Author
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 1,745
- 8,230
Nimekuwa naangalia msafara na shughuli ya kumuaga Hayati John Pombe Joseph Magufuli tangu Dar es Salaam mpaka leo Dodoma kila sehemu naona mama Janeth analia kwa uchungu sana. Lakini watu wanavyolia wanamuongezea uchungu kwa maeneo yote mwili unapoagwa.
Msiba umefika viwanja vya Dar na watu wengi wameupokea kwa vilio huku mama Janeth akiendelea kupata uchungu na kuanza kulia upya. Leo Dodoma hali ni hiyo hiyo. Namuonea huruma sana na naona anachoka sana.
Ingekuwa amri yangu ningemwomba abaki Chato asubiri msiba. Maeneo ya viwanjani tunamuona analia. Sijajua kwenye misafara na vilio vya watu njiani vinamuongezea uchungu kiasi gani.
Hapo bado Zanzibar, Mwanza na Geita. Tangu March 17 (labda kabla ya hapo). Mama Janeth atakuwa analia tu.
Imetosha sasa tumpumzishe JPM...na Mama Janeth apumzike