Kwanini local channels za Tanzania hazioneshwi kwenye visimbuzi vyote?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Wadau, poleni kwa msiba wa aliyekuwa Amiri Jeshi na Rais wa JMT, John Magufuli.

Hili swala linanishangaza na ningependa kujua TCRA na sheria zao wanasemaje. Local channels za vituo vya televisheni nchini kwa mujibu wa sheria zinaonyeshws bure.

Kimantiki nilitegemea channels za ITV, UTV, Capital TV, EATV, Clouds, TBC1, Star Tv, Channel Ten na nyingine zote ambazo ni local (hazilipiwi), zingeonyeshwa ktk visimbuzi vyote kuanzia TING, Azam, DSTV, Digitek, Star Times na Continental. Lakini ajabu ni kuwa baadhi ya vituo havionyeshi channels zote. Mfano, UTV haipatikani kwenye kisimbuzi cha Star Times.

Kanuni na sheria za kurusha matangazo ya local channels inasemaje? Nadhani sio haki kutunyima walaji haki ya kuangalia local channels kwenye visimbuzi vyote.

Vv
 
UTV ni channel ya Azam haiwezi kuwekwa katik king'amuz kingine mfano sinema zetu na Swahili channel.
Hiyo ni local channel, ni ya bure kwa hiyo ingefaa mwenye kisimbuzi chochote aione bure. Kwenye kisimbuzi cha Digitek UTV haionyeshwi?

Vv
 
Yaani nitumie mabilioni kuwekeza kwenye televisheni ili wewe uangalie bure. Embu kua serious Mkuu.
Hiyo sio hoja yangu, wewe umejibu kijumlajumla, kuna local channels na channels za kulipia, ndo maana hata usipolipia ada ya mwezi, local channels zote hazifungwi.

Vv
 
Unazungumzia channel kutoka makampuni tofauti hii haitawezekana free to air utaipata kutoka TBC tuu .
 
Hiyo ni local channel, ni ya bure kwa hiyo ingefaa mwenye kisimbuzi chochote aione bure. Kwenye kisimbuzi cha Digitek UTV haionyeshwi?

Vv
Nani kakuambie ni local chanel???

kuonyeshwa au kuona hyo chanel baada ya kifurushi kuisha sio sifa ya kuiita local chanel.

rudi ukasoma mwongozo wa tcra

utv sio local chanel na haiko kwenye list ya local chanel za tz
 
Kila media yenye king'amuzi anachofanya ni kuhitaji mapato ili aweze kuendesha kituo chake, vinginevyo wataanza kupunguza staff alafu mje muanzishe uzi wa utetezi hapa.

Mkitaka free to air nunua dish lako la ukubwa wa kati na kung'amuzi/decoder yenye uwezo mkubwa kufikia dvb s2x +t4 na kiwe FHD 1080p/h.265 10/12bitt ukifunga hiyo kitu utazipata zote za bongo na nje ya bongo.
 
Wadau, poleni kwa msiba wa aliyekuwa Amiri Jeshi na Rais wa JMT, John Magufuli.

Hili swala linanishangaza na ningependa kujua TCRA na sheria zao wanasemaje. Local channels za vituo vya televisheni nchini kwa mujibu wa sheria zinaonyeshws bure.

Kimantiki nilitegemea channels za ITV, UTV, Capital TV, EATV, Clouds, TBC1, Star Tv, Channel Ten na nyingine zote ambazo ni local (hazilipiwi), zingeonyeshwa ktk visimbuzi vyote kuanzia TING, Azam, DSTV, Digitek, Star Times na Continental. Lakini ajabu ni kuwa baadhi ya vituo havionyeshi channels zote. Mfano, UTV haipatikani kwenye kisimbuzi cha Star Times.

Kanuni na sheria za kurusha matangazo ya local channels inasemaje? Nadhani sio haki kutunyima walaji haki ya kuangalia local channels kwenye visimbuzi vyote.

Vv

Ilitungwa sheria ili kuipa nafasi TBC kuangaliwa na kila mtu kwa lazima. Mama kupitia Nape amesha fungua anga, soon zitaanza kurushwa.
 
Back
Top Bottom