Uhuni wa Startimes udhibitiwe

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Sheria inawataka warusha maudhui wa televisheni kuonyesha bila malipo matangazo ya vituo visivyolipiwa (local channels). Miongoni mwa channels zinazotakiwa kuonyeshea bure kwa mujibu wa sheria ni Televisheni ya Taifa (TBC1).

TBC1 kama ilivyo vituo vyote vya televisheni vya Taifa vya kila nchi walipewa haki ya kuonyesha baadhi ya mechi za FIFA World Cup bure. Kituko cha hawa Startimes ni kuwa wakati wa mechi huwa wanaizuia TBC1 kwa wale ambao hawajalipia ada za mwezi. Hivi ni kinyume kabisa na sheria.

Ninaanini kabisa kuwa mamlaka husika kupitia TCRA wanafahamu uhuni na ukiukaji huu wa sheria wa Startimes lakini kwa sababu zisizojulikana wanaachia tu! Hivi inakuwaje TCRA wanaachilia ukiukaji huu wa sheria? Wajibu wao nini? Ina maana TCRA wanasubiri tulalamikie ndio wachukue hatua? TCRA kazi imewashinda? Haki zetu za kutazama TBC1 bure zinaporwa na TCRA mnashudia.

Vv
 
Acha upotoshaji, tumeangalia mpaka fainali na hatujawahi kulipia tangu mwezi wa Saba huko. Sometimes fault connection au bad weather inafanya kinga'amuzi kisome tofauti lakini Kwa hili la MALIPO umedanganya.
 
Unapenda kamserereko
Ninavyo visimbuzi vya kampuni 3 tofauti, sina sababu ya kulioia vyote. Isitoshe TBC1 sio ya kulioia, ni free, au wewe unalipia TBC1?

Pili, hyo sio hoja, hoja ni sheria kuzingatiwa na uwajibikaji.

Vv
 
Back
Top Bottom