Kwanini mabaya ya marehemu hayasemwi hata kama akiuawa kwenye tukio la uhalifu?

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Mtu kafa kwenye fumanizi, au kauliwa na wananchi wenye hasira kali alipokiwa akivunja nyumba, lakini atapambwa huyo, na hutousikia uovu wake.
Why?????
 
Mtu akishakufa kinachobaki ni kumwombea ili apate pumziko la milele huko aendako!

Mabaya yake ataenda kuyakuta mbele ya safari, hata ukiyasema wakati ashakufa itasaidia nini?
 
Mtu akishakufa kinachobaki ni kumwombea ili apate pumziko la milele huko aendako!

Mabaya yake ataenda kuyakuta mbele ya safari, hata ukiyasema wakati ashakufa itasaidia nini?

Inasemekana yanasemwa mazuri tu ili jamii iliyo baki ijifunze.
Lakini,si na mabaya nayo yangesemwa ili kuiasa jamii?
 
Mtu akishakufa kinachobaki ni kumwombea ili apate pumziko la milele huko aendako!

Mabaya yake ataenda kuyakuta mbele ya safari, hata ukiyasema wakati ashakufa itasaidia nini?
na kwanini basi tusimzike kimya kimya ili kama ni mwema au mbaya ikajulikane mbele ya safari,huo uzuri unaozungumzwa na kuacha ubaya unasaidia nini ?
 
lakini tungekuwa tunasema ukweli daima naamini ukimwi ungeisha maana wanaokufa kwa ukimwi hutajwa kufa kwa magonjwa tofauti kwenye historia zao.
Sio kweli! Aliyekufa kwa ukimwi huwa anajulikana hata kama kwenye historia ya marehem watasema amekufa kwa TB! Kitakachofanya ukimwi uishe ni watu kuamua kurudi kwenye maadili au UTU wao na sio historia ya marehemu!
 
amini hii miaka ya mwanzo imewapoteza watu wengi sana hasa pale marehemu alipoacha mke mzuri sana.
 
watu8 kwanza sijasema place nmesewa plane (ukiweza goole 'seven body' na 'seven plane' itakusaidia kuelewa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom