke yao wenye akili na maamuzi bora ,hapo ndipo tunapokwama.
Ipo nja ya kujipatia maslahi kwenye rasilimali etu , kama CCm wameshindwa ,mundhani ndio na wengine watashindwa kufikiri kama nyinyi?
Huo ni Ukiritimba kama ule wa Mwalimu.
Alipo mzee mwinyi akafungua milango na nchiikafunguka, na Mkapa akja akaendeleza ,mpaka Nyerere akajiona Pimbi pale serikali ilipouza mashirika yake yote na kushughuika na kukusanya kodi tuu.
tazamaleo tulipofika.
Mbona wapinzani haohao kwanza walilaumu mikataba ya awali kwamba nchi inadhulumiwa. Baadaye wakalaumu kuvunjwa mikataba waliyoiita ya kihuni na kuwatetea wanaotudhulumu madini.

Akili ya mbu kama hii italisaidia taifa kweli?
 
Sio kila mlevi anashiriki,kuna watu watafanya kwa niaba yetu,wenye uchungu na ni wazalendo kwa taifa hili
 
INAKUAJE UKOSE MASLAHI KAMA SUALA HILI UNALIFANYA LA KITAIFA NA KUWASHIRIKISHA WADAU WENGINE ?
WAPINZANI NI SEHEMU MUHIMU YA TAIFA NA WSHAURIWAZURI TUU KWENYE MAMBO MBALI MBALI
Pale Raisi anapojiona yeye na timu yake ndio peke yao wenye akili na maamuzi bora ,hapo ndipo tunapokwama.
Ipo nja ya kujipatia maslahi kwenye rasilimali etu , kama CCm wameshindwa ,mundhani ndio na wengine watashindwa kufikiri kama nyinyi?
Huo ni Ukiritimba kama ule wa Mwalimu.
Alipo mzee mwinyi akafungua milango na nchiikafunguka, na Mkapa akja akaendeleza ,mpaka Nyerere akajiona Pimbi pale serikali ilipouza mashirika yake yote na kushughuika na kukusanya kodi tuu.
tazamaleo tulipofika.
Wapinzani gani? Hawa wa Tanzania? Hujanishawishi bado. Hawa ni sawa na mbwa wa maskini akipewa chakula anakula na akiina mavi mavi anakula. Hajui kizuri ni kipi na kibaya ni kipi. Lisu anachojua ni kulaumu hata kama anatibiwa mhimbili.
 
Hopeless arguments.

Uzalendo siyo kuifanya tu serikali ipate share kubwa lakini pia ni pamoja na kuwa logical and realistic.

Tanzania ilikuwa na advantage over Mozambique. Maana ugunduzi mkubwa ulifanyika Tanzania kabla ya Mozambique.

Mikataba ya mafuta na gas inafahamika. Gas, mafuta na madini vipo katika mataifa mengi. Unapotengeneza mikataba unaitazama dunia ili uishi katika uhalisia. Ukiweka masharti magumu kupindukia, utakimbiwa (kama ilivyotokea kwa Tanzania), na ukijishusha kupita kiasi unaweza kuambulia faida ndogo.

Ni sawa na mtu aliye na duka. Huenda ungependa uuze sukari kilo 1 kwa shilingi 10,000 ili upate faida kubwa kwa kila kilo. Kama wastani wa bei ni sh 2,800, ukiwa mjinga ukaamua kuuza kilo 1 ya sukari kwa sh 10,000 kwa mategemeo ya kupata faida kubwa, utaishia kukosa kabisa au kupata faida kidogo kuliko anayeishi kilo 1 kwa sh 2,750.

Tanzania kwa kuweka masharti magumu nje ya uhalisia, hatutapata chochote. Upeo wa watoa maamuzi umekuwa duni wakiamini kuwa siku zote kupata faida kunategemea zaidi kodi kubwa. Leo wanahaha kuwarudisha wawekezaji wa gas waliondoka, na wawekezaji hao wamesema wazi kuwa hawatarudi kuwekeza Tanzania, labda mpaka baada ya miaka 5, kwa sababu pesa waliyopanga kuwekeza Tanzania, tayari wamewekeza Mozambique. Kutokana na ujinga wetu, tumekosa uwekezaji kwenye gas yetu, tumebaki kukenua meno kufurahia uwekezaji wa mafuta nchini Uganda eti tutafaidika na bomba la gas kupita nchini mwetu!

Ugumu wa kuwekeza Tanzania, ndio uliowakimbiza wawekezaji wa sejta ya gas Tanzania. Wawekezaji wakaamua kuongeza juhudi kubwa za utafiti kwa upande wa Mozambique. Kwa vile tunachangia aquifer, sasa wanaweza kupata gas nyingi kwa kutokea Mozambique. Wamepata gas nyingi kwenye bonde la mto Ruvuma kwa kupitoa upande wa Msumbiji.

Mwishowe kitakachotokea ni kuwa na mgogoro na Msumbiji, sawa na ilivyokuwa kati ya Kuwait na Iraq. Visima vitajipanga mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, na gas kuvunwa kupitia upande wa Mozambique.

Hoja za Kafulila ni za kutengenezwa. Makampuni ya gas Tanzania hayakuondoka kwa sababu ya uaghali wa uchimbaji bali ni kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya uwekezaji kwa upande wa Tanzania.

Mazingira magumu ya uwekezaji kwa Tanzania hayajawa kwa sekta ya gas na madini tu bali ni kwa sekta zote. Hiyo ndiyo sababu ya wawekezaji wengi wa ndani na nje ya Tanzania, ambao mwanzo walikuwepo Tanzania, kuamua kwenda kuwekeza zaidi nje ya Tanzania. Na huko nje wanafurahia mafanikio ya uwekezaji wao. Na leo ni vigumu sana kuwarudisha.

Uchumi ni sayansi, siyo ubabe au amri. Ubabe na amri, unawezankuifanyia familia yako (japo siyo sahihi) lakini huwezi kumfanyia mtu ambaye ana uamuzi wake, wa kufanya au kuacha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ana mikwaju mbona kashindwa kushawishi wajumbe, kafulila ni wa kupuuzwa.
 
kama ana mikwaju mbona kashindwa kushawishi wajumbe, kafulila ni wa kupuuzwa.
Usihamishe magoli, huwa mnasema serikali imesaini mikataba ya kihuni, serikali imeruhusu rasilimali zetu kuibiwa, serikali imesaini mikataba ya dharura, leo watu wanashauriana mnaleta porojo. Hamueleweki...
 
INAKUAJE UKOSE MASLAHI KAMA SUALA HILI UNALIFANYA LA KITAIFA NA KUWASHIRIKISHA WADAU WENGINE ?
WAPINZANI NI SEHEMU MUHIMU YA TAIFA NA WSHAURIWAZURI TUU KWENYE MAMBO MBALI MBALI
Pale Raisi anapojiona yeye na timu yake ndio peke yao wenye akili na maamuzi bora ,hapo ndipo tunapokwama.
Ipo nja ya kujipatia maslahi kwenye rasilimali etu , kama CCm wameshindwa ,mundhani ndio na wengine watashindwa kufikiri kama nyinyi?
Huo ni Ukiritimba kama ule wa Mwalimu.
Alipo mzee mwinyi akafungua milango na nchiikafunguka, na Mkapa akja akaendeleza ,mpaka Nyerere akajiona Pimbi pale serikali ilipouza mashirika yake yote na kushughuika na kukusanya kodi tuu.
tazamaleo tulipofika.
Unahitaji kwenda shule. Na sio kila kiu uchangie mengine sio saizi yako.
 
Ulishaambiwa wapinzani wao ni watu wa kupinga tu..hawajawahi kuunga mkono hoja yoyote hata bungeni..kuwashirikisha ni sawa na kuchukua kiroba cha sukari na kwenda kumwaga baharini ukitegemea maji ya sukari.
Woga, uwezo mdogo wa kujenga hoja.
 
Mbona wapinzani haohao kwanza walilaumu mikataba ya awali kwamba nchi inadhulumiwa. Baadaye wakalaumu kuvunjwa mikataba waliyoiita ya kihuni na kuwatetea wanaotudhulumu madini.

Akili ya mbu kama hii italisaidia taifa kweli?
Tatizo CCM wanfanya maamuzi peke yao, ndio maana hatuachi kuwatuhumu,na yanapotokea mapungufu lazima lawama wabebe peke yao,
Ila kwa Taifa kubwa kama hili ni lazima uwashirikishe wadau ,jambo ambalo ccm hawafanyi.
Wanawachukulia wapinzani kama maadui na si washauri hapa ndio tunapo kwenda kombo kama taifa
 
INAKUAJE UKOSE MASLAHI KAMA SUALA HILI UNALIFANYA LA KITAIFA NA KUWASHIRIKISHA WADAU WENGINE ?
WAPINZANI NI SEHEMU MUHIMU YA TAIFA NA WSHAURIWAZURI TUU KWENYE MAMBO MBALI MBALI
Pale Raisi anapojiona yeye na timu yake ndio peke yao wenye akili na maamuzi bora ,hapo ndipo tunapokwama.
Ipo nja ya kujipatia maslahi kwenye rasilimali etu , kama CCm wameshindwa ,mundhani ndio na wengine watashindwa kufikiri kama nyinyi?
Huo ni Ukiritimba kama ule wa Mwalimu.
Alipo mzee mwinyi akafungua milango na nchiikafunguka, na Mkapa akja akaendeleza ,mpaka Nyerere akajiona Pimbi pale serikali ilipouza mashirika yake yote na kushughuika na kukusanya kodi tuu.
tazamaleo tulipofika.
Kwa ukanjanja wako ulitaka jpm asaini harakaharaka , halafu iwekiki kwenu, kwamba inchi inauzwaa kwa mabeberu, hovyo kabisaa

VIVA JPM.
 
Back
Top Bottom