Kwanini Malkia Elizabeth hamiliki Paspoti ya kusafiria?

Kwanini Malkia Elizabeth hamiliki Paspoti ya kusafiria?

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,712
When travelling overseas, The Queen does not require a British passport. As a British passport is issued in the name of Her Majesty, it is unnecessary for The Queen to possess one. All other members of the Royal Family, including The Duke of Edinburgh and The Prince of Wales, have passports.

Kwanini yeye tu, mbona hata Marais wa mataifa yenye nguvu Duniani kama US, RUSSIA, CHINA na nyingine wana papspoti?

Je, kuna kiongozi mwingine, ambaye ana hii privilege? Ina maana ana kitu gani cha ajabu??
 
Hivi passport ni nini? Ni kitambulisho. Kitambulisho ni nini? Ni document yenye taarifa za msingi za mhusika. Kama mhusika taarifa zake za msingi zinajulikana popote duniani ana haja gani kubeba document yenye taarifa hizo hizo zinazojulikana popote? Nonesense! That's why Her Majesty or His Holiness does not need to carry id cards.
 
Its funny that jibu lako lipo kwenye hayo maandishi ya kiingereza na bado unatuuliza

Okay hana passport wala leseni sababu hivyo vitu viwili vipo chini ya majina yake, wakaona haina haja yeye kumiliki.
Swala la kuwa kwa jina lake sio shhida ila anasafiri nchi nyingine kwa kibali gani kwenda nchi nyingine?
 
Utawala wa kifalme (monarchy) ni wa maisha i.e. hadi kifo, tofauti na utawala wa kidemokrasia ambapo mtu hupewa dhamana kwa kipindi fulani.

Mf: Obama sasa hv ni raia wa kawaida kisheria, nikimaanisha kabla na baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi wa umma kama raisi yeye ni mwananchi na raia kama raia mwingine ila malkia/mfalme yeye ukomo wake ni pale mauti yanapomkuta.
 
Umejibu vizuri sana mkuu.

Swali la jamaa lilikuwa linahitaji jibu kama hili, ila JF siku hizi kumeibuka muchknows ambao badala ya kukujibu swali wanakunanga.
 
Umejibu vizuri sana mkuu.

Swali la jamaa lilikuwa linahitaji jibu kama hili, ila JF siku hizi kumeibuka muchknows ambao badala ya kukujibu swali wanakunanga.
Thanks Chief.

Nadhani muuliza swali alipotea kidogo tuu kuelewa hivyo alihitaji kufahamishwa au kuoneshwa tofauti za kiutwala ambazo hazikuwa direct ktk article aliyoinukuu.

Na nimetoa maelezo mafupi tuu ili nisimchanganye ila naamini kuna points za ziada sijaziweka na taratibu akifuatilia atapata elimu zaidi
 
Thanks Chief.
Nadhani muuliza swali alipotea kidogo tuu kuelewa hivyo alihitaji kufahamishwa au kuoneshwa tofauti za kiutwala ambazo hazikuwa direct ktk article aliyoinukuu.
Na nimetoa maelezo mafupi tuu ili nisimchanganye ila naamini kuna points za ziada sijziweka na taratibu akifuatilia atapata elimu zaidi

Namna uliyotumia kumjibu ni namna walau sahihi ya kumwelewesha mtu.

Imagine, kwenye post yake kuna mahali panasema, "As a British passport is issued in the name of Her Majesty, it is unnecessary for The Queen to possess one."

Mimi pia nimeelewa, na ningependa kuongeza maswali, tuna nchi kama Saudi Arabia ambazo ziko chini ya tawala za kifalme, utaratibu wao ukoje kuhusu passports? Kama passports zao zinakuwa in the names of Kings, hao Kings nao hawamiliki passports?
 
Back
Top Bottom