Kwanini maisha ni Ubatili?

Angalia tu ile ajali ya ndege ,ndoto nyingi zimepotea ,yaani ujujua mwingi binadamu ila hajui hata sekunde moja mbele atakuwa wapi.

Honestly ,mimi tangu nitambue sina mipango ya muda mrefu japo nina mafanikio sijawahi kuhofia mbele sana ila najua nitakufa .
 
Ili uchelewe kukufa
Ila mwisho wa yote utakufa tu,nini maana ya kuhangaika au kuhofia kifo ambacho hujui kitakukutia wapi na saa ngapi.

Mwaka 2018 nilikua namuuguza jamaa yangu wa karibu,usiku mmoja alikuja mgonjwa yuko mahututi sana. Madaktari na wataalamu mbalimbali wa afya walijitahidi mpaka yule jamaa akawa sana kabisa mpaka inafika asubuhi.
Kuliookucha jamaa alikua fit kiasi ukilinganisha na hali aliyokua nayo,basi jamaa aliamka pale akaenda toilet,akanywa uji,n.k na kuanza kutupigisha story mle wodini. Zaidi alimshukuru sana Mungu kwa kumuepusha na umati kwasababu bado ana mipango mingi na tegemezi wengi sana.

Tulipiga story kama nusu saa hivi,jamaa akarudi zake kulala hapo kitanda. Na alipolala hakuamka tena ikawa ndio bye! bye! (R.I.P).

So unaona jinsi maisha yanavyopoteza maana.
 
YESU alikuwa na mambo ya chini chini sana ila chakula chake kikuu ilikuwa samaki na mikate na divai mara moja moja. Yumkini ameacha mali nyibgi sana ambazo ndugu zake hawana taarifa nazo
Yule mwanamke kisimani hajamuachia watoto kweli? Au Mariam Magdalena, usikute kuna ambayo tulifichwa.
 

Duu, it's sad story, but alikufa kifo kizuri sana. Alikufa huku anaongea na bila kuwasumbua watu wake kumuuguza
 
Unapambana na kujinyima ili kujenga kitegauchumi chako baada ya kuzeeka na kufariki watoto wanakiuzilia mbali na kutumia pesa yote kwenye starehe:
Ukiwa duniani mche Mungu na tafuta mali ili ikuwezeshe kuishi maisha yako wewe mwenyewe ukiwa hapa duniani:

Watoto haki yao ni kuwapa elimu tu, ili iwawezeshe kujitegemea kama ilivyo kwako:
 
Hatari Sana ndugu😁..wanadai Kuna peponi ambako hakuna dhiki Wala njaa,na ili ufike Kuna sheria tena wamekupangia na kukuwekea usimamizi wa sheikh & padri.ushenzi mtupu😓
 
Ni kweli maisha haya ni ubatili mtupu kwa mtu asiye na Kristo Yesu moyoni mwake. Wenye Yesu mioyoni mwao wana kitu kinachoitwa AHADI YA UZIMA WA SASA NA ULE UTAKAOFUNULIWA BAADAE.
Kila nikifikiria ubatili wa maisha haya,ndipo nazidi kumshukuru Yesu kwa kuja.

Ndio maana siku zote namwomba anisaidie niyafanye mapenzi yake kwa muda alionipa wa kukaa hapa duniani nikijua kwamba Mimi ni mvuke tu!
 
Ni kweli kwamba kwenye hicho kitabu kuna ahadi ya mabikra 72 peponi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…