Kwanini kwenye kubadili Passport hakuna foleni kama NIDA licha ya kesho kuwa siku ya mwisho?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,581
15,350
Wakuu nimekuwa nikifuatilia jamaa wanasema hakuna foleni kabisa wala msongamano kihivyo.

Najiuliza:
Je, sisi wabongo mambo ya kusafiri nje sio hobby yetu?

Swali lingine la uzushi, hawa Idara ya Uhamiaji kwanini eti ili Mtanzania apate Passport lazima awe na kama sababu au ushahidi wa huko anakokwenda?

Kwanini isingekuwa tu kama vitambulisho vya taifa, maana kila mtu anaweza kwenda mahali popote wakati wowote kutegemeana na fursa.
 
Hivi nchi nyingine unachukua pass kama nyanya?? Hawaulizi vidhibitisho na ushahidi wa uendako?
mkuu sijui,
Maana wengi huwa wanatumia uongo tu ili waipate ( safari) kabla ya safari.
Sina uelewa mnene wa mambo ya passport na sīu nikiwa nataka kwenda majuu ntafuata procesure, ila kwa mtazamo wangu wakikulima nilipaswa kuimiliki tu ili ikitokea nasonga mbele siendi kuomba tena huko.

Mfano Graduate yoyote ilipaswa awe na pasport bila kujali anauhakika wa safari au la, maana ameshakuwa raia wa dunia anaweza kwenda hata nje ya nchi akipata kazi.

kuna kama kaurasimu flani, alafu ni kama kuhalalisha watu watumie uongo ili wapate kitu halali (wanaotegemea kupata mwanya wa kwenda nje ila bado hawana mchongo na wanataka passport)
 
wakuu nimekuwa nikifuatilia jamaa wanasema hakuna foreni kabisa wala msongamano kihivyo.

Najiuliza
Je, Sisi wabongo mambo ya kusafiri nje sio Hobi Yetu?

Swali lingine la uzushi, hawa uhamiaji kwa nini eti ili mtanzania apate passport lazima awe na kama sababu au ushahidi wa huko anakokwenda?
Kwa nini isingekuwa tu kama vitambulisho vya taifa, maana kila mtu anaweza kwenda mahali popote wakati wowote kutegemeana na fursa.
PAASPORT ILI USAFIRI KWENDA KIBITI AU NAMTUMBO HE HE
 
wakuu nimekuwa nikifuatilia jamaa wanasema hakuna foreni kabisa wala msongamano kihivyo.

Najiuliza
Je, Sisi wabongo mambo ya kusafiri nje sio Hobi Yetu?

Swali lingine la uzushi, hawa uhamiaji kwa nini eti ili mtanzania apate passport lazima awe na kama sababu au ushahidi wa huko anakokwenda?
Kwa nini isingekuwa tu kama vitambulisho vya taifa, maana kila mtu anaweza kwenda mahali popote wakati wowote kutegemeana na fursa.

Foleni zilikuwa mwaka jana - mwezi wa June na July - mara walipotangaza kuwa hatuwezi kusafiri na passport ambazo muda wa kuisha umebakia miezi sita. Uhamiaji makao makuu kulikuwa ni balaa. Hivyo watu wengi wanaosafiri walibadili mwaka jana.
 
asante sana.
ungekuwa china ningekuambia akiza supu ya popo
Hata Wapemba wanakula popo. Tena popo wa kwao wale wakubwa na wana "species" fulani ya popo ipo Pemba tu haipatikani kwengine duniani.

Safiri sana utaelimika sana kuliko uliyosomeshwa shule zetu za kusomea ujinga.
 
Foleni zilikuwa mwaka jana - mwezi wa June na July - mara walipotangaza kuwa hatuwezi kusafiri na passport ambazo muda wa kuisha umebakia miezi sita. Uhamiaji makao makuu kulikuwa ni balaa. Hivyo watu wengi wanaosafiri walibadili mwaka jana.
nyie jamaa mnaosafiri nchi za mbali huwa mko makini sana hata kama ni divison zero au hajawahi kukanyaka shule.
wengi wanaakilijanja.

ila sisi wamatumbi Utatuona NIDA tunavyopambana na Deadline ili tusajiri simu huku hata kitambulisho sio kipaumbele.
 
wakuu nimekuwa nikifuatilia jamaa wanasema hakuna foreni kabisa wala msongamano kihivyo.

Najiuliza
Je, Sisi wabongo mambo ya kusafiri nje sio Hobi Yetu?

Swali lingine la uzushi, hawa uhamiaji kwa nini eti ili mtanzania apate passport lazima awe na kama sababu au ushahidi wa huko anakokwenda?
Kwa nini isingekuwa tu kama vitambulisho vya taifa, maana kila mtu anaweza kwenda mahali popote wakati wowote kutegemeana na fursa.
Boss, pengine unazungumza kwa kusikia tu, juzi na jana nilipita maeneo yale, nikaona mtu ameshika fomu yenye nambari 383 saa 5 kasoro asubuhi.

Alifanikiwa kufanya finger print na picha saa 11 jioni, na hapo ni kwamba, wazee, wajawazito, wenye watoto chini ya miaka 4 na wagonjwa walikuwa wanaitwa kwa kuzingatia hali zao. Pengine kwa siku mbili tu pale HQ, walipokea zaidi ya maombi 2000, bado hujafuatilia maombi ya kutoka wilayani.
 
Watanzania watu wa ajabu Sana, wanaomiliki passport record za uhamiaji zinasema nitakribani laki tisa, ambao mpaka Leo ikiwa imebaki siku moja ya hitimisho LA kutumia passport za awali, walibadilisha ni laki mbili tuu. Sasa utashangaa wiki ijayo watakavyo jazana uhamiaji
 
Naomba kujuzwa mahitaji ambayo ni lazima uwe nayo ili ufikie vigezo vya kubadilishiwa Passport.
Kuna wanaosema lazima uwe na 150,000/=.
Je, ni kweli?
 
Langu nje ya mada kidogo...
Hivi mtoto wa chini ya miaka 18, anaruhusiwa kujiandikisha/kuandikishwa ili apate kitambulisho cha uraia..??
 
Boss, pengine unazungumza kwa kusikia tu, juzi na jana nilipita maeneo yale, nikaona mtu ameshika fomu yenye nambari 383 saa 5 kasoro asubuhi.

Alifanikiwa kufanya finger print na picha saa 11 jioni, na hapo ni kwamba, wazee, wajawazito, wenye watoto chini ya miaka 4 na wagonjwa walikuwa wanaitwa kwa kuzingatia hali zao. Pengine kwa siku mbili tu pale HQ, walipokea zaidi ya maombi 2000, bado hujafuatilia maombi ya kutoka wilayani.
wanasema ikifika saa kumi, wote waliopo watahakikisha wanahudumiwa.
nimesikia jamaa yao mmoja anajinadi redioni
 
Back
Top Bottom